Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi in kidole au kiganja?Maelezo ya huyo mwanamke nani aliyatoa na kufanikisha kuandika? Kama Watu wamezuiliwa ni nani ameona kwamba kidole kimekatwa! Nani anajua kuwa huyo mwanamke alikuwa msiri wake??
Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IECB Bwana Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ' Kitaarifa ' zaidi kutoka kwa ' Wadau ' mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ' Wabobezi ' wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea Kifo hiko cha ' Kikatili ' kabisa.
Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu zilizopita kabla ya hayo ' Mauaji ' yake ya ' Kikatili ' kutokea hivyo nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ' tathmini ' mwenyewe ' Kimoyomoyo ' kisha mwishoni wote tutajua ni nani ' Kamuua ' Marehemu Chris Msando.
Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa ' Oparesheni ' za IECB alijibiwa na kupewa ' Ushirikiano haraka sana.
Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa za Yeye ' Kutishiwa ' maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ' Ulinzi ' aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.
Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ' Onyo ' kali la kutozungumza na Chombo chochote cha Habari nchini Kenya na ' Mamlaka ' na kuambiwa kwamba Mtu pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa Habari na Mawasiliano.
Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ' alikaidi ' hiyo amri kutoka katika ' Mamlaka ' ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ' mauaji ' yake.
Tukio #5.
Wakati akiwa ' mubashara ' kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha Habari Marehemu alisikika ' akiwahakikishia ' Wakenya wote kuwa kwa jinsi alivyotengeneza ' Mfumo ' wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ' Kuudukua ' hata iweje na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ' hack ' taarifa zozote za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ' Kiganja ' chake kwani ili upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ' Kiganja ' chake cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.
Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ' Kimafia ' na labda pengine alijisahau kuwa siku zote ukitaka tu ' Kuuawa ' Kimafia basi Mtu wako wa Karibu sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ' Mwanamke ' ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ' Mwanamke ' kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ' Kimafia ' ndipo akamtega Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ' Wauaji ' wake wale ' Mafia ' walikuwepo.
Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ' Wauaji ' wake wa ' Kimafia ' walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ' Udukuzi 'wowote utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ' chake ndipo hata katika ' mauaji ' yake ya juzi ' Kiganja ' chake cha Mkono ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ' Wauaji ' na kuuacha mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.
Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule ambaye atakuwa kafanikisha ' mauaji ' ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi wote kitu ambacho ' Wauaji ' hawa walikifanya kwa ' Kumuua ' na Yule Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ' Mission Accomplished '.
Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ' Muuaji ' Mkuu wa Marehemu Chris Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ' Ushirikiano ' mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ' wamechoka ' na haya mauaji ya ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti.
Nawasilisha.
Hii ni taaluma, na mlet mada kaongea kitaalamu, sasa kama kuna kilichokukwaza hiyo haimuhusu maana maswali yako ya kishabiki hata wewe unaweza kuyajibu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee; umeitendea haki makala yako.Angalia usihusishwe kwenye huo msafara.
Sent using Jamii Forums mobile app
We can't say for certain the Government is involved or not. Anybody could have planned this incidents.The question is why and who is to benefit?
Du sijui na sisi 2020 itakuwa hivi
Acha ulongo wako! Nani kasimlia kuwa mwanamke alimwambia kuwa wapite barabara fulani! Wakati waliokuwa wawili na wote wamekufa! Ukamatwe kusaidia polisi!
Don't lie! Who said the women had convinced Chris to use the gang's dedicated road while all of them died in a tragedy! Let you be apprehended to help police investigation!
If you know your enemy than yourself you shall never suffer a defeat
Ogopa sana wanawake, kuwa makini nao, ni mama zetu Ila uhalibifu duniani umetokana nao, nafasi kama hizi zinahitaji watu waliopitia jeshini, huko kuna NIDHAMU kuuWakiniweza wakafukue ' Kaburi ' la aliyenipika. Ukishazijua njia zao na Wewe unacheza nazo hizo hizo hadi mwishowe wanaomba ' Urafiki ' na Wewe na hata ' Kukuogopa ' pia. Huyo ' Marehemu ' Msando nimemlaumu kitu kimoja tu na nimeshangaa sana kama kweli alipita humo ' Vyuoni ' na kujifunza mambo ya ' Kimafia '. Hivi Wewe unajua fika kuwa ' unawindwa ' na pia unajulikana fika kuwa ni Mpenda ' Mbunye ' halafu ' Mafia ' wanakutegea ' Mbunye ' na Wewe bila ' Kushtuka ' unaivagaa tu kwanini usife na wakafanikisha lao?
Vifo vingi sana / mauaji mengi mno ya ' Kimafia ' wanawake huhusishwa 100% na ndiyo maana Mimi hadi ' Kufa ' Kwangu sitokuja kumuamini ' Kiumbe ' aitwae Mwanamke.
Finger print haina uhusiano na mzunguko wa damu.Ndio maana nasema hivi kwenye mauaji yake kuna maswali wengi.... Halafu hivi kama kiganja kikikatwa finger print itafanya kazi? Hivi finger print haitegemei mzunguzo wa damu?
Nimeamini mapenzi ni upofu,jamani kumbe alikuwa na kabinti kwa 21 yrs old.Cha kusikitisha yule binti ni mkikuyu na wana almost months since wameanza kudate.Naona alikuwa player sana ndo maana kategeka kirahisi mno.Jamani na akili zote za kuwa IT engneer ila hakuweza kabisa kujikinga na penzi la mkikuyu Carol shafir Ngumbu.Jamani Wanaume nanyi mjifunze,michepuko ni kutafuta kifo tu.Angetulia na mkewe haya yasingemkuta.
acha uwongo wewe lini msemaji wa kdf alsema wanaratibu wizi wa kura?
anyway endelea kupotosha wajinga wasofatilia siasa za Kenya
by the way wa tz hawata piga kura kenya
keep it .........'your propaganda won't work out
Mwangosiiiii,Mawazoooo,Ben Saananeeee!!!Tunaweza tusiwe na uhakika lakini haina shaka kifo cha huyu bwana kilipangwa. Wakenya wakitafuta uongozi UTU huwaondoka kabisaaa.
Sent using Jamii Forums mobile app