Exclusive: Haya Ndiyo Matukio Makubwa Yaliyopelekea Mauaji Ya Bosi Wa Iebc Musando Huko Kenya


Una hoja nzuri lakini hebu tujiulize na tujifikirishe kidogo tu hivi kati ya Jubilee na NASA na akina nani wana 100% ya ' Kutekeleza ' mauaji yao kwa kuyaratibu vizuri kwa msaada wa State Security Organs za Kenya? Mkuu hivi kwa mazingira haya tu ya Kifo cha ghafla cha yule Waziri Major General Nkaissery ambaye nae alikuwa akiongoza idara ' Nyeti ' na huyu wa jana Msando na naambiwa kuwa hivi leo mchana tena Msemaji wa Jeshi la Kenya ametoweka hajulikani alipo mara baada tu ya Kukubali kuwa baadhi ya ' Nyaraka ' za Siri za Uibiwaji wa Kura zilikuwa zinaratibiwa moja kwa moja na Jeshi la Kenya ( KDF ).

Sasa kama Marehemu Msando ' kauliwa ' hadi kukatwa ' Kiganja ' chake nahisi huyu wanaweza wakamuua na wakakuta viungo vyake wamevitoa na kuvitandaza pembezoni mwa mwili wake. Nimetahadharisha na nazidi kutahadharisha kuwa kama ' Waangalizi ' wa uchaguzi huu wasipokuwa makini pamoja na nchi ' Washirika ' kukemea haya ' mauaji ' tutegemee Vita kubwa sana kuibuka nchini Kenya. Ukweli ni kwamba Kenyatta na Ruto hawatakiwi na Wakenya kwani wameharibu mno Uchumi wa Kenya lakini kama haitoshi wanasababisha ' mauaji ' yote haya ili kuwatisha Watu na hasa Watu wa Tume ( IECB ) ili waogope na kubwa zaidi hawataki akina Odinga na Musyoka wachukue nchi kwakuwa wanajua wakishinda tu ile Kesi ya akina Kenyatta na Ruto kule ICC the Hague itaibuliwa na hakuna ' ubishi ' wowote kwamba akina Kenyatta na Ruto walihusika kwa 100% na wanajulikana sana kwa ' Umafia '.
 
Tusisahau na kwetu Kibiti mkuu,..
Mauaji yemekua mengi kuliko Kenya.. So kama unazo nyepesi na Kibiti tungeanza na hizo kwanza....
 
Habari ya wauaji kukata kiganjia siyo kweli. Mwili umepatikana na mikono yote miwili ila inayo majeraha ya kisu.Picha Zipo mtandaoni ,kwa sababu za kimaadili siwezi kuzirusha hapa.

Sibishani na Wewe uliopo Tanzania bali nimepata hizo taarifa na Watu muhimu sana na ambao nawaamini na tunaaminiana kuwa moja ya ' Kiganja ' chake kimekatwa na kwamba hata hao waliokikata walitaka tu wakitumie katika kuwekea alama ya System zao za Mfumo wa ICT wa Tume ( IECB ) ili waweze ' Kudukua '. Na kwa taarifa yako tu ni kwamba ni Yeye mwenyewe ' Marehemu ' ndiyo alikuwa na direct access na IECB ' data system ' na ndiyo maana hata hao ' Wauwaji ' walitumia kila aina ya mbinu ili tu wamuue lakini wale sahani moja na hicho ' Kiganja ' chake. Na kuwepo sasa kwa ' Kganja ' chake sishangai kwani yawezekana baada ya kufanikiwa kufanya walichokifanya basi hao ' Wauwaji ' wakashirikiana na Madaktari ambao wengi wao huwa ni sehemu ya ' Umafia ' ili kukirudishia haraka hata kwa ' Kukishonea ' tu ili ' Kuwazuga ' Wananchi.

Jiulize tu swali kwamba hali ni shwari kwanini hadi sasa Police wamezuia ' Wanafamilia ' kwenda ' Mortuary ' kuungalia huo mwili? Na jiulize pia swali ni kwanini hadi sasa Police ya Kenya inakataa mwili wa Chris Msando kufanyiwa independent post-mortem? Yawezekana Wewe ukawa ni ' Mgeni ' wa masuala ya ' Kimafia ' ila nikusaidie tu hakuna Watu wenye mbinu za uhakika na zilizokwenda shule na ambazo pia ziko well coordinated kama ' Mafia '. Nimetumia hapa neno ' Mafia ' lakini in actual sense sijamaanisha ' Mafia ' unaowajua Wewe basi namaanisha ' Systems ' za ' Kiusalama ' za nchi husika.
 
Tunaweza tusiwe na uhakika lakini haina shaka kifo cha huyu bwana kilipangwa. Wakenya wakitafuta uongozi UTU huwaondoka kabisaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wakenya tu,... Humu ndani mwako yanayofanyika ni makubwa saaana.... Mambo yanafanywa kimya kimya na kawaida ya watanzania ni wasahaulifu saaana, sijui tuna tatizo gani!
Hata history ya nchi yetu hatuifahamu kama history ya nje!...
 
