Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Hawa wazungu wakishaona silaha zimedoda wanaanza kuwatisha.

maajabu hawahawa Somalia ambao juzi wameomba msaada wa kijeshi TZ baada ya kuona Shughuli ya M23 kule Congo leo wametuzidi.?
 
kwenye jeshi umeenda mabali uko wapi usalama wa taifa? zaidi ua kashifa ya kutesa watu? siku hizi hata ukikaa mtaani lazima ujuwe huyu usalama wa taifa tofautibna miaka ya nyuma. huu ndo ukweli hata kama watanuna ili kulinda bibarua vyao. wakiingia kazini wanasahau kuwa wao ni watoto wa wakulima maskini kama mimi wanaanza kudhduru watuwakayi mama na baba yake hata chumvi hawana na mpaka anakuwa oficer ana suruali moja ya siku ya mahafali
 
MKUU YERIKO Nakukubali mno,kwa hili nipo kinyume.

  1. Kenya wanasumbuliwa na al shabaab,wakenya wanauwawa na vijikundi vya kigaidi vidogo dogo.wangekuwa na intelgensia imara na jeshi imara,wasingesumbuliwa.kenya hajawahi kufanya mission yoyote ya kijeshi kama vile ukombozi wa kusini mwa Afrika nyakati zile,wana well equiped army,wanakosa displined army,wanakosa experienced army.
  2. Kongo hawana jipya,kabla aliingiliwa ikulu karibu auawawe miaka miwaili iliyopita,anasumbuliwa na vikundi vya waasi,M23 TZ chini ya mwavuli wa UNO waliwapa kipigo cha paka mwizi,na biashara yao ikaisha.Kongo angekuwa na inelgensia imara na jeshi imara angekuwamaliza vikundi vya waasi mwenyewe.Jizi tu Mheshimiwa Rais Kikwete alifunga mafunzo ya maafisa wa Jeshi,wengi walikuwa toka Kongo.
  3. Uganda zaidi ya miongo miwili anasumbuliwa na Joseph Kony,kijikundi tu kidogo ambacho kikitokea tanzania wanagongwa toka kwenye pori walilojificha na kesho tunahesabu Mizoga tu.angekuwa na jeshi imara asingesumbuliwa namna hiyo.
NB.Opesesheni ya Kumuondoa Mohamedi Bakari Commoro ilisemekana ni impossible Tz iliomba logistic tu,ikapata ikaenda na yule bwana aliondoka alfajiri na majeshi yetu yakamvalisha dila na mtandio,wakamwambia aende kwa amani.

Ukombozi wa nchi za kusini Mchango wa Tanzania,Sudani na nyingine nyingi.Nasikitika Yeriko kuwa mimi ni shabiki mkubwa na mwanachama wa CHADEMA,inapokuja issue ya kitaifa hasa jeshi mimi naliheshimu sana,unaandika hapo kwa sababu nchi ina amani kwa sababu ya jeshi letu unalolitusi,bora ungezungumzia jeshi la polisi kuliko JWTZ jeshi letu lililotukuka.

EAST AFRICA EAGLE naomba uje umpe shule Yeriko Nyerere na mods wapeleke uzi huu Jamii forum Intelgensia ambako kuna watu hawingii huku jukwaa la siasa,ili ajibiwe kwa weledi wa hali ya juu!

Kwa kumalizia wewe na mimi labda hatujui sawasawa kuhusu jeshi letu.Nashauri Ngome wamchukue Yeriko nyererer wakamhoji Pale Ngome upanga kwa nini analitusi jeshi letu tukufu.
Nmesikitishwa sana na ndugu Yeriko nyerere.

