Exclusive. Hatimaye Yusuph Manji amerejea rasmi Yanga na amemsajili Ibrahim Ajib

Mbona taarifa za jana zinasema simba ilimalizana na Ajib na Mkude???

Wewe wa wapi Mkuu? Yaani unaongelea ya jana wakati ni hivi punde tu Ajib ameshamalizana na Yanga na huenda kati ya Kesho hadi Jumapili Mkude nae akajiunga na Yanga! Kumbe mlidhani kuwa GENTAMYCINE natania tu au nimeamua tu Kujichetua na kuwapeni hii taarifa ambayo kitalembwa ( Mtangazaji wa Efm Oscar Oscar ) alidhani nimeitoa katika Radio yao ya Efm huku akisahau kuwa Yeye ni Mtoto mdogo mno Kwangu hasa katika uwezo wa kupata taarifa zile nyeti kabisa au muhimu. Yaani Mimi kabisa na Utaalam na Ufundi wangu niitegemee Efm kunipa News Tip? Ana bahati sitomchamba kwakuwa namjua ni mwana Simba SC mwenzangu ila angekuwa ni mwana Yanga FC nadhani angejuta kunifahamu.
 
Ajib alitakiwa atazame soka la kulipwa,kwenda yanga ni kwenda kuua kipaji chake kama ilivyomtokea Kaseke.
 
hahahaaah sawa mkuu. So Ngoma na Niyonzima nao ni uhakika Simba????
 
unasiliza radio unakuja kujifanya eti habr za chini chini! umeshindwa nini kuweka wazi chanzo cha hbr ?

Umejipanga lakini kutaka majibizano na Mimi? Hili ni ONYO langu la mwisho Kwako. Si jukumu lako Wewe kunitaka Mimi niweke bayana Source ila kwa mapenzi yangu makubwa kabisa kwa mtandao huu wa JamiiForums mwenyewe nimeamua kuisaka hii taarifa kisha Kiupendo kabisa wa JF nikaileta humu ili ikijulikana basi Credits zote ziende kwa JamiiForums. Silipwi chochote na JF ila naupenda mno huu Mtandao na kuna wakati hadi nasikia tu raha Mimi kama Mimi kutafuta taarifa zangu za Kiuchunguzi kisha nazileta humu JF ili zianzie kujulikana humu.

Na ili nikuonyeshe kuwa Wewe bado ni Mtoto mdogo mno Kwangu na najiamini halafu napenda kile ninachokifanya Kesho nakuja na taarifa yangu ya Kiuchunguzi kabisa na Kashfa moja nzito ya Kijamii inayoihusu Kituo cha Mabasi ya Dalala cha Ubungo Simu 2000 halafu Jumamosi nakuja na taarifa yangu nyingine kabisa na matukio yanoyotokea mara kwa mara Mlima Nyoka Mbeya na kwa Kiasi gani Watu fulani wenye Mamlaka wanahusika.

Huyu ndiyo GENTAMYCINE a.k.a Talented and Charismatic a.k.a l'animateur maestro. Ndiyo Kwanza umekuwa Member hivyo jitahidi kwanza uje kuwa Senior Member kisha ndipo uje utufikie Majabali tuliotukuka kabisa akina JF - Expert Member.
 
Simba nadhani wamejutia sana kumpoteza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…