FACT CHECK: Roma hakutekwa, alijiteka kwa maslahi binafsi ya kiMuziki

FACT CHECK: Roma hakutekwa, alijiteka kwa maslahi binafsi ya kiMuziki

Siku chache zilizopita mwanamuziki maarufu wa miondoko yakufokafoka almaarufu Roma mkatoliki aliripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe record zinazomilikiwa na kijana jina maarufu (J mada),inasemekana ilikuwa ni majira ya usiku wavamisi walipowasili katika viunga vya ilipo studio hizo.

Kulingana na maelezo yaushaidi uliotolewa na shuhuda (the city) mwanadada aliyefika muda mchache kabla gari lawatekaji kuondoka alisema "ilikuja Noah nyeupe na wakashuka watu watatu,baada ya hapo wakatuamrisha mimi,bin Laden na wageni kutoka morogoro tuingie ndani ya geti,tulipoingia ndani ya geti walituuliza kwamba tumemkuta junior au tumemkuta Roma,tukasema junior hayupo ila Roma yupo ndani,wakatuamrisha Tukamuite Roma,tukamuita Roma,Roma akatoka akaulizwa wewe ndio ROMA na ilivyoonekana hawakumjua na pia walimuambia simu yake ipo wapi atokenayo Roma alitokanao sikuweza kujua nini kiliendelea kwa sababu waliongelea nnje ya gari,walirudi ndani wakamlazimisha binladen aingie studio akiwa amesindikizwa na mmoja wao na Wakarudi tena wakachukua TV zilizopo pale,wakatoka na imma walikuwepo wote ndani ya studio,studio ikabaki tupu,walivyotoka hapo wakaniambia mimi na wageni wengine waliotoka morogoro tusiende popote na nilichosikia baada ya hapo ni mshindo wa gari na gari kuondoka "

Fact:katika ushahidi wa shuhuda (Rozaree) umejidadavua watekaji hawakuwa na haiba yautekaji kwani kiwango Chao cha ustaarabu kilikuwa juu sana ukilinganisha na watekaji wengine tunaowasikia na hata kuwashuhudia.
Hoja ya kwanza (1):watekaji waliuliza tumemkuta Roma na wakatuambia tukamuite?? Niajabu kwa mtekaji kuwa na nidhamu ya namna hii, mara nyingi hutumia nguvu kuhakikisha wanatimiza lengo Lao,mtekaji gani huyu anaogopa kuingia ndani anawaambia mashuhuda nendeni mkamuite Roma ??
Hoja ya pili (2):watekaji wakamuuliza Roma,wewe ndio Roma.sikawaida kwa msanii maarufu kama Roma ashindwe kujulikana tena na hawa watekaji ambao kwa asilimia kubwa huenda wakawa ni vijana,tena vijana hawa ndio wapenzi namba moja wa mziki huu wakufokafoka unaoimbwa na Roma ni wazi na sio rahisi kutokumfahamu Roma.
Hoja ya Tatu (3):watekaji wakaingia ndani na binladen,picha tunayoipata hapa bado watekaji walikuwa na ustaarabu napo hawakutaka kuingia studio wenyewe bado waliitaji mtu mwenyeji waingie nae ndani, wavamizi wengi hutumia nguvu na wakati mwingine huwa hawajali Mali ya waliodhamiria kumteka hawa waliomteka Roma watofauti sana.viashiria hivi vya ushahidi wa rosare unatuonyesha wazi kunamaslahi binafsi yakisanà na wala siutekaji kama unavyoripotiwa..

Hoja ya 4.watekaji wakatuambia tusiondoke
.watekaji baada yakuwachukua wahusika wakuu waliwaamuru the city na wenzake wasiondoke hii inamaana bado walitaka kuhakikisha usalama wa studio unakuwa salama hivyo walionyesha kujali na kudhamini Mali na vifaa vinginee vya studio. hali isiyo ya kawaida mtekaji kuhakikisha ulizi wa Mali za mtekwaji.

Upande wa mmiliki wa Tongwe record :nae mmiliki wa Tongwe record aliskika akiongea akisema "usiku wa jana likitokea tukio lakutisha sana,walikuja watu ambao hawakufaamika wametoka wapi au wametumwa na nani,bahati nzuri mimi si kuwepo studio,wakamuhoji ROMA baada ya kumuhoji Roma wakamuhoji na monie ambaye ni msanii wangu pia kutoka Tongwe record baada yakumaliza mahojiano yao wakaingia ndani studio wakachukua TV, computer pamoja na kamera"

Maelezo ya mmiliki wa studio na shuhuda namba moja hayatofautiani sana bado yote yanaukakasi wa kiwango cha ustaarabu wa hawa watekaji.

Hoja watekaji walimuhoji ROMA.ni tanzania pekee watekaji hupata muda wakuhoji mtekwaji,sidhani kama inaingia akilini kuskia mtekaji anaweza kufanya interview na mtekwaji,nguvu na ubabe huwa hawana muda wa kuwa wakarimu na kuchukua maelezo mara zote watekaji hawana huo muda,ili lililotokea kwa Roma ni maigizo yenye maslahi binafsi.

Kauli ya mkuu wa mkoa mh.Paul makonda.mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa ni haki na wajibu wake kuhakikisha mkoa unakuwa salama pamoja na Raia wake,ni haki na sahihi mkuu wa mkoa kuingilia kati upotevu wa watu wake.

Mh.Makonda aliskika akisema
"bado tunayomamlaka yakudhibiti kila aina ya utekaji na kuhakikisha wanannchi wetu wanaendelea kuwa salama,sambamba na hilo nawapa imani tu haitafika jumapili tutakuwa tumeshawapata ndugu zetu wote wanne na mimi naomba kwa dini zetu kwa imani zetu kila mmoja kokote kule alipo aombe ili tuhakikishe ndugu zetu tunawarejesha wakiwa salama.

Kutokana na kauli ya mh Paul makonda imepelekea watanzania kijuiliza maswali kadhaa.

Hoja ya kwanza (1).
kauli ya haitafika jumapili Roma na wenzake watakuwa wamepatikana.Niwazi kauli hii ni Tata na ilikuwa na viashiria vya huenda kuna Jambo muheshimiwa alikuwa analifahamu zaid, tena ukizingatia huwa anaukaribu na vijana hawa wanaofanya sanaa,nikweli jumapili hajafika na vijana wamepatikana,mh ni kijana anajua mbinu nyingi za vijana wenzake wanazotumia kujipatia umaarufu nadhani alishashtukia na akatoa kauli iliyojipambanua kuna kitu anafahamu.

Hoja ya pili (2).kauli yakuwarejesha Roma na wenzake wakiwa salama nayo ni moja ya kauli iliyotolewa na mh mkuu wa mkoa tutawarejesha wakiwa salama kauli hii nayo iliashiria mchezo mzima huenda mkuu wa mkoa alikuwa anajua mahali alipo mkatoliki.

Uchambuzi wa kauli ya mhusika mkuu (Roma)
.Roma mara baada yakupatikana alipelekwa kituo cha Polisi ambapo naamini aliacha maelezo yakutosha.

Roma aliskika akisema " kutokana na mazingira na situation nzima hatutakuwa na muda mrefu wakuzungumza, kwakifupi tu niwaakikishie mimi ni mzima mpaka Sa hivi kiafya na kiakili hata monie,bin LadenI wote tuwazima wa afya,niwaakikishie sisi wote ni wazima tunaendelea vizuri"


Hoja ya kwanza (1)
.nifuraha kuskia wapo salama ila yapo maswali ya kujiuliza nini hasa lengo la watekaji je ni kweli watu hawa walitekwa? ni kweli mtekaji anaweza kuwateka wasipigwe hata vibao kimoja kiasi cha kuachiwa wakiwa 100% sawa bila jeraha na hata mkwaruzo wowote?

Hoja namba mbili (2).mavazi ya Roma siku anatekwa na siku anaonekana,siku anatekwa Roma aliripotiwa kuwa alikuwa amevaa t shirt nyeupe suruali ya blue aina ya Jinsi, ila siku anapatikana alionekana akiwa na mavazi meusi .Niwazi uko alikokuwepo alipata fursa ya kupata huduma muhimu kama kuoga na hata kubadilisha nguo bado kuna ulakini wa aina hii ya utekaji,sio rahisi kwa watekaji kuwa na moyo wa namna hii vijana wasanaa inaonekana walikuwa bado katika mwendelezo wa sanaa yao,haingii akilini aina hii yautekwaji kwakweli.

My take.tusishangae na kuskia nyimbo mpya ya Roma katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa,attention aliyokusudia kuipata amefanikiwa kwa 100% otherwise kesho siku ya jumatatu atuambie wa Tanzania hoja nzito kutuakikishia ni kweli alitekwa na sio kutafuta umaarufu kisanaa.

