EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

Mimi nataka Sonko ashinde tu, basi.

Hao wengine wala sijali.
 
OFFICIAL PRESIDENTIAL RESULTS:

01:20am August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) Imetangaza matokeo ya vituo 29,209 Uhuru Kenyatta kura 6,044,745 (55.27%) na Raila Odinga kura 4,805,159 (43.93%).


LIVE VIDEO FEED:



fe7a316c97d3b4563a4c2cbca91a7a97.jpg


c6e580981b0395e5277b6f9e203969ff.jpg


FACT 1: Kenya spent 49.9billion Kshs to organize this election and it's the most expensive since country's independence

KENYA: Uchaguzi Mkuu unafanyika leo, Wapiga kura milioni 19 watachagua Rais, Wabunge, Maseneta, Magavana, Madiwani na Wawakilishi wa Wanawake.

Raia wa Kenya wataamua nani atakuwa Rais wao na Makamu wa Rais kwa miaka 5 ijayo.

Ushindani mkubwa sana uko kati ya vyama vya Jubilee na NASA na wagombea wake wa Urais, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Pamoja na kura ya urais pia watapiga kura ya kuchagua magavana wa Kaunti, wawakilishi wa kata(madiwani) na wawakilishi wa Seneti na Bunge.

Fuatilia hapa kupata updates za uchaguzi huu unaohusisha takribani wapiga kura milioni 20 waliojiandikisha.

Waliojiandikisha: Milioni 19
Vituo vya kupigia kura: 40,000
Idadi ya Wakenya: Milioni 48

WASIFU WA WAGOMBEA KWA UFUPI

Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) iliwaidhinisha wanasiasa wanane ambao watawania urais katika uchaguzi mkuu huu wa Agosti mwaka huu.
Walioidhinishwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee ambaye atakuwa anawania kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Bw Raila Odinga ambaye anawania urais kwa mara ya nne.

Bw Odinga, aliyehudumu kama waziri mkuu katika serikali ya muungano ya Rais Mwai Kibaki kati ya 2008 na 2013, anawania urais chini ya umoja wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA).

Katika uchaguzi huu wa tarehe 8 Agosti, kutakuwa na wagombea wanne pia ambao ni wagombea huru (hawana vyama).

Abduba Dida

Anawania urais kupitia chama cha Alliance for Real Change (ARK) na muungano wa Tunza Coalition.
Alikuwa mwalimu wa shule ya upili ya Lenana jijini Nairobi.
Hii ni mara yake ya pili kuwania urais baada ya mwaka 2013 ambapo alipata kura 52,848 na kumaliza wa tano.

Cyrus Jirongo

Ni mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Anawania kupitia chama cha United Democratic Party (UDP).

Alipata umaarufu kisiasa mwaka 1992 alipokuwa katika kundi la vijana wa chama cha KANU, Youth for KANU 1992 waliokuwa wakimfanyia kampeni Rais Daniel arap Moi wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka huo.

Ekuru Aukot

Anawania urais kupitia chama cha Thirdway Alliance Kenya (TAK), na ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Alihudumu kama katibu katika Kamati ya Wataalamu waliosaidia kutunga Katiba Mpya ya Kenya ambayo iliidhinishwa na kuanza kutekelezwa mwaka 2010. Asili yake ni Kapedo, Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya na amejitangaza kama mtu anayeleta mwamko mpya katika uongozi nchini Kenya. Amekuwa pia akitetea makabila madogo.

Japhet Kaluyu

Ni mgombea huru ambaye amerejea nchini Kenya hivi majuzi kutoka Marekani. Amejieleza kama mwalimu, mshauri na mwandishi ambaye ana uzoefu wa kufanya kazi Wall Street. Anasema amebobea katika utafiti katika sekta ya afya na msomi. Ni mara yake ya kwanza kuwania urais.

Joseph Nyagah

Ni mwanasiasa wa muda mrefu nchini Kenya ambaye alihudumu kama waziri wa vyama vya ushirika chini ya Rais Mwai Kibaki, na baadaye akawa mshauri wa Rais Kenyatta. Babake, Jeremiah Nyagah, alikuwa waziri wakati wa utawala wa mwanzilishi wa taifa la Kenya Jomo Kenyatta.

Bw Nyagah, ambaye alikuwahi kuwakilisha Kenya katika Umoja wa Ulaya, alihudumu kama mbunge wa eneo la Gachoka, Kaunti ya Embu mashariki mwa Kenya kabla ya kuteuliwa waziri. Anasema ndiye pekee anayeweza kutatua matatizo yanayoikumba Kenya, kutokana na uzoefu wake katika uongozi.

Akihojiwa na runinga ya NTV baada ya kuidhinishwa, alidokeza kwamba aliacha kazi yake ya kuwa mshauri wa rais baada ya kugundua kwamba ushauri aliokuwa anaoutoa haukuwa unafuatwa.

