mputamaseko
JF-Expert Member
- Apr 1, 2013
- 1,401
- 949
Nahisi atakuwa ameponzwa na maneno kutoka katika kinywa chake. Either way R.I.P# Hii ndio Africa the DARK continent in the Universe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakenya hawana mshipa wa aibu. ...uhuruto? au Ramusyo?
Maelezo yako mbona yana hitimisha kuwa kuwa Jubilee ndio wamehusika? Kwanini si NASA kwa kutafuta public sympathy kupitia mgongo wa Kura kuibiwa na kuingiza nchi kwenye machafuko? NASA hata kabla ya kupotea kwa msando walileta story za kuibiwa kura na hata baada ya Msando kupatikana ndio wameonesha wazi kuwa hawana imani na mfumo wa matokeo ,,,,Kwanini sio kwamba hili jambo limepangwa ili kuonesha ulimwengu kuwa Kura zinaibiwa?
Mimi bado nina wasi wasi kabisa na pande zote kuhusika........maana mazingira ya kifo cha Msando bado kina waweka kwenye mashaka pande zote mbili kuhusika...
Tusisahau na kwetu Kibiti mkuu,..Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IECB Bwana Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ' Kitaarifa ' zaidi kutoka kwa ' Wadau ' mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ' Wabobezi ' wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea Kifo hiko cha ' Kikatili ' kabisa.
Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu zilizopita kabla ya hayo ' Mauaji ' yake ya ' Kikatili ' kutokea hivyo nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ' tathmini ' mwenyewe ' Kimoyomoyo ' kisha mwishoni wote tutajua ni nani ' Kamuua ' Marehemu Chris Msando.
Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa ' Oparesheni ' za IECB alijibiwa na kupewa ' Ushirikiano haraka sana.
Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa za Yeye ' Kutishiwa ' maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ' Ulinzi ' aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.
Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ' Onyo ' kali la kutozungumza na Chombo chochote cha Habari nchini Kenya na ' Mamlaka ' na kuambiwa kwamba Mtu pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa Habari na Mawasiliano.
Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ' alikaidi ' hiyo amri kutoka katika ' Mamlaka ' ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ' mauaji ' yake.
Tukio #5.
Wakati akiwa ' mubashara ' kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha Habari Marehemu alisikika ' akiwahakikishia ' Wakenya wote kuwa kwa jinsi alivyotengeneza ' Mfumo ' wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ' Kuudukua ' hata iweje na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ' hack ' taarifa zozote za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ' Kiganja ' chake kwani ili upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ' Kiganja ' chake cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.
Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ' Kimafia ' na labda pengine alijisahau kuwa siku zote ukitaka tu ' Kuuawa ' Kimafia basi Mtu wako wa Karibu sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ' Mwanamke ' ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ' Mwanamke ' kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ' Kimafia ' ndipo akamtega Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ' Wauaji ' wake wale ' Mafia ' walikuwepo.
Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ' Wauaji ' wake wa ' Kimafia ' walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ' Udukuzi 'wowote utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ' chake ndipo hata katika ' mauaji ' yake ya juzi ' Kiganja ' chake cha Mkono ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ' Wauaji ' na kuuacha mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.
Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule ambaye atakuwa kafanikisha ' mauaji ' ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi wote kitu ambacho ' Wauaji ' hawa walikifanya kwa ' Kumuua ' na Yule Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ' Mission Accomplished '.
Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ' Muuaji ' Mkuu wa Marehemu Chris Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ' Ushirikiano ' mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ' wamechoka ' na haya mauaji ya ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti.
Nawasilisha.
Habari ya wauaji kukata kiganjia siyo kweli. Mwili umepatikana na mikono yote miwili ila inayo majeraha ya kisu.Picha Zipo mtandaoni ,kwa sababu za kimaadili siwezi kuzirusha hapa.
