Experience yangu ya matumizi ya tiGO fiber

Experience yangu ya matumizi ya tiGO fiber

leoleo-tu

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Posts
2,224
Reaction score
6,784
Nimekuwa nikitumia superkasi kwa muda na nilijaribu ile ya airtel japo performance zilikuwa poa ila nilikuwa nikipata shida ya latency kuwa kubwa maana mainly shughuli zangu zina involve calls za zoom and google meet.

so recently tigo wamesambaza fiber yao mpaka huku bunju nikaamua na mimi nijaribu.

Nikalipia kifurushi cha 70,000 amapo wanakuletea rooter ambayo ina ethernet ports 5 na inatoa wi-fi. Hiki kifurushi cha 70,000 ni cha 10mbs.

Kwa sasa huduma yao iko faster nilipolipa kusurvey hadi kufunga ni ndani ya siku tano.

kwa sasa naweza kusema naona value for money maana mimi speed ya mb 10 inanitosha kwa streaming downloading na kusurf kwa computer 2 na simu nyumbani. Ping yao kwa sababu ni fiber ni ya chini sana na speed kwa kiasi kikubwa ni stable.

Hadi sasa siku ya 3 sijapata changamoto yoyote na ni beyond my expectation.

1723608013903.png
 
Mkuu habari. Kwa mfano nikaamua kuiweka huduma hii kwenye eneo langu la biashara ili kuvutia wateja wapate free wi-Fi wanapokuja kupata huduma inaweza kunipatia faida?
Swali gumu sana, inaweza na isiweze depending na biashara mfano:
Unamiliki Bar mtu anakuja kwa ajili ya Wifi tu anakunywa soda moja anakaa masaa 3.
Kwa Barbershop iko poa sana, nimewai ona inavuta sana wateja.
 
Mkuu habari. Kwa mfano nikaamua kuiweka huduma hii kwenye eneo langu la biashara ili kuvutia wateja wapate free wi-Fi wanapokuja kufanya manunuzi ya bidhaa, je inaweza kunipatia faida?
Utapata faida kubwa sana mkuu.
Mteja akija lazima anunue kitu ili apate WiFi.

Sometimes tunakaaga kwenye restaurant kufanya kazi,

Najua mwigulu anaichungulia hii fursa jinsi yakuweka aweze kutupiga na huku.
 
Ni innovation nzuri
ndio mkuu, ninachohofia ni kama mteja anaweza kufanya matumizi makubwa ya data alafu kifurushi kikaniishia kabla ya mwezi, nafikiri hii huduma inaweza kuniongezea trafficking kwenye biashara hasa wanafunzi wakiwa ndio walengwa wakubwa
 
Usije chinganya na limited bando utakufa kwa pressure tafuta unlimited wewe.
 
Natamani
Utapata faida kubwa sana mkuu.
Mteja akija lazima anunue kitu ili apate WiFi.

Sometimes tunakaaga kwenye restaurant kufanya kazi,

Najua mwigulu anaichungulia hii fursa jinsi yakuweka aweze kutupiga na huku.
ufafanue zaidi hapa

Nikitaka Wi_fe apate mteja tu na sio mpita njia inawezekana kwa hapa dukani kwangu?
 
ndio mkuu, ninachohofia ni kama mteja anaweza kufanya matumizi makubwa ya data alafu kifurushi kikaniishia kabla ya mwezi, nafikiri hii huduma inaweza kuniongezea trafficking kwenye biashara hasa wanafunzi wakiwa ndio walengwa wakubwa
hapa mimi natumia unlimited speed 10mbs/sec ni 70000 kwa fiber
 
Back
Top Bottom