Prof Michael Wainaina

Yeye ni mgombea huru ambaye amekuwa mhadhiri wa fasihi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Amekuwa mkosoaji mkuu wa mfumo wa sasa wa kisiasa Kenya na pia mchanganuzi wa siasa. Anasema aliamua kuwa mgombea huru kwa sababu vyama haviwapi nafasi vijana na wanawake.

Raila Odinga

Ni kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ambaye anawania chini ya muungano wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA). Aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa kwanza wa Kenya, wadhifa ulioundwa kufuatia Mkataba wa Kitaifa ulioafikiwa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, ambapo aligawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki.

Ni mara yake ya nne kuwania urais Kenya. Mwaka 2013, akiwa bado na mgombea wake wa sasa Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka, alishindwa na Rais Uhuru Kenyatta. Alipinga matokeo hayo mahakamani lakini mahakama ikatupilia mbali kesi hiyo.

Uhuru Kenyatta

Anawania kwa muhula wa pili kupitia chama cha Jubilee Party ambacho asili yake ni muungano wa Jubilee wa vyama vya TNA na URP alioutumia kushinda urais mwaka 2013. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ni mwanawe mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta. Mgombea wake mwenza ni Bw William Ruto kutoka eneo la Bonde la Ufa la Kenya. Wawili hao wanawaomba wapiga kura kuwachagua tena kuendeleza maendeleo ambayo wanaamini serikali yao imetekeleza katika kipindi cha miaka minne ambayo wamekuwa madarakani.

Bw Kenyatta aliwania urais mara ya kwanza 2002 dhidi ya Mwai Kibaki kupitia chama kilichokuwa kinatawala wakati huo, chama cha KANU cha Rais Moi aliyekuwa anaondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 24. Alishindwa na akawa kiongozi wa upinzani na kwa pamoja na Bw Odinga wakafaulu kupinga Katiba Mpya iliyopendekezwa mwaka 2005. Mwaka 2007, alimuunga mkono Rais Kibaki uchaguzini.

========

UPDATES:

View attachment 560756
Vijana wa Kaunti ya Kisumu wakiwa kwenye mstari wakisubiri kupiga kura.

View attachment 560757
Kaunti ya Siaya nao hawajataka kuwa nyuma.

d8a791dd363227292d5e7e5d0038f123.jpg

Man on a life support machine casts his vote at Dandora Primary School

48cb4990f0198f08c84aeb19959f6d49.jpg

Voters patiently waiting to cast their votes at Moi Avenue primary, Starehe constituency in Nairobi

LIVE TEXT FEED:

08:50am updates

> Rais Uhuru Kenyatta amewataka wakenya wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wanaowapenda

> NASA wameamua kufuta kauli yao dhidi ya KDF baada ya kuhakikishiwa kuwa kila kitu kitaenda kwa mujibu wa taratibu na sheria

> Waangalizi wa EU wameridhika na mwenendo unaoonekana hadi sasa

> Wakenya wengi wamekiri kuwepo kwa propaganda kwa njia ya mitandao ya kijamii na hivyo kuwachanganya wengi

09:50am updates

df39ac57afe4eb0c080a6da1047863ce.jpg

> Takribani Wafungwa 167 wameruhusiwa kupiga kura na hata wanahabari wameruhusiwa kuhojiana nao kupata maoni yao juu ya uchaguzi huu (picha inajieleza)

> Tume ya Uchaguzi(IEBC) imekanusha kukwama kwa zoezi la Uchaguzi huko Kisumu. Wamesema kila kituo kuna vifaa vya akiba

> Gavana Wycliffe Oparanya amepiga kura katika Shule ya Msingi ya Mabole, Butere. Amewataka Wakenya kufanya uamuzi wa busara

11:30am updates:

> Waziri wa Kilimo katika Kaunti ya Meru, Genaro Gatangugi na Mbae Kiugo wameshambuliwa na wananchi baada ya kufumaniwa wakinunua vitambulisho eneo la Imenti Kusini

12:00pm updates:

> Mgombea Urais, Raila Odinga(NASA) anaelekea kupiga Kura katika kituo cha shule ya msingi Kibera

> Mgombea Urais kwa tiketi ya Jubilee, Uhuru Kenyatta amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Mutomo, Gatundu Kusini

> Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 64, Patrick Wame amezirai na kufariki dunia baada ya kupiga kura ktk kituo cha Lela, Nyando.

> Maafisa wawili wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujaribu kubadili majina ya makarani wa vituo. Maafisa hao walitaka kuwaweka Makarani wanaowataka wao kinyume na utaratibu. Tukio limetokea Kandara, Murang'a.

> Watu 24 wamejeruhiwa katika kituo cha Shule ya Msingi Moi Avenue baada ya kukanyagana wakati wakisubiri kupiga kura.

======
3: 00 PM UPDATES


> Mwanamke mmoja amejifungua Mtoto wa Kike katika kituo cha kupigia kura kilichopo Pokot Kaskazini. Mtoto huyo amepewa jina la Chepkura kwasababu amezaliwa siku ya uchaguzi.

