Fact Checking: Rais Magufuli hukumteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya kumaliza Ubunge wa Muleba

Kama unamsikiliza Lissu vizuri huwa anaeleza hali iliyopita, ilivyo sasa na yeye atafanya nini akichaguliwa.
mie nasikia tu risasi,sijui mguu haunyooki,magufuli aleze walionipiga risasi wameenda wapi
 
wewe ndio Muongo
Magufuli alirudisha nyumbani mabalozi wote,waliotemwa wakatemwa,waliorudi wakarudi na wapya wakaingia
Yupo sahihi kwa kuwa alimfanyia extension,muda wa Masilingi kustaafu umepita bwashee,acha kusema Rais wetu muongo

Hajasema alimfanyia extension kasema kamteua.

Kufanya extension haimaanishi kuteua, ni kuextend uteuzi uliopo.

Hata ukifikisha umri wa kustaafu, haustaafu mwenyewe mpaka upewe barua ya kustaafu.
 
Aseme Ukweli

Watu walikuwa wanamsikiliza huku kimoyomoyo wakijisemea huyu mzee haoni haya kupiga watu kamba mchana kweupeee?

Kama anapiga watu kamba kwa vitu obvious kama hivi, Je, ni kweli atatimiza ahadi anazozinadi kwenye kampeni?
Kwani angeshindwa kumtumbua na kumchagua mwingine!? Kitendo cha kubaki ni Sawa na kuchaguliwa.
 
Mkuu Kiranga , during campaign time, what matters most is not about facts, just politics.
P

Mkuu,

What matters most to whom?

In any case, Magufuli "being economic with the truth" is not limited to campaign time.

Yani rais mpinga rushwa anakataza CAG asikague vitabu vya ATCL?

Rais mtetezi wa wanyonge anasema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao, na hapo hapo anasema maendeleo hayana chama, na hapo hapo anasema msipomchagua mgombea wa CCM hamtapata maendeleo?

Is this directionless pitter-pattering what passes for politics these days?
 
oktoba utajua kuwa hujui kuchambua
 
Mkuu Kiranga, what matters most to Tanzanians.
Hakuna mtu yoyote aliyesema Magufuli ni malaika!. Magufuli is just a human being, just like you and me, and he can do mistakes, lakini tukubali, tukatae, Magufuli anafanya makubwa mazuri kwa nchi hii, anastahili kuongezewa miaka mitano tena, not as a favour kumpendelea au kumhurumia, but deserving, anastahili!.
P
 
Jamaa anajipendekeza kupitiliza kisa kutafuta uteuzi.
 
Jamaa anajipendekeza kupitiliza kisa kutafuta uteuzi.
Duh, Mkuu Kishina cha Mshahara, mtu anayejipendekeza kupitiliza ili kutafuta uteuzi, si kazi yake itakuwa ni kusifu tuu?!, atathubutu kukosoa?. Mimi humu kila siku ni mkweli daima, kwenye mazuri, nitasifu, na kwenye mabaya nitakosoa.
Angalia tarehe ya bandiko hili,

Halafu uniambie hili ni bandiko la mtafuta uteuzi?
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Uchaguzi, (NEC), Lawamani Kuwaengua Wagombea Kwa Hoja Nyepesi Nyepesi, Je ni Ukiukwaji wa Haki za Binaadamu? Jicho Letu
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…