Fact Checking: Rais Magufuli hukumteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya kumaliza Ubunge wa Muleba

Fact Checking: Rais Magufuli hukumteua Masilingi kuwa Balozi Marekani baada ya kumaliza Ubunge wa Muleba

Kama unamsikiliza Lissu vizuri huwa anaeleza hali iliyopita, ilivyo sasa na yeye atafanya nini akichaguliwa.
mie nasikia tu risasi,sijui mguu haunyooki,magufuli aleze walionipiga risasi wameenda wapi
 
wewe ndio Muongo
Magufuli alirudisha nyumbani mabalozi wote,waliotemwa wakatemwa,waliorudi wakarudi na wapya wakaingia
Yupo sahihi kwa kuwa alimfanyia extension,muda wa Masilingi kustaafu umepita bwashee,acha kusema Rais wetu muongo

Hajasema alimfanyia extension kasema kamteua.

Kufanya extension haimaanishi kuteua, ni kuextend uteuzi uliopo.

Hata ukifikisha umri wa kustaafu, haustaafu mwenyewe mpaka upewe barua ya kustaafu.
 
Aseme Ukweli

Watu walikuwa wanamsikiliza huku kimoyomoyo wakijisemea huyu mzee haoni haya kupiga watu kamba mchana kweupeee?

Kama anapiga watu kamba kwa vitu obvious kama hivi, Je, ni kweli atatimiza ahadi anazozinadi kwenye kampeni?
Kwani angeshindwa kumtumbua na kumchagua mwingine!? Kitendo cha kubaki ni Sawa na kuchaguliwa.
 
Mkuu Kiranga , during campaign time, what matters most is not about facts, just politics.
P

Mkuu,

What matters most to whom?

In any case, Magufuli "being economic with the truth" is not limited to campaign time.

Yani rais mpinga rushwa anakataza CAG asikague vitabu vya ATCL?

Rais mtetezi wa wanyonge anasema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao, na hapo hapo anasema maendeleo hayana chama, na hapo hapo anasema msipomchagua mgombea wa CCM hamtapata maendeleo?

Is this directionless pitter-pattering what passes for politics these days?
 
Mkuu Missile of the Nation, kwanza Asante kwa bandiko lako la facts checking na asante kutuwekea video clip ya Magufuli alichosema Muleba, Magufuli is very right.

Amesema Masilingi aliteuliwa balozi baada ya kumpisha jimbo Mama Tibaijuka, hata kama mwanzo aliteuliwa na JK, baada ya Serikali mpya kuingia madarakani, Rais mpya anawateua upya mabalozi wote, ma RC wote na ma DC wote, hata kama mwanzo waliteuliwa na mtangulizi wake, re appointment amefanya yeye, hivyo he is right Magufuli amemteua Masilingi.

Moja ya sifa za ziada za Magufuli ni Mkweli Daima!.

Nawashauri Watanzania wenzangu, Wazalendo wa kweli wanaolitakia mema taifa hili, October 28 tusifanye makosa!.
P
oktoba utajua kuwa hujui kuchambua
 
Mkuu,

What matters most to whom?

In any case, Magufuli "being economic with the truth" is not limited to campaign time.

Yani rais mpinga rushwa anakataza CAG asikague vitabu vya ATCL?

Rais mtetezi wa wanyonge anasema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao, na hapo hapo anasema maendeleo hayana chama, na hapo hapo anasema msipomchagua mgombea wa CCM hamtapata maendeleo?

Is this directionless pitter-pattering what passes for politics these days?
Mkuu Kiranga, what matters most to Tanzanians.
Hakuna mtu yoyote aliyesema Magufuli ni malaika!. Magufuli is just a human being, just like you and me, and he can do mistakes, lakini tukubali, tukatae, Magufuli anafanya makubwa mazuri kwa nchi hii, anastahili kuongezewa miaka mitano tena, not as a favour kumpendelea au kumhurumia, but deserving, anastahili!.
P
 
Inaelekea hujaisikiliza hiyo clip vizuri, au kama umeisikiliza umeamua kuweka pamba masikioni.

Magufuli anasema alimteua Masilingi kuwa balozi baada ya kumaliza ubunge wake, ukweli ni kwamba Masilingi alikuwa balozi Netherands kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, wakati huo Magufuli ni waziri katika serikali ya Kikwete

Kisha Masilingi akateuliwa na Kikwete mwaka 2015 mwezi Agosti kuwa balozi wa Tanzania Marekani. Kwa hiyo JPM anavyodai kuwa alimteua Masilingi kuwa balozi baada ya ubunge wake siyo kweli. Ni kikwete ndiye aliyemteua.

Tunataka Raisi msema kweli
Jamaa anajipendekeza kupitiliza kisa kutafuta uteuzi.
 
Jamaa anajipendekeza kupitiliza kisa kutafuta uteuzi.
Duh, Mkuu Kishina cha Mshahara, mtu anayejipendekeza kupitiliza ili kutafuta uteuzi, si kazi yake itakuwa ni kusifu tuu?!, atathubutu kukosoa?. Mimi humu kila siku ni mkweli daima, kwenye mazuri, nitasifu, na kwenye mabaya nitakosoa.
Angalia tarehe ya bandiko hili,

Halafu uniambie hili ni bandiko la mtafuta uteuzi?
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Uchaguzi, (NEC), Lawamani Kuwaengua Wagombea Kwa Hoja Nyepesi Nyepesi, Je ni Ukiukwaji wa Haki za Binaadamu? Jicho Letu
P
 
Back
Top Bottom