hizi ni simulizi tu za watu wenye hekima, wakati taifa la iziraeli walipoingia kwenye matatizo watu wenye hekima wakaandika maandiko hayo kuwapa mwongozo wa jinsi kuvumilia na kuondokana na matatizo
Ayubu alikuwa anaishi mji wa UZI muji ambao haujapa kuwapo tangu dunia ianze kuwapo, jaribu kuangalia ramani zote za kibibilia za zamani hakuna mji km huo.
Umemzunguza MUHIBIRI wajua hicho kitabu kiliandikwa na nani? mbona humtaji mwandishi wake?
kwa maelezo yako yoooote uloeleza hapo juu naomba tuanze na asili ya binadamu
kwanza tambua kuwa bibilia hiyo iliandikwa kwa madhumuni ya ujenzi wa taifa la Iziraeli tu hivyo walikusanya mambo mema na mabaya wakayaita yote ni ya Mungu, na uandishi wa bibilia mambo mengi yametokana na simulizi za miungu ambazo zimekarabatiwa mfano unapoamini kwamba utatu wa Mungu, Mungu baba, Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu, miungu hawa walikuwapo kabla ya Ibrahimu, cha ajabu wewe unaamini Miungu wa tatu wakati Ibrahimu unayedai kuwa ni baba yako wa imani alisema Mungu mmoja, imekuwaje wewe unaamini miungu wa tatu?, unasema Mungu wako ana mtoto mmoja ambae ni Yesu kwa upande wapili (Waisilamu) wanadai Mungu hazai kwakuwa hana mke,
science ni neno la kigiriki lenye maana ya maarifa, maana yake maarifa ni science na bibilia yako inasema hivi kumcha bwana ni chanjo cha maarifa yaani Science kwa maana nyingine Science inatokana na Mungu sio Dini.
kwa hiyo dini ni tegemeo la wajinga na wapumbavu, baali Mungu ni tegemeo la watu wenye busara, hekima na maarifa
pole yako unootegemea dini, Mungu hatafutwi kupitia dini anatafutwa kupitia maarifa ambayo ni Science
Sikatai kwa kila msaafu wa dini yapo mambo mazuri yanopaswa yazingatiwe, na mengine ni mambo yaliyopitwa na muda kwa bahati mbaya dini zinakazania mambo yaliyopitwa na wakati
Swali la kizushi, km leo Mungu angelipuliza kipenda na kutangaza kuwa amefuta adhabu ya kifo binadamu hatutokufa tena na kila kitu binadamu anachokihitaji atapata bila masharti yeyote, hivi kuna atae enda nyumba ya ibada kuomba? na km ataenda ataenda kuomba nini?
dini zilianzishwa na wanadamu kumshawishi Mungu awaondolee kifo, ndio sababu kila dini inastahili yake ya kumwendea Mungu, wengine hulia, wengine hupiga magoti, wengine husali uchi, lkn staili zote hizo zimeshindwa kumridhisha Mungu kuwaondelea wanadamu kifo, dini zilipoona kwamba wanadamu wanaendelea kufa wakaja na ushawishi mwingine kwa maana ya kwamba hata binadamu akifa ataenda mbinguni wataishi milele, simulizi ya maisha ya umilele huo zinatofautiana kati ya dini na dini wengine wanadai huko hakuna kula wala kunywa ni kusifu tu, wengine wanassema kule kuna vinywaji vitamu na kuhudumiwa na vimwana wazuri, je ukweli ni upi? nani aliyekwenda mbinguni na kurudi?
1:hizi ni simulizi tu za watu wenye hekima, wakati taifa la iziraeli walipoingia kwenye matatizo watu wenye hekima wakaandika maandiko hayo kuwapa mwongozo wa jinsi kuvumilia na kuondokana na matatizo
----> umeamua kurahisisha. Matatizo gani, Lini, Yalisababishwa na nani, Mbona bado wanamatitizo mengi pamoja na uwepo wa maandishi hayo, nielezee mfano wa nchi iliyoondolewa matatizo kwa maandishi,
Mfano tu Jerusalem Imebomolewa Mara Mbili, Imezungukwa na kutekwa mara 23, Imeshambuliwa mara 52, Mara 44 imekuwa captured and recaptured. Niambie kwa source na evidence wazo hilo walilitoa wapi na anani alilileta . Yaani kwa ufupi natakiwa uelezee Who, When, Where,What, Why and How kama uko tayari tujadili kwa hoja. Maana bibilia haijaelezea au kuandikwa na waisrael tu maana hata Ruth hakuwa muisrael, Baba wao wa imani Ibrahim hajawahi kuwa muisrael na wengine wengi.
Ayubu alikuwa anaishi mji wa UZI muji ambao haujapa kuwapo tangu dunia ianze kuwapo, jaribu kuangalia ramani zote za kibibilia za zamani hakuna mji km huo.
