RASMI: Ibrahim Ajibu ametua Yanga
ShaffihDauda / Dick Dauda / 36 minutes ago
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib Migomba βmiguu ya dhahabuβ rasmi anajiunga na Yanga baada ya klabu yake ya sasa kushindwa kufikia nae makubaliano ya kumbakiza kwenye kikosi.
Taarifa ambazo
www.shaffihdauda.co.tz inazo ni kwamba, Ajab na uongozi wa Simba hawakufikia makubaliano hivyo nyota huyo akaamua kwenda upande wa pili (Yanga) ambao nao walikua wanamfukuzia tangu kitambo.
Kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe kwenye mtandao huu amesema, walijaribu kukaa na Ajib kwa ajili ya mazungumzo ili andelee kubaki Simba lakini mchezaji huyo hakuonekana kuwa tayari kubaki Msimbazi kutokana na kiwango cha pesa alichokua akikihitaji.
βTumemwacha aende anakotaka kwenda kwa sababu hana βspiritβ tunayoihitaji sisi, acha aende tu sisi mbele kwa mbele,β amesema boss huyo.
Jana Jumatano Juni 14, 2017 mtandao huu ulitoa story kuhusu ofa tatu alizokuwanazo Ajib ambazo zilikuwa ni kutoka Simba, Yanga na Singida United ambapo Singida ndio ilikua timu yenye dau refu kuliko Simba na Yanga lakini Ajib alikuwa na wasiwasi kwenda Singida kutokana na kuhofia maisha yake ya baadae katika soka.
Ajib ambaye alianza kutamba Simba akitokea kikosi cha vijana alikuwa mchezaji huru baada ya kuhitimisha mkataba wake ndani ya Simba