Face to Face with Zitto Kabwe: Kuhusu Kupika Data, "Namheshimu Sana Rais Magufuli ila Sio Mkweli!. Uchumi Umesinyaa!.

HUYU KIJANA ANAJITAFTIA MAJANGA
 

Heshima kwako Mkuu Pasco.

Mkubwa hakosei ila huteleza, kwenye ishu ya Raisi kuwa kama baba, hapo kidogo umekanyanga ganda la ndizi mkubwa wangu.

Raisi (Political) ni kiongozi wa nchi anayechaguliwa na watu wa nchi au eneo husika.

Sasa tukianza kuwachukulia viongozi wa kisiasa kama wazazi tutakuwa tunapoteza maana ya Democracy.

***a system of government by the whole population or all the eligible members of a state, typically through elected representatives.
"a system of parliamentary democracy"****

Mfano: Kiongozi hatakiwi kukumbatia uzembe, ila mzazi humfanya mtoto awe mzembe.

Sasa ingekuwa vyema tusiweke hisia kwenye siasa. Hisia zibaki kwenye maswala ya Uzazi.

Tukianza kuweka hisia kwenye viongozi tuliowachagua itakuwa vigumu kuwawajibisha siku watakapo kosea. Ni kama baba mwenye nyumba akiwa anatembea na Housegirl.

Mkuu Pasco naheshimu sana hoja zako ila naomba kwenye hili tujaribu kutofautisha. Tujaribu kujitengenezea utaratibu ambayo utawafanya hawa tuliowachagua watutumikie badala ya sisi kuwatumikia.

Shukran.
 
Uzalendo utawezekana endapo baba mwenye familia ataipenda familia yake yote na c kwa kuwabagua.
"Huyu wa [emoji216] kijani ndio nampenda sana" lakini huyuuu[emoji111]!!!
TusteMegee Uzalendo kwa style hii
 
zito bwana; ukimsikiliza utagundua kuwa hana takwimu kinzani ili kubackup argument yake kwamba takwimu zilizopo zimepikwa. Alichonacho ni hisia tu zinazotokana na kile anachokiita tafsiri ya takwimu zilizopo. Tafsiri inayoweza kuwa potofu.

Sio afya sana kisiasa kuja public kwa msukumo wa hisia tu, unahitajika kuwa na ushahidi kwani tuhuma anazotoa yeye zinahitaji ushahidi.

Bila kuwa na takwimu kinzani hoja yake inakosa Mashiko.
 
Mnakubaligi ushahidi nyie mbululaz wa lumumba.
C mlipewa ushahidi wa gari lisilojulikana no. T............[emoji61] mbona mpaka leo kimyaaa.. eti gari halijawahi kutoka ndani ya arusha.
Nasari kaleta ushahidi wa mchakato wa ununuzi wa madiwani wa arusha mmemwambiaje? Shubbamiit[emoji83] cocrooche[emoji90]
Mbona hamuendi kununua madiwani wa mbeya mtwara?
.......Cyùuuuuuu[emoji117][emoji108]
 
Kwa akili zako fupi unahisi gavana ni mtu wa kujibu hoja za kiuchumi tu? Kwani uchumi ni nini au we uchumi unafikili ni pesa tu
 
Siku mkikutana tena na Zitto, usisahau kumuuliza njaa aliyotwaminisha kuwa ipo, mbona hadi leo hajawahi kufa mtu na hiyo njaa aliyo twaminisha, na xile takwima za kwamba maghala hayana chakula wakati chakula kilikuwemo kwenye maghala alizipika au hakuzipika?
 
Nachoshangaa hakuna kiongozi wa serekali ameliongelea suala na kulipa ufafanuzi zaidi ya kile alichokisema rais,lakini zitto kwa upande wake amewza kulielezea vizuri tukaelewa. Viongozi wa serekali mpo wapi kuelezea mambo haya msimuache raisi aeleze kila kitu!!..
 

Uko sahihi Zitto anapaswa na anastahili (na wananchi wote tunastahili) kujibiwa kwa hoja, si vitisho. Ila ni kweli si watu wote tunamwamini Zitto 100%. Ila akiibua maswali yajibiwe, bila kujali uwezekano kwamba amekula njama na watawala.
 
Sasa Paskali mbona ndio umemuumiza zaidi president wetu? Yaani ni kama umempa Zitto nafasi ya kushindilia vizuri msumari, Lol!!

Nishawaambia Zitto asipewe nafasi ya kujieleza, bado hatuna mtu wa kujibishana nae kwa hoja na data. Atatuumbua zaidi
Wewe ni kumwembe? , kama sie Basi mnafanana kwa fact
 
Zipo hoja za msingi kabisa ambazo zimetolewa na kijana Zitto, kwa mfano ujenzi wa treni za umeme ni kweli tumeomba msaada, au uenda tumekopa mabilioni ya fedha. Zitto, siyo wa kumpuuza kuna kitu hakipo sawa kwenye serikali hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…