Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
1. Ni kwa nini unaomba kuiongoza nchi ambayo ulizunguka Mataifa mbalimbali ya mabeberu kuichafua

2. Ulisema Raisikuzuia makinikia bandarini nchi yetu itashitakiwa na kufilisiwa. Je, wewe ukiwa Rais utawaruhusu mabeberu kufanya lolote walitakalo katika nchi yetu?

3. Sera zako siku zote ni kusema ubaya ya JPM na uhuru wa vyombo vya habari na haki. Je, kwa kipindi chako chote cha miaka 5 utashughulika na JPM na uhuru wa vyombo vya habari pekee?

5. Unasaga sana maendelea ya vitu. Imekuaje leo unawaahidi watu wa ukerewe kuwajengea daraja la kuwaunganisha na Bunda?
 
Mh. Tundu Lissu, naomba majibu juu ya hii kero yangu ya kibiashara kati ya Tanzania bara na visiwa vya Zanzibar.

Utadhibiti vipi hizi Kodi zinazotozwa Mara mbili mbili unapoagiza mzigo kutoka Zanzibar unalipia ZRB, TRA na ukifika Tz bara unalipia Tena TRA?

AHSANTE
 
Swali;
1.Bwana Tundu Lissu umesema ukiwa Rais utawapeleka watu wengi kwenye Mahakama ya wazungu "The Hague" Je wewe utakuwa Rais wa Watanzania au Rais wa Wazungu!?

Jibu swali Bwana Tundu Lissu.
 
swali: swala la ajira limekuwa tishio hasa kwa vijana na kufanya elimu kuonekana haina thamani, Je serikali yako ipo tayari kuhakikisha suala la ajira ni jukumu la serikali na kuweka fao la kutafuta ajira kwa angalau miaka mitatu baada ya mtu kuitimu?
 
Tundu Lisu watanzania wameshakuelewa na wameshakukubali. Utashinda uchaguzi ila hautatangazwa.

Shida ni ubovu wa Katiba yetu.

Hongera sana kwa kuamsha watanzania kutoka usingizini. Wengi ni wajinga na hata haki zao za msingi hawazielewi. CCM waliwekeza kwenye ujinga ili waweze kutawala milele.
 
Kwako Lisu wewe ni mgombea uraisi na hujawa raisi hadi ikitokea ukapochaguliwa.

Baadhi ya watanzania nikiwemo Mimi sikuamini kama kweli Una Nia njema na nchi hii, ulikwenda kuonana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania sihitaji kujua uliongea nini swali ni Kwanini Balozi ajitetea kwamba mazungumzo yenu hayakuhusu uchaguzi wakati hakuna aliyemuuliza huoni hadi hapo tayari katupa mwanga ya nini mlichoongea?
 
Mhe. Utakua Tayari kuleta katiba mpya ndani ya miaka mitatu ya mwanzo?
 
Mheshimiwa Lissu, kwa namna hali ya kampeni zilivyo, unaonyesha kabisa umeshinda!

Swali, Je ni kwa namna gani umejipanga kuhakikisha tunakabidhiwa dola ili hali inajulikana CCM hawako tayari kukabidhi kwa njia yoyote ile?!
 
Maswali:

1. Mheshimiwa utasaidiaje kupunguzwa kwa mzigo wa ulejeshwaji wa mkopo wa HESLB kutoka asilimia 15% ambayo ni kubwa sana pia ongezeko la deni la 6% linalodaiwa kuwa value retention fee VRF na inapunguza uwezo wa wengi wetu kukabili mahitaji ya wategemezi wetu ambao walisubiri sana kwa hamu tumalize masomo tukawakomboe.

2. Utawezaje kurudisha madaraka kwa wananchi ili na wewe ukiwa katika nafasi ile usiwe mtu wa kutamka tena kwa kudhalilisha watu unapowatoa madarakani kwa sababu ya makosa mbalimbali iwe ya kweli au si ya kweli.

3. Taifa letu tunategemea sana kilimo lakini ni aibu sana shule zilizokua zinafundisha somo la kilimo kwa sasa si jambo linalotiliwa mkazo kabisa ...utasaidiaje kuhuisha somo la kilimo kwa theory na practical?
 
Mheshimiwa Tundu Lissu,Pole na mchakamchaka wa kampeni.

Naomba nikuulize swali moja:

Mara kadhaa nimekusikia ukiongelea watakaoshiriki wizi wa kura kuwapeleka ICC, unadhani hiyo ICC watalishughulikia inavotaka? Wagombea waliotangulia hawajawahi kufanya hivyo?.
 
1. Chama cha CHADEMA, ambacho wewe ni mgombea wake mlikuwa mnajinasibu kwa kupinga Rushwa na ufisadi. Mbona Sera hiyo chama chako imeiacha, je ni ufisadi na Rushwa zimekwisha, hasa kwenye chama chako kwenye ruzuku, michango ya wabunge pamoja na fedha za mifuko ya majimbo?.

2. Wewe ni Mzalendo?. Mbona Sera zako nyingi ndani yake kuna chuki, kutojali, dharau kwa watanzania kwa kuwachonganisha na serikali yao ili kuvuruga amani na utulivu uliopo?. Huu uongozi unaoutaka utakufaidia nini, kama hakutakuwa na amani?

Maana the way you behave, ni kama kuna watu wamekutuma uchafue kisima cha amani ambacho watanzania wote twategemea maji yake?