----> UZI
kwanza sio kila mji umeandikwa kwenye kitabu upo kwenye ramani, ingekuwa hivyo na bustani ya edeni na miji ya awali kabla ya gharika ingekuwepo. Unapouliza kuhusu UZ, inabidi uulize miji kama Misri,Kushi, kanani maana yote iliwanza kwa kwa majina ya watu au familia, kutambulika hadi kufikia kiwango cha kutoka kwenye ramani inategemea na Ukubwa, na umaarufu ya mji yawezekana mji ukawa ndani ya mji mwingine mkubwa kabisa zaidi ya huo na ukamezwa.
Baadhiu ya ushahidi wa Uwepo wa UZ physically
1: Soma Mwanzo 10:23, 1 Nyakati 1:17 UZ ni jina la mtu kama walivyo au familia na baadae ikawa mji kama ambavo famila na nyingine Misri,Edom,etc ikiwemo familia ya mzee yakobo (Israel) ikaja kuwa nchi unayodhani iko nyuma ya nadhalia zako.
2:Ayubu 4:1 Rafiki yake ayubu Elifadhi anasomwa kama mtemani ambao walikuwa wanakaa edomu maana yake alitoka ediomu akaenda UZ kumsalimia Ayubu so huwezi kutenganisha edom na uz.
3:SOma ayubu 1:15,17 UZ ilikuwa subject ya attack ya wakaldayo ambao wap wanajulikana.
Lamentations 4:21 reads: "Rejoice and be glad, O daughter of Edom, that dwellest in the land of
Uz"
hapo unaweza kuona kuwa land of uz ipo maeneo ua edomu . Ni kitu ambacho kilikuwepo na sio uzushi.
Umemzunguza MUHIBIRI wajua hicho kitabu kiliandikwa na nani? mbona humtaji mwandishi wake?
Hapa sielewi unataka nini, mwandishi wa kitabu au huamini kama kilikuwepo. hilo ni somo lingine, sijaelewa lengo lako ukimfahamu ndio utaamini au unataka nini.
Bibilia iliandikwa kwa dunia nzima, ndio maana sio waisrael wote wanaamini hiyo tunaoiita bibilia. ZIonism haiamini katika kufa na kufufuka kwa yesu. Sijui unaongelea waisraeli wapi.
Kuhusu kuwepo kwa miungu watatu hakuna uhusiano na kuwepo kwa utatu. natamua uwepo wa Osirus-Isis-Horus (utatu mtakatifu wa kipagani) na vingine vingi ambavyo vinarandana na vya shetani na hata hao wayahudi wenyewe walivipitia na kumuacha Mungu. Lakn ukikaa ukatulia utagundua hizo ni counterfit za shetani na hazina uhusiano na Mungu anavyoelezwa kwenye bibilia. Kuhusu ni Mmoja au mmoja katika watatu hiyo ni mada yake na hapa sio mahala pake kwa sas.
Swali la kizushi, km leo Mungu angelipuliza kipenda na kutangaza kuwa amefuta adhabu ya kifo binadamu hatutokufa tena na kila kitu binadamu anachokihitaji atapata bila masharti yeyote, hivi kuna atae enda nyumba ya ibada kuomba? na km ataenda ataenda kuomba nini?
Assumption hii ni invalid hadi ujue kwa nini tunakufa. Mahaka ya Mungu ni ya haki sio kama za huku duniani, Aliposema Utakufa hakika, ilikuwa hivyo. Hilo swali ungeliuliza kama adam asingekiuka makubaliano jee maisha yale yangeendelea duniani hadi sasa je tungekuwa tunaenda ibadani, Bado Mungu na adam na mke wake walikuwa na ukaribu sana kama baba na watoto wake au Mungu na Viumbe vyake. Kwa nini Ujiulizi hayo maswali kati ya malaika na Mungu wanaishije kwa nini wasiache kumuabudu kama wanaishi nae kila siku huko na hawana shida yoyote?
dini zilianzishwa na wanadamu kumshawishi Mungu awaondolee kifo, ndio sababu kila dini inastahili yake ya kumwendea Mungu, wengine hulia, wengine hupiga magoti, wengine husali uchi, lkn staili zote hizo zimeshindwa kumridhisha Mungu kuwaondelea wanadamu kifo, dini zilipoona kwamba wanadamu wanaendelea kufa wakaja na ushawishi mwingine kwa maana ya kwamba hata binadamu akifa ataenda mbinguni wataishi milele, simulizi ya maisha ya umilele huo zinatofautiana kati ya dini na dini wengine wanadai huko hakuna kula wala kunywa ni kusifu tu, wengine wanassema kule kuna vinywaji vitamu na kuhudumiwa na vimwana wazuri, je ukweli ni upi? nani aliyekwenda mbinguni na kurudi?
hapa mzee unaonyesha kwamba huelewi unachokizungumzia. niambie aliyeanzisha hivyo vutu na hayo malengo yawezekana kwenye msururu wa dini na madhehebu wakawepo wenye mtazamo huo. Lakini mimi naamini chochote kuhusu dini ibada kusali kimeelezwa kenye bibilia na ndio chakufuatwa bila kwenda kushoto wala kulia. na huko unapoongea kwenye kadamnasi mtandao ndipo unatakiwa kujengea hoja zako sio maneno ya kusikia au hisia. vinginevyo unakuwa hueleweki unataka au unapinga nini.