charty
JF-Expert Member
- Oct 28, 2013
- 7,460
- 5,992
Mie nimewaza sana juu ya huyu kijana.Bora mwili wake ungepatikana tu uwe mfu au hai ili ndugu zake waache kusononeka. Ben ni fumbo kwakweli.Nimemkumbuka ghafla Ben Saanane.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mie nimewaza sana juu ya huyu kijana.Bora mwili wake ungepatikana tu uwe mfu au hai ili ndugu zake waache kusononeka. Ben ni fumbo kwakweli.Nimemkumbuka ghafla Ben Saanane.
Lakini Msando sikuona sababu ya yeye kusema wazi kwenye media kuwa hakuna atakaye ingilia mfumo wa matokeo labda akatwe kiganja....Kwangu mimi niliona kama alikuwa amewapa mbinu wauwaji kabisa na zile zilikuwa tambo zisizo na msingi na hapa kusema kweli kabisa ndipo niliamini hakuna kitu kinaitwa Tume huru...
Kama mtu alipata wasaha kutazama mahojiano ya Msando atagundua kabisa kuwa alikuwa na upande wake na ndio maana alikuwa anaweka tambo na katika maongezi yake alionesha wazi kabisa uchaguzi uliopita uliingiliwa na wazi alikuwa ana watuhumu Jubilee...
Kwa hiyo Msando angeliweza kuhakikisha hakuna anaye ingilia mfumo wa matokeo kwa kuonesha vitendo na sio lazima kuweka tambo na kuonesha jinsi ambavyo wanaweza kuingilia matokeo...hilo ni kosa alilo lifanya pale kwenye usaili wake.
Halafu Kifo chake kina utata sana maana upande wa pili ule unaweza kuwa umetekeleza hii mission ili kuonesha kuwa wahusika ni watu fulani na kuhalalisha kuwa kura zimeibiwa na kabla ya kifo chake NASA walisema wamegundua kuna mpango wa wizi wa kura sasa najiuliza kwanini wasiwe NASA wame usika kwenye hili jambo ili kuthibitisha madai yao kuwa kuna mpango wa wizi wa Kura?
Halafu ni jana tuu NASA wamehoji usalama wa Kura zao baada Msando kuuwawa...
Bado naamini kuna mengi sana nyuma ya kifo cha Msando.
Maelezo yako mbona yana hitimisha kuwa kuwa Jubilee ndio wamehusika? Kwanini si NASA kwa kutafuta public sympathy kupitia mgongo wa Kura kuibiwa na kuingiza nchi kwenye machafuko? NASA hata kabla ya kupotea kwa msando walileta story za kuibiwa kura na hata baada ya Msando kupatikana ndio wameonesha wazi kuwa hawana imani na mfumo wa matokeo ,,,,Kwanini sio kwamba hili jambo limepangwa ili kuonesha ulimwengu kuwa Kura zinaibiwa?Ni kweli alikuwa na upande ambao ni upande wa haki kitu kinachoendana na kiapo chake. Mawazo yako yanafikirisha lakini yamekaa 'kikwenu' zaidi. Nadhani upumbavu wetu waafrika na madikteta wengine duniani katika ujasiri wa kuiba kura ungeelekezwa katika ujasiri wa kuwatangazia wananchi kuwa "hatuna haja ya uchaguzi" ingelikuwa na maana zaidi kuliko kupoteza muda na watu muhimu!
Tunaweza tusiwe na uhakika lakini haina shaka kifo cha huyu bwana kilipangwa. Wakenya wakitafuta uongozi UTU huwaondoka kabisaaa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi kutopewa Ulinzi haraka hakufanyi hitimisho kuwa Jubilee ndio wahausika maana wengine tunaweza kusema kuwa NASA wametumia huu mwanya kummaliza ili kuonesha na kuthibitisha kuna wizi wa kura....Kwa nini uwaze NASA wakati JUBILEE ndio walitakiwa watoe uLINZI KWAKE NA HAWAKUFANYA hivyo
kwangu mimi hii soo ni ya bwana RUTTO na U.K
Ndio maana nasema hivi kwenye mauaji yake kuna maswali wengi.... Halafu hivi kama kiganja kikikatwa finger print itafanya kazi? Hivi finger print haitegemei mzunguzo wa damu?Habari ya wauaji kukata kiganjia siyo kweli. Mwili umepatikana na mikono yote miwili ila inayo majeraha ya kisu.