Mh Lissu, hongera na pole kwa maswahibu uliyopitia na mikiki ya kampeni!
Maswali yangu:
1. Hivi sasa kuna miradi mikubwa ambayo serikali ya JPM imeianzisha na inaendelea kuijenga ikiwemo mradi wa SGR na ule wa bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo eneo la Stiegler's Gorge, Morogoro pamoja na ufufuaji wa ATCL!
Je, miradi hii ambayo tayari serikali imeshawekeza fedha nyingi utaiendeleza ama utachukua hatua gani endapo itabainika ina ufisadi ndani yake?
2. Mheshimiwa aliyeko madarakani kwa sasa, Rais Magufuli amekua akisikika mara kwa mara kuwa anataka mwaka huu uwe fundisho kwa wapinga maendeleo, akidai kuwa wanaompinga siyo wapenda maendeleo na atawafunza! Wewe umekuwa ukimpinga hadharani bila kuogopa, je unadhani pengine kauli hizo zinakuhusu wewe!? Na kama ndivyo majibu yako ni yapi kwenye hizo kauli..!?
3. Mh. Kwenye sekta ya madini ambayo imeonekana ukiipigia sana kelele hasa kwenye suala la makinikia, je utakapoingia madarakani utaendelea kuruhusu makinikia kusafirishwa kama ilivyokuwa awali ama utatumia mbinu gani kuhakikisha kuna usawa katika sekta hii! Je utakuwa tayari pengine kuweka mikataba yote hadharani kama bunge lilivyokuwa linadai!?
4. Waliovunjiwa nyumba zao Kimara, je utakuwa tayari kuwalipa? Na utawachukulia hatua gani wale wote waliohusika kuwavunjia wale wananchi nyumba zao?
5. Dar esa salaam, imekuwa na miundombinu mibovu sana, hasa kwenye suala la kuthibiti mafuriko!
Je ni hatua zipi utakazochukua angalau ziwe za muda mfupi na mrefu ili kuthibiti mafuriko ambayo yamekuwa yakilikumba hili jiji kws muda mrefu!?
Nashukuru, mheshimiwa kwa kujitokeza kujibu maswali yetu humu, nakutakia kila la kheri, tarehe 28/10/2020 Watz tumeamua tuna jambo letu!