EXCLUSIVE: Download Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya hapa na toa maoni

EXCLUSIVE: Download Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya hapa na toa maoni

Ok, thus good mkuu, muda wote nimekuwa najiuliza nitaipataje hii document kwenye soft copy, sasa umetibu kiu yangu, stay blessed ndg MMASSY.

Amang'ana mbuya ghale.
 
Last edited by a moderator:
Rasimu ni taaaam sana najisikia kama TZ na TZ Bara inakuwa mpya yenye mafanikio makubwa sn kwa siku zijazo, naona mafaniko makubwa yaja kwa wa TZB, tunamshukuru Mungu sn kwa kuwawezesha wazee wetu kutuwekea nchi katika mikono salama, tunamuomba Mungu awape uhai waone matunda ya kazi yao.

Viva Warioba, Viva Salim kazi yenu ni njema tunaamini ss TZ kutakuwa mahala pakukimbilia kama Marekani na mahala pengine duniani.
 
thanx all members mliotoletea rasimu hii naamini watanzania wengi hawakutegemea hili kwani tulidhani ni siasa tuu...thanx god
 
Wakubwa shikamooni!

Nimeridhishwa na maeneo mengi katika rasimu ya katiba hasahasa mfumo utakaotumika kuwapata viongozi wataoteuliwa na Rais pia suala na idadi ya mawazir ni zuri. Kwa upande wa serikali 3 ndugu zangu tufikirie mara mbili litatugharimu sana katika utekelezaji wake, wazanzibar na wachache mno itakuwa ni kama tunamlea mtoto kwa kumdekeza.

Hebu tufikirie taifa lenye watu milioni 50 linakuwa na marais watatu, makamu wa Rais watano, mawazir wakuu 3. Hii sio haki Serikali 2 hizi au 1 zinatutosha sana bado hatuna uchumi wa kuhimili lundo la vyeo. Nachelea kuunganisha na ile kaul ya Rais kuwa wattengeneza ajira nyingi
 
Kimsingi nimependa sana sehemu inayozungumzia Haki za Msingi inatoa mwanya wa kusimamia utungwaji wa sheria sera na utekelezaji unaozingatia haki za msingi za binadamu.

Hongera sana Tume. Sipati picha Utawala mpya au seriali mpya inayokuja kama si muadilifu ni mbabaishaji kama baadhi ya Viongoi wangu wa CCM kazi wanayo hakuna atakaedumu.
 
Nina kushukuru sana, nami ninawatumia na wengine wenye uhitaji na nafasi ya kuusoma! ASANTE JF pia.
 
Nimeinyonya yote,naipitia taratiibuu kabisa...

Raha sana,ha ha ha,,kweli jamii forum yatoshaa...!!
 
Nimependa sana kipengele kinachodhibiti idad ya wabunge kuwa 75 tu na mawazir 15 tena kwa ku-apply.. coz kwa muda mrefu nchi ye2 imekuwa na kundi kubwa la wanasiasa Wachumia tumbo.. mambo meng yamesemwa wengine huingia bungeni kwa hongo za ngono, kurith nk..!

wengine wamekuwa wabunge for 35yrs plus.. thank to God wote tufanye kaz kwa bidii waache kula mgongoni kwetu! VIVA ..WARIOBA!
 
Nimesoma hadi ukurasa wa 40 Haya ndo mnisaidie.

Katiba haijasema mda specific wa kumpeleka mtu mahakamani inasema apelekwe mapema iwezekanavyo! Hii tunarudi kulekule mtu atawekwa hadi mwezi kwao wao ni mapema!

Kwenye muundo wa serikali kwanini Tanzania bara na si TANGANYIKA?

Katika uteuzi Rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha
siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi. HAPO VIP?
 
Mungu ibariki JF!