Sio wakenya tu,... Humu ndani mwako yanayofanyika ni makubwa saaana.... Mambo yanafanywa kimya kimya na kawaida ya watanzania ni wasahaulifu saaana, sijui tuna tatizo gani!Tunaweza tusiwe na uhakika lakini haina shaka kifo cha huyu bwana kilipangwa. Wakenya wakitafuta uongozi UTU huwaondoka kabisaaa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi kutopewa Ulinzi haraka hakufanyi hitimisho kuwa Jubilee ndio wahausika maana wengine tunaweza kusema kuwa NASA wametumia huu mwanya kummaliza ili kuonesha na kuthibitisha kuna wizi wa kura....
Lakini Msando sikuona sababu ya yeye kusema wazi kwenye media kuwa hakuna atakaye ingilia mfumo wa matokeo labda akatwe kiganja....Kwangu mimi niliona kama alikuwa amewapa mbinu wauwaji kabisa na zile zilikuwa tambo zisizo na msingi na hapa kusema kweli kabisa ndipo niliamini hakuna kitu kinaitwa Tume huru...
Kama mtu alipata wasaha kutazama mahojiano ya Msando atagundua kabisa kuwa alikuwa na upande wake na ndio maana alikuwa anaweka tambo na katika maongezi yake alionesha wazi kabisa uchaguzi uliopita uliingiliwa na wazi alikuwa ana watuhumu Jubilee...
Kwa hiyo Msando angeliweza kuhakikisha hakuna anaye ingilia mfumo wa matokeo kwa kuonesha vitendo na sio lazima kuweka tambo na kuonesha jinsi ambavyo wanaweza kuingilia matokeo...hilo ni kosa alilo lifanya pale kwenye usaili wake.
Halafu Kifo chake kina utata sana maana upande wa pili ule unaweza kuwa umetekeleza hii mission ili kuonesha kuwa wahusika ni watu fulani na kuhalalisha kuwa kura zimeibiwa na kabla ya kifo chake NASA walisema wamegundua kuna mpango wa wizi wa kura sasa najiuliza kwanini wasiwe NASA wame usika kwenye hili jambo ili kuthibitisha madai yao kuwa kuna mpango wa wizi wa Kura?
Halafu ni jana tuu NASA wamehoji usalama wa Kura zao baada Msando kuuwawa...
Bado naamini kuna mengi sana nyuma ya kifo cha Msando.
Kumbe una akiliii zoteeLakini Msando sikuona sababu ya yeye kusema wazi kwenye media kuwa hakuna atakaye ingilia mfumo wa matokeo labda akatwe kiganja....Kwangu mimi niliona kama alikuwa amewapa mbinu wauwaji kabisa na zile zilikuwa tambo zisizo na msingi na hapa kusema kweli kabisa ndipo niliamini hakuna kitu kinaitwa Tume huru...
Kama mtu alipata wasaha kutazama mahojiano ya Msando atagundua kabisa kuwa alikuwa na upande wake na ndio maana alikuwa anaweka tambo na katika maongezi yake alionesha wazi kabisa uchaguzi uliopita uliingiliwa na wazi alikuwa ana watuhumu Jubilee...
Kwa hiyo Msando angeliweza kuhakikisha hakuna anaye ingilia mfumo wa matokeo kwa kuonesha vitendo na sio lazima kuweka tambo na kuonesha jinsi ambavyo wanaweza kuingilia matokeo...hilo ni kosa alilo lifanya pale kwenye usaili wake.
Halafu Kifo chake kina utata sana maana upande wa pili ule unaweza kuwa umetekeleza hii mission ili kuonesha kuwa wahusika ni watu fulani na kuhalalisha kuwa kura zimeibiwa na kabla ya kifo chake NASA walisema wamegundua kuna mpango wa wizi wa kura sasa najiuliza kwanini wasiwe NASA wame usika kwenye hili jambo ili kuthibitisha madai yao kuwa kuna mpango wa wizi wa Kura?
Halafu ni jana tuu NASA wamehoji usalama wa Kura zao baada Msando kuuwawa...
Bado naamini kuna mengi sana nyuma ya kifo cha Msando.
Uhuru na Ruto wako tayari kuuwa ili wabaki ikulu
Swali la kuuliza ,who stands to benefit from Chris Msando death?
Una hoja nzuri lakini hebu tujiulize na tujifikirishe kidogo tu hivi kati ya Jubilee na NASA na akina nani wana 100% ya ' Kutekeleza ' mauaji yao kwa kuyaratibu vizuri kwa msaada wa State Security Organs za Kenya? Mkuu hivi kwa mazingira haya tu ya Kifo cha ghafla cha yule Waziri Major General Nkaissery ambaye nae alikuwa akiongoza idara ' Nyeti ' na huyu wa jana Msando na naambiwa kuwa hivi leo mchana tena Msemaji wa Jeshi la Kenya ametoweka hajulikani alipo mara baada tu ya Kukubali kuwa baadhi ya ' Nyaraka ' za Siri za Uibiwaji wa Kura zilikuwa zinaratibiwa moja kwa moja na Jeshi la Kenya ( KDF ).
Sasa kama Marehemu Msando ' kauliwa ' hadi kukatwa ' Kiganja ' chake nahisi huyu wanaweza wakamuua na wakakuta viungo vyake wamevitoa na kuvitandaza pembezoni mwa mwili wake. Nimetahadharisha na nazidi kutahadharisha kuwa kama ' Waangalizi ' wa uchaguzi huu wasipokuwa makini pamoja na nchi ' Washirika ' kukemea haya ' mauaji ' tutegemee Vita kubwa sana kuibuka nchini Kenya. Ukweli ni kwamba Kenyatta na Ruto hawatakiwi na Wakenya kwani wameharibu mno Uchumi wa Kenya lakini kama haitoshi wanasababisha ' mauaji ' yote haya ili kuwatisha Watu na hasa Watu wa Tume ( IECB ) ili waogope na kubwa zaidi hawataki akina Odinga na Musyoka wachukue nchi kwakuwa wanajua wakishinda tu ile Kesi ya akina Kenyatta na Ruto kule ICC the Hague itaibuliwa na hakuna ' ubishi ' wowote kwamba akina Kenyatta na Ruto walihusika kwa 100% na wanajulikana sana kwa ' Umafia '.
Kitengo cha ICT ni kigumu sana katika tume ya uchaguzi. Leo tunawasema wakenya ila tunasahau kuwa Mkurugenzi wa ICT wa Tume ya uchaguzi ya Tanzania Dk. Sisti Cariah mwaka 2015 aliondolewa kwenye nafasi yake siku 25 kabla ya uchaguzi na hadi leo hakuna maelezo kwamba alipelekwa/alihamishiwa wapi na kwa sababu gani.
Unapinga Nini Mkuu ?Kuna watu walikuwa wanapiga kelele humu kuwa demokrasia ya kenya imeiva ya kwetu ni mbichi na chachu! Wakasisitiza kuwa tume ya uchaguzi ya kenya iko huru sana!
Tumia Kichwa kufikiri sio matak*Muulize Mbowe utamu wa madaraka...maana uenyekiti tu wa chadema ni vita nna vifo hutokea (rejea Chacha Wangwe)
Umewaza kama nilivyowaza mimi.... Kwa kifupi ni ukweli usiopingika jamaa kweli ameuwawa ila maelezo ndio yanaleta utata. Kama hao 'mafia' walimuua hata huyo mwanamke ili kuficha siri, sasa ni nani alietoa hiyo taarifa ya kumshauri njia ya kupita? Kuna mengi na ya uhakika ambayo yanaweza kujulikana baada ya uchunguzi huru. Lakini kabla ya hapo kila mmoja atakuwa anajaribu kujenga hoja za kuangushia lawama upande wa pili (upande kinzani).Kwahiyo hizo taarifa umepataje ikiwa wote wawili wameuawa.?? Je nani alikuambia mwanamke ndio kamwambie wapitie huko ikiwa mwanamke mwenyewe ameuawa..??
Sent using Jamii Forums mobile app
Naskia Raila anataka proffesional IT atoke Uingereza kukaimu nafasi ya Msando....
Najiuliza hawa wazungu hatakuwa na interest zao wakamweka atakaye kuja kuangalia maslai yao?...