> Mawakala watatu wa Jubilee wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuendesha zoezi la kuhesabu kura ktk Kituo cha Heshima Shule ya Msingi.

> Gari moja lenye namba za usajiri bandia za KBY 840C likiwa katika msafara unaolindwa limekamatwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi na kukutwa na karatasi za kura ziliwe zimewekewa alama kwa Wagombea wa Jubilee. Limekamatwa huko traveling under escort found carrying (KIEMS) Mandera, Banissa.

>
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chebukati atoa taarifa fupi ya namna Uchaguzi unavyoendelea nchini humo.
  • Wafula Chebukati akiongea na Waandishi wa habari asema zoezi la Uchaguzi linaendelea vyema kwa maeneo mengi nchini humo.
  • Zoezi la kupiga kura linaendelea vyema Magerezani, kwa yale maeneo yaliyochelewa kuanza kupiga kura wataongezewa muda.
  • Chebukati: Vituo vitatu vilivyopo Laikipia vilipata changamoto za kiusalama lakini changamoto hizo zimetatuliwa na zoezi la kupiga kura linaendelea.

=====

4: 00 PM UPDATES

> Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, amekwama kupiga kura baada ya kukosa jina lake kwenye orodha ya majina ya wapiga kura iliyotolewa na Tume

> Katika vituo vipatavyo 40,883 vya kupigia kura, vituo sita vilikuwa na mpiga kura mmoja aliyeandikishwa.

> Raia wa kenya 4,300 walijiandikisha katika nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Afrka Kusini. Wamepiga kura katika nchi hizo.


5:34 PM
> Hatimaye Rais Mstaafu, Mwai Kibaki afanikiwa kupiga kura ikiwa ni dakika 34 baada ya muda wa kupiga kura kuisha.

> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chekibukati amesema vituo 300 vimeongezewa muda wa kupiga kura kutokana na changamoto mbalimbali.

Ametoa mfano wa baadhi ya vituo hivyo na changamoto zilizojitokeza;
  • Huko katika Kaunti ya Turkana vituo 18 havikufunguliwa kwa wakati kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia usiku wa kuamkia leo.
  • Jimbo la Ndia ambalo linavituo vya kupigia kura vipatavyo 70 ambavyo vilikumbwa na changamoto ya kuishiwa na karatasi za kupigia kura. Pia Vituo vya Nakuru Mashariki(Eneo lenye vituo 185) vilikumbwa na changamoto hiyo.
=======

FUATILIA HAPA MATOKEO YA UCHAGUZI

RESULTS

Odinga chaliiiiiiiiii pwaaaaaa
 
73% reporting
Uhuru 6.1 million votes
Raila 4.9 million votes

Kuna tetesi kwamba Raila hayatambui matokeo, kama hili ni kweli basi nahofia uvunjifu wa amani Kenya.
 
73% reporting
Uhuru 6.1 million votes
Raila 4.9 million votes

Kuna tetesi kwamba Raila hayatambui matokeo, kama hili ni kweli basi nahofia uvunjifu wa amani Kenya.

Chapa viboko tu hao
 
Mh! Panga zinaanza kucharangwa usiku huu wakati yeye atakimbilia Tanzania akahifadhiwe na nanihii.

Kumekucha....[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
b498f8838f8dd917c91e71d354e46179.jpg
 
Waafrika ndivyo tulivyo.
Yaani tupo radhi wafe mradi tupate madaraka.

Tumelaaniwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa sijui Kibaki alinufaika na nini tu!!

Halafu ule ulikuwa ni wizi dhahiri kabisa yaani.

Kwa hiyo Raila kuwa na wasiwasi juu figisu ana sababu inayoeleweka.

Ni rahisi kumwambia yeye akubali matokeo lakini si rahisi kuwaambia wezi walio na madaraka kuacha wizi wao.
 
Screenshot_20170809-040848.png
Screenshot_20170809-040356.png
DGv3yzEXoAAioSs.jpg
DGv3xoUXgAAJSS-.jpg


Mpaka sasa kimeshanuka huko. Raila hatambui matokeo yoyote mpaka sasa kwani matokeo yanayotambulika kisheria ni kutoka FORM 34a ambayo tume ya uchaguzi ilitakiwa iwe imeupload kwenye system. Ukienda Twitter utaona hadi odinga ameshatoa tamko. Wakenya wengi wanatweet tume iache Uzembe huo kwani they have jobs to go and schools to attend.
 
Sasa sijui Kibaki alinufaika na nini tu!!

Halafu ule ulikuwa ni wizi dhahiri kabisa yaani.

Kwa hiyo Raila kuwa na wasiwasi juu figisu ana sababu inayoeleweka.

Ni rahisi kumwambia yeye akubali matokeo lakini si rahisi kuwaambia wezi walio na madaraka kuacha wizi wao.
Nakuelewa vizuri NN

Ila kwa uchaguzi huu nionavyo mimi Odinga hakuwa wakushinda. Or hajashinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom