Sidhani kama kuna haja ya kumtusi Yeriko, ninachoona chanzo chake cha hii taarifa ndio kimempotosha..Ningependa kumhakikishia Yeriko na wengine kuwa pamoja na madhaifu tuliyonayo kwenye sehemu nyingine, jeshi liko liko vizuri mno..nathubutu kusema afrika mashariki na kati hamna anayesogelea..baadhi ya vinchi vilikuwa na kelele kidogo kipindi fulani baada ya kuuziwa na kupewa nyongeza ya silaha na Israel, wakaambiwa hakuna aliyenazo ukanda huu basi wakavimba vichwa..kama ni mfuatiliaji mzuri wa habari za propaganda zinazoandikwa kila kukicha zinadai ni Afrika kusini waliowasarambatisha M23 hawasemi Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kabisa, kama una ndugu yako aliyeko ama bado yuko na jeshi letu la kulinda amani DRC muulize kuhusu baadhi ya silaha zilizokutwa kwenye kambi ambazo M23 walikimbia..ni za kisasa sana ambazo waasi pamoja na kupora madini DRC hawawezi kuzipata kirahisi. Ukweli unabaki palepale, mziki wetu wanaujua hizo zote ni propaganda zao...