Ukana Shilungo.
 
usalama wa taifa imebaki jina tu. wakipata kazi tu lazima ujuwe fulani ni usalama wa taifa tofauti na miaka iliyo pita hata mlima shamba kibarua anaweza kuwa usalama wa taifa haipo tena hiyo. siku hizi omekuwa cheo cha kutishia raia acheni mambo yenu lindeni nchi yetu na kama usalama wa taifa haikuwa wito wako rudi kwenu kalime shamba la mahindi maharage au machingwa. mbayavzaidi hizo nafasi wanapewa watu ambao hata uwezo wao wa kufikiri ni finyu
 
Ukana Shilungo

nakuunga mkono mkuu,hata mimi namkubali yeriko but kwa hili hapana takwimu zingine hutolewa kiusalama zaidi kwa manufaa ya watu Fulani au nchi fulani,nahisi tz hainunui silaha ndio maana imekuwa hivo.akili za kuambiwa changanya na za kwako
 
Last edited by a moderator:
Elimu ikishazorota tutarajie kilal kitu kuzorota...
 
Khaa!! Yericko unakurupuka sana. Labda uelewa ni tatizo kwako . hebu kasome tena kwa makini chanzo chako kisha uje kubadili heading hapa 😛eep:
 
Uongo huu, Jeshi letu haliwezi kuzidiwa na Jeshi la Nigeria.
 
Sidhani kama kuna haja ya kumtusi Yeriko, ninachoona chanzo chake cha hii taarifa ndio kimempotosha..Ningependa kumhakikishia Yeriko na wengine kuwa pamoja na madhaifu tuliyonayo kwenye sehemu nyingine, jeshi liko liko vizuri mno..nathubutu kusema afrika mashariki na kati hamna anayesogelea..baadhi ya vinchi vilikuwa na kelele kidogo kipindi fulani baada ya kuuziwa na kupewa nyongeza ya silaha na Israel, wakaambiwa hakuna aliyenazo ukanda huu basi wakavimba vichwa..kama ni mfuatiliaji mzuri wa habari za propaganda zinazoandikwa kila kukicha zinadai ni Afrika kusini waliowasarambatisha M23 hawasemi Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kabisa, kama una ndugu yako aliyeko ama bado yuko na jeshi letu la kulinda amani DRC muulize kuhusu baadhi ya silaha zilizokutwa kwenye kambi ambazo M23 walikimbia..ni za kisasa sana ambazo waasi pamoja na kupora madini DRC hawawezi kuzipata kirahisi. Ukweli unabaki palepale, mziki wetu wanaujua hizo zote ni propaganda zao...
 
Nigeria wanaoshindwa na Boko Haram nao wapo juu kijeshi!

tanzania imeshinda waasi gani? na kwambia usiombe tanzania watokeee waasi tutajuta hakuna jeshi humu siasa kila kona imejaa tutakufa mpaka basi
 
jeshi imara atakaae tu chokoza ataona cha mtema kuni by jk:A S wink:
 
Ukana Shilungo
Mkuu, ni bora umemweleza Yeriko kwa kuangalia uhalisia wa jeshi letu na majeshi ya nchi jirani. Tanzania ndio kinara wa kulinda amani barani Afrika. Tanzania tumewateketeza M23 tena kwa muda mfupi sana. Majeshi yetu yameweza kuhakikisha nchi inakuwa na amani na usalama muda wote. Mwache Yeriko adanganyike na fugures za mataifa ya magharibi
 
Last edited by a moderator:
tanzania imeshinda waasi gani? na kwambia usiombe tanzania watokeee waasi tutajuta hakuna jeshi humu siasa kila kona imejaa tutakufa mpaka basi
Tanzania haijashinda waasi wowote ndiyo maana ipo ya mwisho! Sasa Nigeria imeshinda waasi gani mpaka ishike namba ya juu?
 
Kama Nigeria ni ya 5, basi tusiwe na hofu kwa Tanzania kuwa ya mwisho. Hii listi haijapangwa na kocha, imepangwa na mashabiki.
Umeona eeeeh! Hata South Africa ambayo ndiyo ina jeshi imara barani Africa haijawa ya kwanza! Inashangaza sana hii
 
Back
Top Bottom