FACT CHECK: Roma hakutekwa, alijiteka kwa maslahi binafsi ya kiMuziki

Swali muhimu ni hao waliotekwa walipatikana wapi??

Hapo ni wajibu wa police na serikali nzima ambayo imeonekana ikishutumiwa kujinasua katika hili na kuuthibitishia umma kwamba hao vijana walijiteka!

na nani kawapeleka polisi? walinyofolewa chimbo lipi?
 
Kaka huyo jamaa amezoea kuangalia movie za zombie na Bongo Movie..hana analojua kuhusu ujasusi na umafiaso. Msamehe tu ndio Great Thinker hao wapi likizo
 
Huu utetezi tungeweza ku uconsider kama bashite hangeropoka kuwa kabla ya jumapili watapatikana,

hapo ndo alipoharibu
 
Kweli kama wale waliovamia clouds walivyokuwa wapole.......ss na yule master wao aliesema watapatikana before jpili ndo tuseme nae alikuwa director wa hiyo muvi? Studio ni studio tuu....aliyevamia studio ya clouds ndo hyo hyo aliyevamia tongwe records.....afu anajishebedua kuwapata watekaj before jpili....p.u.m.b.a.v.u...
 
Hivi huko Lumumba huwa hamruhusiwi hata kutafakari na kuchanganua mambo japo kidogo sana!!!?
 
Maneno ya wapinzani na mitego yao ya kitoto kwa viongozi wa Serikali iliyoko madarakani, vinachekesha na kukinaisha.

Ukweli ni kwamba Kiongozi Mkuu Serikalini (Rais) ametamka hadharani (dunia nzima imesikia) kuwa "SIJARIBIWI". Ni ujumbe mzito kutoka kwa mtawala anayejiamini. Potelea mbali apachikwe majina na kusemwa maneno ya kila aina. Mwisho ni yule aliyeshika ncha ya kisu kukatwa tu.

Hivyo, upinzani unapaswa kutafuta jinsi nyingine na mikakati mipya ya kukabiliana naye, hasa inayogusa maslahi ya Wananchi moja kwa moja. Kwa sasa wanachokifanya wapinzani ni kutafuta huruma ya wananchi kulinda ufedhuri wao wa kudharau mamlaka kwa makusudi.

Hakika hadi 2020, wapinzani watakuwa wameisoma namba kama hawatabadilika. Na mwisho wake waambulie viti vichache vya uongozi katika nchi hii (Serikali za Mitaa na Bunge).

TUSIANDIKIE MATE. MWENYE MACHO / MASIKIO HAAMBIWI TAZAMA / SIKIA
 
Ha haaa haaaa habari nilikuwa nasubiri nione comment yako mkuuu!
Ni kweli hilo hata mimi nimejiuliza sana nikakosa majibu!
Safi sana kuliona hilo
 
Huu utetezi tungeweza ku uconsider kama bashite hangeropoka kuwa kabla ya jumapili watapatikana,

hapo ndo alipoharibu
Na siku zote Bashite hajui madhara ya matendo au maneno yake. Yaani ability ya ku-foresee madhara ya maneno au matendo yake ya Leo kwa ajili ya kesho iko chini sana . Hadi Leo nashangaa wanaoendelea kumwamini wanatumia vigezo gani?
 
Kakado kajipange upya kudanganya na hizo hela ulizopewa kufanya watu eti wanajiteka mwombe upya msamaha bibi yako inawezekana ulilogwa halafu hujijui ,Mungu akusamehe bure
 
Umeandika vizuri sana but kuna kitu hujaweka katika uchunguzi lakini kuna kasoro kidogo.
Umesema Roma alikuwa mzima kwa asilimia mia moja kitu ambacho sio kwl kutokana na maelezo ya wakili wake ambaye alithibitisha kuwa Roma hakuwa sawa na pia ukiangalia video wakati anashika kwnye gari alikuwa anachechemea.
Lakini pia naona katika uchunguzi wako ume base katika upande mmoja tu wakuwa Roma amejiteka na upande wa pili wa mkuu wa mkoa kuwa anahisika katika utekaji huo.
Kutokana na hoja hizo naona moja kwa moja uchunguzi wako haujakamilika.
 
Hakika hadi 2020, wapinzani watakuwa wameisoma namba kama hawatabadilika. Na mwisho wake waambulie viti vichache vya uongozi katika nchi hii (Serikali za Mitaa na Bunge).

TUSIANDIKIE MATE. MWENYE MACHO / MASIKIO HAAMBIWI TAZAMA / SIKIA

Wabadilike vipi sasa wapinzani, yaani huoni ninyi ndo mnapaswa kubadilika? Nyie watu sijui huwa mnalishwa nini!!!
 
Hii aina ya muandiko nahisi ni yule mkurugenzi wa shihata ya zamani siku hizi wanaita nini sijui wapo pale mbele bank house nae ni PhD holder ya pumba zile za miaka miwili kama baba Bashite
 
Wengi wa upinzani wanataka kujua ukweli gani au hadi mtekwaji aseme! Mbona mnaishi kwa nadharia tu ya chuki dhidi ya utawala uliopo, na kutokukubali ukweli.

Nasema hivyo nikiwa na uhakika kuwa Roma atakayosema kesho (kama akifanya hivyo) kinyume na matarajio yenu, humu mtajaza kashfa dhidi yake na utawala ati katishwa kutokusema ukweli.

Yangu masikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…