Kimsingi kutopewa Ulinzi haraka hakufanyi hitimisho kuwa Jubilee ndio wahausika maana wengine tunaweza kusema kuwa NASA wametumia huu mwanya kummaliza ili kuonesha na kuthibitisha kuna wizi wa kura....

Hili nalo ni neno ila kwa ' Scenario ' hii huwezi kuwatoa akina Kenyatta na Ruto katika hili na hasa ukiwa unajua vizuri historia za ' Kimafia ' za hawa ' Marafiki ' wanafiki wawili.
 

Uki judge kwa kutumia hizo sababu 7 ni moja tu unaweza kuihusisha na NASA pamoja na Jubilee ile ya kumumia mtu wa karibu. Nyingine zote zinapoint kwenye mamlaka zaidi.
 
Kumbe una akiliii zotee
 
Uhuru na Ruto wako tayari kuuwa ili wabaki ikulu

Na ndilo wanalolifanya sasa Mkuu. Na sababu Kuu hasa ya hawa kutekeleza ' Mauaji ' haya ya ' Kimafia ' ni hofu tu ya kwamba kama akina Odinga na Musyoka watachukua nchi ' watafufua ' ile Kesi yao ya Post Election Violence iliyopo ICC ' The Hague ' ambayo na yenyewe pia ilibidi wale ' Mashahidi ' wauliwe huku wengine wakihongwa Pesa ili ' kukwepesha ' ushahidi huku wengine wakimbia Kenya na kwenda ' Kujificha ' kwa hofu ya kutafutwa na ' Wauwaji ' wa Kenyatta na Ruto.
 


Hapo kwenye kukata kiganja haijathibitishwa ,halafu hivi finger print inaweza fanya kazi hata kama hakuna mzunguko wa damu? au alikatwa baada ya kuwaonesha kila jambo walilo hitaji? Lakini kulikuwa kuna ulazima gani kuutangazia Umma kuwa Msando ndiye mtu pekee anajua seva zilipo? Msando pia aliingiwa na siasa ndani yake kulikuwa hakuna sababu ya kuongea maneno yanayo onesha kuwa uchaguzi uliyopita ulidukuliwa wakati uwezi kuwapa Umma ushahidi na pia hakutakiwa kujitamba kiasi kile hadi kuwapa mbinu.
Mimi ninacho amini bado kuna utata mkubwa sana kwenye kifo cha huyo Msando ukiangalia kwa undani unaweza ukashindwa kuwakingia kifua wakina Raila...
Ukweli ni kwamba kama wakenye wasipo punguza mihemko ni wazi yatatokea machafuko...
Huyo msemaji wa polisi kasema yuko poa...
 

Hivi anayeondolewa na bado anapumua na tunakula nae ' bata ' Kitaa na Yule anayeondolewa kwa ' Kuuwawa ' na anaenda kula ' Bata ' Kaburini nani ana afadhali?
 
Naskia Raila anataka proffesional IT atoke Uingereza kukaimu nafasi ya Msando....

Najiuliza hawa wazungu hatakuwa na interest zao wakamweka atakaye kuja kuangalia maslai yao?...
 
Madaraka mabaya sana hasa kisiasa, mtu anaua mwenzie kisa uenyekiti wa chama sembuse urais?
 
Kwahiyo hizo taarifa umepataje ikiwa wote wawili wameuawa.?? Je nani alikuambia mwanamke ndio kamwambie wapitie huko ikiwa mwanamke mwenyewe ameuawa..??

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewaza kama nilivyowaza mimi.... Kwa kifupi ni ukweli usiopingika jamaa kweli ameuwawa ila maelezo ndio yanaleta utata. Kama hao 'mafia' walimuua hata huyo mwanamke ili kuficha siri, sasa ni nani alietoa hiyo taarifa ya kumshauri njia ya kupita? Kuna mengi na ya uhakika ambayo yanaweza kujulikana baada ya uchunguzi huru. Lakini kabla ya hapo kila mmoja atakuwa anajaribu kujenga hoja za kuangushia lawama upande wa pili (upande kinzani).
 
Naskia Raila anataka proffesional IT atoke Uingereza kukaimu nafasi ya Msando....

Najiuliza hawa wazungu hatakuwa na interest zao wakamweka atakaye kuja kuangalia maslai yao?...

Uko sahihi kwani ni kweli kwamba Marekani na Uingereza hawawapendi akina Kenyatta na Ruto na hata huko nyuma walijaribu sana kufanya ' mikakati ' yao ili Kenya isitawalike ila walinywea ' kiaina ' baada ya kuona Kenya imeimarisha mno ' uhusiano ' wake na China na ule umoja wa BRICS ' nations ' hali ambayo isingepelekea Kenya kuingia katika matatizo makubwa ya ' Kiuchumi '.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…