Awali ya yote napenda kutumia fursa hii kumpongeza Mhe.Jaji Warioba na watanzania wote kwa ujumla, hatimaye matakwa ya Watanzania kuhitaji mabadiliko ya katiba yameanza kuzaa matunda kupitia rasimu iliyozinduliwa na Makamu wa Rais siku ya jana.Pia napenda kupongeza asasi za kiraia, taasisi za kidini na vyama vya upinzani haswa CHADEMA kwa kuongoza maandamano mara kadhaa kwa lengo la kudai katiba mpya mnamo mwaka 2011 bila kusahau ilani ya uchaguzi ya 2010.

Pia natambua mchango wa CUF, NCCR,TLP,UDP n.k katika harakati za kudai katiba mpya tangu mwaka 1995. Maoni yangu kuhusu uwakilishi wa asilimia 50/50 baina ya wanawake na wanaume katika majimbo haujazingatia kanuni ya asili na kiini cha hoja.

Je, kila mbunge atakuwa anawakilisha matatizo na hoja za jinsia yake? Je, huku si kuimarisha ubaguzi wa kijinsia? Je, si kuongeza expenditure kwenye mishahara? Mfumo uliopo unamakosa?
 
Wadau kwa nini katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Upande mmoja wa muungano usomeke SERIKALI MAPINDUZI YA ZANZIBAR na upande wa pili usomeke SERIKALI YA TANZANIA BARA badala ya SERIKALI YA TANGANYIKA?

Ugumu wa sintofahamu unakuja pale nikifuatilia asili ya jina TanZan+IA = TANZANIA yaani kwenye TANGANYIKA ikachukuliwa TAN na kwenye ZANZIBAR ikachukuliwa ZAN kisha kikaongezwa kiungo cha AI chanzo kikiwa mimi sikijui kilitoka wapi.

Sasa kama fuatilia surah ii ya sita uone jinsi tunavyotaka kuingizwa chaka la Mabwepande huku tukiwa tunajijua.....................

SURA YA SITA
MUUNDO WA JAMHURI YA MUUNGANO
Muundo wa
Muungano
57.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye
serikali tatu ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanzania Bara.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo
Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa
katika Katiba za Washirika wa Muungano.

Vyombo
vya utendaji
vya Jamhuri
ya
Muungano
58.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa ndiyo chombo
chenye mamlaka ya utendaji, Bunge litakuwa na mamlaka ya kutunga sheria
kwa mambo ya Muungano na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama itakuwa ni chombo cha utoaji haki.
(2) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza
majukumu yake kwa kufuata masharti ya Katiba hii.

Mamlaka
ya Serikali
ya
Muungano
59.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya
utekelezaji kwa mambo yote yaliyoorodheshwa kuwa Mambo ya Muungano, na
wakati inapotekeleza majukumu yake, itazingatia mamlaka yake iliyopewa chini
ya Katiba hii.
(2)Utekelezaji wa majukumu ya Serikali utafanywa kwa namna na kwa
misingi iliyowekwa na Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge.
(3) Bila ya kuathiri aukukiuka masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri
ya Muungano, kwa makubaliano na masharti maalum baina yake na Serikali ya
Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara, inaweza kutekeleza jambo lolote lililo
chini ya mamlaka ya Serikali ya Zanzibar au Serikali ya Tanzania Bara kwa
mujibu wa masharti ya makubaliano hayo.

Mambo ya
Muungano
60. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo
baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara ya 58, Serikali ya Muungano
itakuwa na mamlaka juu ya mambo ya Muungano yalivyoorodheshwa katika
Nyongeza ya Katiba hii.

Washirika
wa
Muungano
61.-(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Washirika wa Muungano ni
Tanzania Bara na Zanzibar.
(2) Serikali ya Tanzania Bara itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote
yasiyo ya Muungano yahusuyo Tanzania Bara.
(3) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka juu ya
mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
(4) Washirika wa Muungano watatekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Washirika wa Muungano watakuwa na hadhi na haki sawa ndani
ya Jamhuri ya Muungano na watatekeleza majukumu yao kwa masuala yote
yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Washirika wa Muungano kwa
mujibu wa masharti yatakayowekwa na Katiba za Washirika wa Muungano.

Mamlaka
ya
Washirika
wa
Muungano
62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote
juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka
hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano na
mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawakwa ajili ya ustawi ulio bora
kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.
(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika wa
Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au
ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo
yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa
Muungano.
(3) Mshirika wa Muungano anaweza, wakati wa kutekeleza majukumu
yake chini ya Ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au
taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza
kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika.

Mahusiano
kati ya
Washirika
wa
Muungano
63.-(1) Kila Mshirika wa Muungano anaweza, katika kutekeleza
majukumu yake katika maeneo mbalimbali, kutekeleza majukumu hayo
kwa misingi ya kushirikiana na kushauriana na Mshirika wa Muungano
mwingine au baina ya Mshirika wa Muungano na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano kwa lengo la kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo
ya wananchi.
(2) Washirika wa Muungano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wanaweza kushauriana na kushirikiana katika mambo ya uongozi, utawala,
vyombo vya uwakilishi na kimahakama.
(3) Utendaji wa Serikali za Washirika wa Muungano au wa chombo
chochote kati ya vyombo vya serikali hizo na uendeshaji wa shughuli,
utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na nia na
umuhimu wa haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya
Taifa.

Mawaziri
Wakaazi
64.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atateua Waziri Mkaazi
atakayeratibu na kusimamia mahusiano baina ya Serikali za Washirika na
kati ya Serikali ya Mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2)Mawaziri Wakaazi watakuwa na ofisi zao na watafanya kazi
wakiwa Makao Makuu ya Serikali ya Muungano.
(3) Pamoja na majukumu mengine watakayopangiwa na Serikali
za Washirika wa Muungano, Mawaziri Wakaazi watakuwa na majukumu
yafuatayo:
(a) kushughulikia mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu
ushirikiano au mahusiano ya kimataifa; na
(b) kuwa kiungo baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
Serikali za Washirika wa Muungano na baina ya Serikali za
Washirika wa Muungano.

Mamlaka ya
wananchi
65.-(1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapata mamlaka yake
kutoka kwa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa
na kusimamiwa na chombo kitakachopewa mamlaka na Katiba hii, na
vilevile, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
zitapata mamlaka kupitia uchaguzi wa kidemokrasia utakaoendeshwa na
kusimamiwa na vyombo vitakavyopewa mamlaka chini ya Katiba zao.

(2) Serikali za Washirika wa Muungano, katika kutekeleza
mamlaka zao, zitawajibika kustawisha mamlaka ya wananchi kwa kugatua
madaraka kwa serikali za mitaa zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Bara au Katiba ya Zanzibar, kama itakavyokuwa

66.-(1) Bila ya kuathiri wajibu wa kila raia kwa mujibu wa Katiba
hii, viongozi wakuu wenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya
Muungano waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3) watawajibika, kila mmoja
wao katika kutekeleza madaraka waliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii au
Katiba za Washirika wa Muungano kuhakikisha kuwa analinda, kuimarisha
na kudumisha Muungano.

(2) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara ndogo ya (1), kila
mmojawapo wa viongozi wakuu waliotajwa katika Ibara ndogo ya (3),
kabla ya kushika madaraka yake ataapa kuutetea na kuudumisha
Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi Wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Tanzania Bara; na
(d) Rais wa Zanzibar.
 
Tutoeni maoni kwenye mabaraza ya kata kwamba tunataka ISOMEKE Tanganyika badala Tanzania bara. Kwasababu haijawahi kuwepo nchi inayoitwa Tanzania bara. CCM lazima wakubali hii FACT.
 
Wakuu natumia simu mbona nimeshindwa kuipata hii rasimu?msaada taf.
 
Tutoeni maoni kwenye mabaraza ya kata kwamba tunataka ISOMEKE Tanganyika badala Tanzania bara. Kwasababu haijawahi kuwepo nchi inayoitwa Tanzania bara. CCM lazima wakubali hii FACT.

Hapo ndo ninapoumia na kuchanganyikiwa kwa nini hawataki isomeke TANGANYIKA????????
 
Back
Top Bottom