Brodre
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 2,585
- 1,771
Unaweza kukwepa matone ya mvua lakini siyo kamera za Global Publishers Ltd, zinapoamua kukufanyia kazi, ukibisha waulize Nasibu Abdul &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Diamond' na mke wa mtu, Irene Uwoya.
Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za hali ya juu kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu, walinaswa na kamera za Global kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda, linathubutu kwa kuwa lina ushahidi wa kutosha kutamka kwamba Diamond na Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, waliingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.
=========
heaven on desert hapa unasemaje mkuu... Bwana mdogo ashaanza kula mke ya mtu?