FACT CHECK: Roma hakutekwa, alijiteka kwa maslahi binafsi ya kiMuziki

Mmeshaitoa ile picha ya muasisi wa taifa kwenye ile nanihii yenu kama sheria inavyowataka? Itoeni basi!
 
Mtoa uzi unachekesha. Sijasoma yote ila kitendo cha kulazimisha huo ni utekaji tosha.
Kwa akili yako inawezekanaje mtu akuamlishe ukubali?
Wakaingia ndani, wakamlazimisha Roma achukue simu, na wakabeba na Tv.
Hiv kwa akili yako tu mtu aje kwako, akuambie chukua simu,na achukue Tv unamuangalia tu, tena humjui ni kwa mara ya kwanza halafu anakuambia panda kwenye noah twende. Halafu unapanda, wanaondoka na ww, hapo kwenu hawajui wala mke wako. Simu haipatikani halafu unasema hawajateka. Km hivyo ni raha sana
basi mtoa uzi mm nakuja kwako, namchukua mkeo, pamoja na simu ya mkeo na nitamrudisha mkeo siku 5 kupita. Sawa?
 
Mtoa mada inaonekana hauna uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Uhalifu wa Utekaji na other Organised Crimes. Picha uliyonayo kichwani ni ya "UJAMBAZI" ambao kwa bahati mbaya sana una ilinganisha na "UTEKAJI", kwa kukusaidia tu Watekaji usidhani labda walikua na shida ya kuharibu studio au mali nyingine au kuua mtu, watekaji hawana tamaa ya hizo mali ila wanaangalia ni kitu gani wameagizwa na ni "VALUABLE" cause ya utekaji wao. Mfano wamechukua Kompyuta inayotumiwa kutengenezea nyimbo hiyo ni valuable asset kwao kwa sababu aliyetekwa ni msanii/wasanii na mtayarishaji wa muziki hivyo basi kazi zao huifadhiwa humo kwenye kompyuta. Hata wangekuta Bilioni 100 mezani wasingezigusa unless kama wao wangekua ni Majambazi.

Pia unazungumzia kuhusu roma kubadilisha nguo. Hii ni hoja dhaifu sana, umejiuliza Roma kabla ya kufika oysterbay alitokea wapi?

Pia unashaka juu ya waliotekeleza tukio la utekaji kutokumfahamu Roma eti kisa ni Vijana na Roma ni Msanii. Je una uhakika gani kama waliomteka ni Watanzania? Kila kijana usidhani yuko busy na wasanii.

Kwa kuhitimisha nimeona umejikita sana kwenye hoja ya watekaji kua WASTAARABU, hii ni hoja ya ajabu sana inaonekana wewe ulitarajia waanze kufyatua risasi hewani. HIZI KAZI HAZIFANYIKAGI HIVYO.

Bonafsi nongependa kukushauri ujikite zaidi kwenye kujiuliza kwanini Ndugu Daudi Bashite awe na uhakika juu ya watekwaji watapatikana Lini?, kwanini ahadi yake itimie? Je anakipi anachokijua nyuma ya pazia?.

Hili suala la Daudi Bashite kusema hawa watu watapatikana kabla ya siku fulani na kweli ikatokea sio dogo hata kidogo, ila kwa sababu hii ni Tanzania hakuna atakaye muhoji lakini nakuapia hili suala angelizungumza kwenye nchi za dunia ya kwanza basi yeye ndio angekuwa suspect namba MOJA.

Mwisho kabisa Elewa kilichofanyika ni Utekaji sio UJAMBAZI. Vyote ni UHALIFU katika mizania tofauti.
 
huyu mtu kesho kwanza aanze kutupa identity yake kama roma mkatoliki ni nani..ni elibariki..au ibrahim mussa. tusipoangalia kama taifa tutachezewa na wakora wa mtaani.
 
NGOJA TUONE JUMATATU ATASEMA NINI.
BUT SIWEZI KURUHUSU AKILI YANGU IKUBALI NI KWELI ULIKUWEPO UTEKAJI.

UMETEKWA ALAFU UNASEMA NIATASEMA JTATU!!!?
DR ULIMBOKA ALIPOONEKANA TU ALIANZA KUSEMA ILIVYOKUWA AKIWA KWENYE GARI ANAPELEKWA HOSPITALI.

UMETEKWA UNASEMA NITASEMA JTATU!!?
UNATAKA UKAANDAE HOTUBA!?
ALAFU WATU WANAAMINI KWELI.
HAPA KUNA KITU KATI YA HAWA WASANII NA RC MAKONDA, SISI TUNACHEZA NGOMA ZAO.
 
Wabadilike vipi sasa wapinzani, yaani huoni ninyi ndo mnapaswa kubadilika? Nyie watu sijui huwa mnalishwa nini!!!
Umenukuu sehemu tu ya hoja zangu, ukaacha yenye jibu la swali lako. Rejea bandiko langu.
 
Mleta mada kwanini usisubili mtendewa akasema nini kilitokea? Ukalinganisha na kutoa maoni yako subili mtekwaji atoe yaliyo moyon
 
Watekaji waliotumwa na serikali hawaitaji kuogopa maana wanakuwa wanatekeleza kazi waliotumwa.kwahyo hamna kizuizi cha kuwatisha.lakini watekaji ambao awajatumwa na serikali wao wanafanya fasta fasta wakiogopa kukamatwa na serikali.


Nimekujibu kipumbavu kama ulivyotoa hoja zakipumbavu.
 
Cheki mtanzania ambae hafati mkumbo wa kukurupuka alivyo tumia akili kufikiri na kuja na hoja zinazo jaribu kutuonyesha sura ya pili ya hili tukio,hongera kwa kuumiza kichwa kufikiri kiasi hiki.
 
Umelipwa sh ngapi na [HASHTAG]#Bashite[/HASHTAG]
 
Kajiteka haf kuna mtu anatabiri kabla ya jumapili atapatikana
 
Kila mtu siku hizi amekuwa mchambuzi wa masuala ya usalama

Yaani Tanzania kila mtu ni TISS
 
Hivi huko Lumumba huwa hamruhusiwi hata kutafakari na kuchanganua mambo japo kidogo sana!!!?

Lumumba ndio wapi, inakuuma nini wewe kie kumsoma na kujilia popcorn?

Wewe wa kutafakari andika yako, muache aliyeamua amejitahidi.


Mengine siongezi, nimeamua kumpa support na kulike juu... tu ha ha haaaaa jipige vibao vya usoni.
 
Nimeamini wewe ni bashite!!! Unawaza kibashite bashite tu watekaji walikuwa na akili timamu sio akili
kama zako!!

Huenda mazingira aliyokuwa roma kulikuwa na ulinzi kwaiyo wale walijua hilo hawawezi tu kipiga piga risasi na kuamrisha amrisha tu kila mtu ajue nini kinaendelea
Wasingefanikisha zoezi lao gari lingefuatiliwa na taarfa zingesambaa haraka sana wangekamatwa tu au wasinge toka nae pale

lakini huenda wakati wanaongea na roma walimueleza hali halisi kwamba ukifanya akajua hata mtu mmoja hapa kinachoendelea tutakuua hapahapa fanya kama hamna kinachoendelea fanya kama tulivyokuagiza tuondoke kwa hiyo mtu wapembeni kama uyo dada aliyetoa ushaidi ataona nimaongezi ya kawaida tu yalikuwa yanaendelea pale

Unasema roma amerudi akiwa mzima kabisa??? Sio kweli!! Roma kutembea mwenyewe hawezi anasaidiwa kutembea ila amesema ni mzima kabisa kwa sababu ya usalama wake ndio kama nilivyokwambia vitisho alivyopata sio vya kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…