Hapo huenda ni kudhulumiana au pesa, au mapato ya nyimbo, au mashahiri su beat ya mziki...hakuna siasa, wala serikali hapo
 
Maneno ya wapinzani na mitego yao ya kitoto kwa viongozi wa Serikali iliyoko madarakani, vinachekesha na kukinaisha.

Ukweli ni kwamba Kiongozi Mkuu Serikalini (Rais) ametamka hadharani (dunia nzima imesikia) kuwa "SIJARIBIWI". Ni ujumbe mzito kutoka kwa mtawala anayejiamini. Potelea mbali apachikwe majina na kusemwa maneno ya kila aina. Mwisho ni yule aliyeshika ncha ya kisu kukatwa tu.

Hivyo, upinzani unapaswa kutafuta jinsi nyingine na mikakati mipya ya kukabiliana naye, hasa inayogusa maslahi ya Wananchi moja kwa moja. Kwa sasa wanachokifanya wapinzani ni kutafuta huruma ya wananchi kulinda ufedhuri wao wa kudharau mamlaka kwa makusudi.

Hakika hadi 2020, wapinzani watakuwa wameisoma namba kama hawatabadilika. Na mwisho wake waambulie viti vichache vya uongozi katika nchi hii (Serikali za Mitaa na Bunge).

TUSIANDIKIE MATE. MWENYE MACHO / MASIKIO HAAMBIWI TAZAMA / SIKIA

Natamani ingetokea mtu akaanzisha chama kingine cha upinzani, ili kichangamshe serikali na maendeleo nchini yaonekane.

Wana matumbo yamejaa njaa, hawajali wananchi kabisaaaaaaa.
 
Swali muhimu ni hao waliotekwa walipatikana wapi??

Hapo ni wajibu wa police na serikali nzima ambayo imeonekana ikishutumiwa kujinasua katika hili na kuuthibitishia umma kwamba hao vijana walijiteka!
Naungana nawe katika kuhoji hili
 
Porojo tu utatoaje fact wakati maelezo kwa alietekwa bado

Waliosema wametekwa wamejipa muda mrefu kusema wanayotaka kusema.

Wale walioongea na mapaparazi alipotokomea, ni muhimu sana sana katika jambo hili.

Mkewe pia.
 
Nimependa, ngoja nikae mkao mzuri wa kula nisome nikila butter popocorn.

Nimemaliza ungeongezea kuwa kalipwa pia na kuahidiwa mengi na walio nyuma ya kumchafua RC na Raisi wetu. Yote haya ni madawa, upinzania etc

Watanyooka tu

Awamu hii sio ya kujaribu blah blah blah
Halafu bwana Nape eti "Roma Oooooh No"
 
Waliosema wametekwa wamejipa muda mrefu kusema wanayotaka kusema.

Wale walioongea na mapaparazi alipotokomea, ni muhimu sana sana katika jambo hili.

Mkewe pia.
Lazima wajipe muda ili wawe sawa kisaikolojia kwani kuna uharaka gani
 
Poleni sana JF kwa kubeba kila kitu .
Na kama kuna mtanzania ataunga mkono Jf kufungiwa nitamshangaa sana. Mtandao ambao haubagui nani aseme nini , wakati gani, mahali gani!! Eti huyu naye kaleta uchambuzi huku akijua wazi uchambuzi wake una matobo kama chandarua? Halafu Mods wamemwachia ajimwage anavyojisikia na washabiki wake kina chaneli koko wamejitokeza eti na "popkorn" kumuunga mkono, halafu ajitokeze mtu aseme Jf ifungiwe?? Hoja gani ya yenye uzito wa kuonyesha ukweli wa mleta mada? 1.Kwamba watekaji walitakiwa wavae ovyo ovyo? Hoja dhaifu kuliko zote ni hii, mtoa mada anategemea watekaji wavae marapurapu kwa vile tu kitendo wanachokifanya ni uhalifu? Hiyo dunia ilishapita, majambazi wanavaa suti siku hizi.
2.Kwamba watekaji walitakiwa wawe na sura za kikatili? Huu ni udhaifu wa kuvamia taaluma za watu bila kujijua. Siku hizi mtu anakuua kwa kukununulia kinywaji na kukaa naye kirafiki.
3.Kwamba watekaji walitakiwa wawe wanamjua Roma vilivyo kwa vile anafahamika nchi nzima? Mbona kuna mtu mzima anaitwa Le mutuz alipost hamjui kabisa huyo Roma wenu, na hamkumshangaa mnashangaa watekaji?
4.Kwamba watekaji waliwaambia wasiohusika mbaki hapo hapo? Yaani mlitaka wawaambie nendeni kituo cha Polisi mkatoe taarifa? Walichokifanya watekaji ndicho walichotakiwa kufanya, wale wabaki hapo mpaka watakapotokomea.
5.Kwamba Rc kusema watarudishwa kabla ya jumapili wakiwa salama na ikatokea kweli ni kwa vile yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama? Hoja yenye utani mwingi hii!! Watu wametekwa, wenzao wakaitisha kikao wakasema wewe Rc warudishe wenzetu "maana una uwezo wa kufanya hivyo", nawe kama Rc bila kujiuliza undani wa kauli hiyo unajitokeza na kusema "watarudi kabla ya jumapili tena wakiwa salama", na kweli jumamosi wanaonekana tena wakiwa salama kama ulivyoahidi!! Ni wangapi kwenye mkoa wako wamepotea au kufanyiwa uhalifu ukatoa tamko tu wakaonekana?
6.Kwamba mateka mmoja amerudi na nguo tofauti na alizotekwa nazo? Ukiangalia kwa nje unaweza kuiona ni hoja nzito, lkn hata wote wangeweza kupewa nguo tofauti hasa nyeusi kukidhi matakwa ya watekaji na kuendana na mazingira.
7.Hoja nyingine ni dhaifu kiasi cha kutohtaji majibu.
 
"[/COLOR]

Hoja ya kwanza (1)
.nifuraha kuskia wapo salama ila yapo maswali ya kujiuliza nini hasa lengo la watekaji je ni kweli watu hawa walitekwa? ni kweli mtekaji anaweza kuwateka wasipigwe hata vibao kimoja kiasi cha kuachiwa wakiwa 100% sawa bila jeraha na hata mkwaruzo wowote? [/I]

Si alikua anachechemea yule?
Au na wewe umehadithiwa?? Kijana jipange na propaganda zako mfu
 
Haaaa. Yaani wewe mleta uzi umetumwa na nani kuleta uongo humu? Kawaaminishe bashite wenzako wewe. Inaonekana umejiunga Leo ili kupooza maneno!! Kwani watekaji unataka waje na bunduki ndo uamini? None sense
Kuhusu nguo inamaana ujajua kuwa Ruge aliwapata tangu usiku?
 
""""" hahahahahahahah nguo zimeshuka bei? mana sikukuu hii naona hali mby""""""""'''' ha!!! kumbe mnazungumzia ROMA?
 
Haaaa. Yaani wewe mleta uzi umetumwa na nani kuleta uongo humu? Kawaaminishe bashite wenzako wewe. Inaonekana umejiunga Leo ili kupooza maneno!! Kwani watekaji unataka waje na bunduki ndo uamini? None sense
Mkuu hapo kwenye nguo vipi jamaa alibadilisha. Au
 
Watekaji wa tanzania sio kama unaowaonaga kwenye muvi za ulaya. Huku hata makachero wa usalama wa taifa wakiambiwa watoe vitambulisho huwa wanatoa bastola.
Uongo wangu upo wapi mkuu fafanua kwa fact kiongozi
 
Wewe ni muandishi mzuri 95%
Lakini sio mtoa hoja mzuri 20%
 
d377fb5a6902aafc2d581080421a3522.gif

Mmmhhh mpaka hili boksi la popcon liishe ntakuwa nmeona vya kutosha... j3 ni mwendo wa karanga na all eyes on radio&Tv...wapi mzee wa kuwafunulia watu mixer udaku na facts in issue[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] LMAO
 
Lumumba ndio wapi, inakuuma nini wewe kie kumsoma na kujilia popcorn?

Wewe wa kutafakari andika yako, muache aliyeamua amejitahidi.


Mengine siongezi, nimeamua kumpa support na kulike juu... tu ha ha haaaaa jipige vibao vya usoni.
Hahahaa!!! Ngoja nijitandike vibao pah pah pahh! ila Cocochanel punguza mahaba na ccm dahhh!!!
 
d377fb5a6902aafc2d581080421a3522.gif

Mmmhhh mpaka hili boksi la popcon liishe ntakuwa nmeona vya kutosha... j3 ni mwendo wa karanga na all eyes on radio&Tv...wapi mzee wa kuwafunulia watu mixer udaku na facts in issue[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] LMAO
 
Back
Top Bottom