Ex-Mayor alivyoumizwa na tukio la Kukatika Umeme kwa treni, inaumiza sana sana

Ex-Mayor alivyoumizwa na tukio la Kukatika Umeme kwa treni, inaumiza sana sana

FB_IMG_17224927920410614.jpg
 
NGEDERE NA BUNDI WAOKOA MABILLIONI YA PESA UNUNUZI WA TRENI ZA SGR.
 
NGEDERE NA BUNDI WAOKOA MABILLIONI YA PESA UNUNUZI WA TRENI ZA SGR.
IMG-20240731-WA0407.jpg

NGEDERE mmoja na BUNDI mmoja jana maeneo ya Kidete wilaya ya Kilosa ndiyo kalisanua TAIFA katika ufisadi ununuzi wa Treni za SGR.

Bila NGEDERE jana kufanya kazi nzuri ya "AUDITING" kwa kushirikiana na Bundi,taifa lingekuwa limetapeliwa na TRC chini ya Mkurugenzi wake Bwana KADOGOSA ambaye alisema Treni hizo zinatumia Umeme na Mafuta.

Lakini katika ukaguzi ukifanywa na NGEDERE na BUNDI kutoka ofisi ya CAG ofisi ndogo za Kidete

Bundi jana majira ya saa 2 kwenda saa 3 usiku, alifanikiwa kukaa Juu ya mti mrefu sana na Kuliona Treni la SGR likiwa linatoka Station ya Kilosa kuja Kidete.

BUNDI aliwasiliana na NGEDERE kwa haraka sana,kwa ajili ya ukaguzi wa kutizama "Value for Money" katika ununuzi wa Treni hizo ambazo Taifa liliambiwa zinatumia Umeme na Mafuta.

NGEDERE alifanikiwa kufyatua Nyaya za umeme pasipo kuharibu miundo mbinu ya TANESCO, na hatimaye umeme ukajizima na kurudi kituo cha kupooza umeme cha Godegode.

NGEDERE na BUNDI wanasema walishangazwa na Kuona Treni hiyo ya SGR kuganda kwa masaa 4 na nusu bila kuwasha mfumo wa Mafuta na kuendelea na Safari kuelekea Dodoma.
Wala siyo 2 na nusu kama wanavyosena TRC walivyosema jana

Wakitoa Ripoti ya Ukaguzi wa Treni za SGR NGEDERE amewataka Watanzania kujenga tabia ya kuwa wadadisi kama wao na siyo Kukubali kila taarifa zinazotolewa na Serikali.

BUNDI naye aliongeza kwa kusema kuwa Kama tulilipa pesa ya Kununua Treni za Umeme na Mafuta na zikaja hizi ambazo Umeme ukikatika zinaganda kwakuwa hazina mfumo wa Mafuta basi TRC na Mzabuni aliyetuuzia Treni hizi za SGR arudishe chenji kwa Taifa kabla hatua za Kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Mwisho NGEDERE na BUNDI wamewataka Watumishi na Watendaji wa Serikali kuwa makini na kazi zao,kwakuwa ukaguzi huu wa Kushtukiza utaendelea katika miradi mbalimbali ya serikali mikubwa kwa ajili ya kulinda kodi za Watanzania ambao wamezubaa na hawajitambui.!!
 
Sio muda wa Kukejeli Mradi...tuwe na Uzalendo kama 🇹🇿 🇹🇿
Yawezekana Mazingira ya nchi yetu yakawa ni changamoto katika Kutekeleza mradi.. Mazingira ya Nchi yetu ni tofauti na Mazingira ya nchi za Ulaya hasa Misitu / Wanyama
Hapa Nashauri Wasomi wa Vtuo Vikuu Animal Scientists; Ecologists kutoka vyuo vya SUA; udsm washirikishwe ni jinsi gani Wanaweza Kuzuia Hawa Wanyama kuletA Uaribifu kwenye Huo Mradi
Tuwe na Constructive ideas kuliko kuanzA kutoa Kejeli kuonesha kila kitu kinachofanyika basi hakina Manufaa..
Au kutaka Watu watumbuliwe..
Tupende kuwekeza kwenye Uchunguzi ( Investigation) na kuja na Ufumbuzi wa Matatizo yetu
 
Back
Top Bottom