3. Wabunge ni wawakilishi wa wananchi. Mbona wabunge wengi wa chama cha Mbowe, huwa hawaungi mkono Bajeti, hutoka nje mara kwa mara sasa mule huwa mnawakilisha CHADEMA au watanzania waliowachagua?.

4. Je, una mpango wa kuanzisha chama chako cha siasa baada ya kushindwa p Oct 28?.

Kila la kheri.
 
Mgombea Tundu Lissu

Naomba utufafanulie kuwa ulikana urai wa Tanzania na kupata passport ya nchi nyingine.

Maswali mengine yatafuata baada ya kupata jibu.
 
Mgombea Tundu Lissu,

pole kwa kupigwa risasi na tunamshukuru mwenyezi mungu kukuponya. Swali, ilikuwaje ukaumia upande wa kulia baadala ya kushoto?
 
MHE, TUNDU LISU MGOMBEA URAIS WA JMT KUPITIA CHADEMA. MIE NAULIZA JE,IKITOKEA UKAWA RAIS WA TANZANIA UNADHANI NI YAPI UTAKAYOYAENDEZA YALIYOANZISHA NA CCM KIMAENDELEO NA YAPI UTAYAACHA NA KUYASITISHA?

PILI, JE UNAKUMBUKA NI YAPI YALIYOMEGWA NA SERIKALI YA CCM KUTOKA KWA SERA ZA CHADEMA NA UPINZANI KWA UJUMLA, AMBAYO MWANZONI WALIYAPINGA? NA KISHA SERIKALI YA CCM KUYAWEKA KTK SERA YAKE NA KUYAFANYIA KAZI? TOA MFANO WA SERA HIZO.
 
Mheshimiwa pole na kampeni na hongera pia ,na maswali kadhaa kwako

1. Upi msimamo wako juu ya wawekezaji wa Shantamine wa sambaru ikungi?

2. Una mpango gani wa kuhusu mikoa isiyo na vyuo vikuu?

3. Ukiingia madarakani utachagua mrengo upi wa kushirikiana nao kati ya Magharibu (UsA,UK na France) au ule wa mashariki (rusia ,China na North Korea)
 
Mgombea Tundu Lissu,

Je, huoni ni wakati muafaka kuelezea itikadi ya chama chako na ilani yenu badala ya kumpigia kampeni Dr Magufuli kwa kila baada ya sentensi moja kumtaja?
 
Mh Lissu, hongera na pole kwa maswahibu uliyopitia na mikiki ya kampeni!

Maswali yangu:

1. Hivi sasa kuna miradi mikubwa ambayo serikali ya JPM imeianzisha na inaendelea kuijenga ikiwemo mradi wa SGR na ule wa bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo eneo la Stiegler's Gorge, Morogoro pamoja na ufufuaji wa ATCL!

Je, miradi hii ambayo tayari serikali imeshawekeza fedha nyingi utaiendeleza ama utachukua hatua gani endapo itabainika ina ufisadi ndani yake?

2. Mheshimiwa aliyeko madarakani kwa sasa, Rais Magufuli amekua akisikika mara kwa mara kuwa anataka mwaka huu uwe fundisho kwa wapinga maendeleo, akidai kuwa wanaompinga siyo wapenda maendeleo na atawafunza! Wewe umekuwa ukimpinga hadharani bila kuogopa, je unadhani pengine kauli hizo zinakuhusu wewe!? Na kama ndivyo majibu yako ni yapi kwenye hizo kauli..!?

3. Mh. Kwenye sekta ya madini ambayo imeonekana ukiipigia sana kelele hasa kwenye suala la makinikia, je utakapoingia madarakani utaendelea kuruhusu makinikia kusafirishwa kama ilivyokuwa awali ama utatumia mbinu gani kuhakikisha kuna usawa katika sekta hii! Je utakuwa tayari pengine kuweka mikataba yote hadharani kama bunge lilivyokuwa linadai!?

4. Waliovunjiwa nyumba zao Kimara, je utakuwa tayari kuwalipa? Na utawachukulia hatua gani wale wote waliohusika kuwavunjia wale wananchi nyumba zao?

5. Dar esa salaam, imekuwa na miundombinu mibovu sana, hasa kwenye suala la kuthibiti mafuriko!

Je ni hatua zipi utakazochukua angalau ziwe za muda mfupi na mrefu ili kuthibiti mafuriko ambayo yamekuwa yakilikumba hili jiji kws muda mrefu!?

Nashukuru, mheshimiwa kwa kujitokeza kujibu maswali yetu humu, nakutakia kila la kheri, tarehe 28/10/2020 Watz tumeamua tuna jambo letu!
 
1. Kuna ufa mkubwa unaoonekana kwa sasa katika nchi yetu. Ufa huu mkubwa unatokana na siasa. Tofauti za kiitikadi zimepunguza mapenzi baina ya wananchi.

Je, Serikali yako itachukua hatua zipi katika kuuziba ufa huo?

2. Katika kipindi cha awamu hii ya tano (2015-2020) tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa kisiasa, wakihama vyama vyao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi kwa kile kinachoitwa "kuunga juhudi mkono." Wapo wanaohusisha uungaji huo mkono na rushwa (kuwa viongozi hao wamenunuliwa kwa pesa au ahadi za vyeo). Swali, je Serikali ya Chadema itaitaka TAKUKURU kufanya uchunguzi huru kuweza kubaini iwapo rushwa ilitumika kama ushawishi kwa viongozi hao au waliunga juhudi kwa mapenzi yao?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom