Fabrizio Romano azitambulisha jezi mpya za Kimataifa za Yanga. Hakika Yanga ni kubwa sanaaaa

Hiyo timu unaiona ni kubwa ni kubwa kwako sababu umeiweka mioyoni mwako,hiyo ni timu ya kawaida sana ina haki sawa na timu zingine zinazocheza premier league ya TZ.
 
Kushinda Ubingwa wa CAF kunahitaji UWEKEZAJI, yaani HELA. Hakuna mtu anayeweza kuwekeza kwenye timu yenye poor marketing. Jiuze katika soko kubwa upate wawekezaji wakubwa, wakupe timu Bora ili ushinde Mataji makubwa.
Yanga kwa level ya Uwekezaji wake imeunda timu Bora msimu huu, kadiri ya Uwekezaji unavyokua ndivyo ubora utakavyopanda.
 
Katambulisha jezi zenu personally mkamrekodi.

Sijaona hiyo habari kwa pages zake sababu anajua ni ndogo sana.
 
Kumbuka Yanga na Simba kwa uwekezaji wao huohuo wa kuungaunga walikaribia kutwaa kombe la shirikisho la CAF kila moja kwa wakati wake

Hata hizo robo fainali za CAFCL hawakua wanatolewa kwa aibu. Kulikua nafasi 50/50 kati yao na wapinzani wao za kusonga mbele ila bahati haikua yao

Pesa wanazotumia kusajili rundo la wachezaji hasa kutoka nje ya nchi ambao wengine viwango vyao ni vya kawaida sana wangezitumia kusajili wachezaji wachache wa level juu

Pamoja na kukubaliana nawe kuhusu kufanyika kwa proper marketing(fan base zao ni kubwa sana), matokeo ya uwanjani yanarahisiha mambo mengi kama hilo la kuvutia wawekezaji
 
Usajili wa mwaka huu kwa Yanga umeonesha thamani halisi kidogo ya Uwekezaji nadhani, hii inatia moyo kuwa, Uwekezaji wao ukikua unaweza kuleta mabafiliko makubwa zaidi kwenye ubora wa kikosi.
Na labda Uwekezaji katika ubora wa kikosi mwaka huu, unaweza kuvutia wawekezaji zaidi mbeleni, hasa kama kikosi hiki kitafika hatua kubwa katika mashindano ya Kimataifa.
 
Hyo ndy maana halisi ya usemi usemao.

Ukiona kobe juu ya mti ujuwe amepandishwa
Simba tayari yupo level za juu ahitaji drama kujitambulisha.
 
Vichwa vinavyo ongoza club hizi ni vile vya CCM ukitaka ufafanuzi njoo taratibu nikuchambulie uelewe
 
Shida sio amezindua nani..shida ya mashabiki na wapenzi wa Utopopolo ni uwezo wa Kununua hizo jezi..kama tu kiingilio cha sh. 3000 hadi walipiwe itakuwa jezi.
 
Jezi ya kimataifa haina logo ya CAF uto ni wajinga sana
 
Ligi ya tanzania bado haiwavutii wachezaji wa level za juu, bado simba na yanga hazina uwezo wa kupambana na timu kama al ahly, pyramids, mamelodi kiuchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…