Exclusive: Haya Ndiyo Matukio Makubwa Yaliyopelekea Mauaji Ya Bosi Wa Iebc Musando Huko Kenya

Kitengo cha ICT ni kigumu sana katika tume ya uchaguzi. Leo tunawasema wakenya ila tunasahau kuwa Mkurugenzi wa ICT wa Tume ya uchaguzi ya Tanzania Dk. Sisti Cariah mwaka 2015 aliondolewa kwenye nafasi yake siku 25 kabla ya uchaguzi na hadi leo hakuna maelezo kwamba alipelekwa/alihamishiwa wapi na kwa sababu gani.
 
Jawani, jamani, ...majirani zetu wanahitaji kuombwewa maana wanakoelekea sasa ni mashaka matupu!
Haya hapa mengine...

View attachment 555255
Huyu baada ya ndugu zake kuanza kupiga kelele, leo kajitokeza na kudai yuko salama, alibanwa tu na kazi. Sasa sijui akibanwa na kazi ndio hata familia yake anasahau kuiarifu?
 
Mashaka yako yanaweza kuwa n'a mashiko lkn kwenye Upelelezi mtu akifa kitatanishi Polisi wanatafuta mtu wa mwisho aliekuwa na Marehemu Kwa maelezo ya mleta mada nikwamba Jamaa hata alipoomba Ulinzi wakulu hawakujali...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wake mwenda zake ndani ya city mortuary, inasemekana una majeraha mabaya mikononi na shingoni kuashiria aliteswa sana kabla hajauliwa.
 
Muulize Mbowe utamu wa madaraka...maana uenyekiti tu wa chadema ni vita nna vifo hutokea (rejea Chacha Wangwe)
 
Watu hawajui duniani twa pita tu na fahari zote za dunia tutaziacha......pumzika kwa amani Ndg....hakika kila mwana wa Adam ni lazima ayaonje mauti.
Angalia tu fahari ya uenyekiti wa chadema jinsi inavyopoteza watu
 

Kumbuka watu hawakuwa na imani na mfumo huo kwa kurejea historia ya uchaguzi uliopita ambapo mfumo uli feli na kusababishwa manual system kutumika. Hivyo kulikuwa na haja kubwa yeye kusema hivyo ili kuuaminisha umma kuwa safari hii mfumo uko vizuri, hakuwa na kosa lolote.
 

Uko sahihi 100% kuwa Marehemu Msando hiki ' Kifo ' amekitafuta mwenyewe kwani hakuna ' System ' yoyote ile duniani itakayokuacha salama kama ukifanya mambo aliyofanya Yeye. Na sijui alijiamini nini hadi akawa anajiaminisha vile alivyowaaminisha Wakenya. Katika nchi ambazo Mfanyakazi yoyote wa Tume ya Uchaguzi huwa ana 99% za ' Kuuwawa ' Kimafia kama akileta ' fyoko fyoko ' ni za Afrika ( japo sijui kama na Tanzania hapa Kwetu tabia hii ipo Wahenga mtanisaidia hapa )
 
Hii ni moja kati ya sababu za viongozi corrupt wa Africa kuipinga ICC.
1. Kubadili katiba ili wabakie madarakani
2. Kuwaweka vizuizini wapinzani
3. Mauaji ya watu wasiokubaliana na matakwa yao (assassination)
4. Kuminya uhuru wa habari
5. Kuhodhi mwenendo wa vyombo vya dola

Mwisho wa siku wanakaa kwenye vikao vyao na kusapotiana kujitoa ICC bila haya wakisema wazungu wanazingua.
 

Akhsante na tupo pamoja Mkuu na hii ndiyo Afrika.
 
Maelezo ya huyo mwanamke nani aliyatoa na kufanikisha kuandika? Kama Watu wamezuiliwa ni nani ameona kwamba kidole kimekatwa! Nani anajua kuwa huyo mwanamke alikuwa msiri wake??
nimesoma Leo dada yake marehemu huyo bint miaka 21 alisema caro alimuambia anatoka out ma msando kwenda kunywa na wanajua yeye na msando walikuwa mahawara ingia daily nation.Co.ke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…