Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Ukana Shilungo,
Nasikitika kwa kutokuielewa mantiki ya thread hii,

Kwanza niwapi Yericko alipolitusi jeshi? kukopi link inayohusu nchi yetu ni tusi au kuelimisha.

Pili mifano yako kuwa Kenya inashindwa na al shabab tu siyo irrelevant utafiti huu ni wa uwezo wa nchi na nchi sio wa kupambana na vikundi vya kigaidi, unachanganya kazi ya jeshi la polisi na kazi ya jwtz.

Jeshi letu kukishinda kikundi cha M23 kuna factors nyingi mojawapo hatukuwa peke yetu pili hatukuenda na vifaa tulikuwa chini ya uangalizi wa un hata mishahara haikutoka kwetu.

Kwa hiyo kusema kuwa Nigeria wanashindwa na Boko haram basi hawana jeshi imara ni kujidanganya, mbona sisi tunahangaishwa na panya road wenye mapanga tu ina maana jeshi letu halina uwezo kiasi hicho.
 
Hii list imepangwa kibiashara tu mpanga listi anataka tukanunue silaha kwao
 
tanzania imeshinda waasi gani? na kwambia usiombe tanzania watokeee waasi tutajuta hakuna jeshi humu siasa kila kona imejaa tutakufa mpaka basi

kitendo cha kukosekana waasi tz ni ishara tosha kuwa tuna jeshi makini! Nakuhakikishia hakuna kenge yeyote atakaeleta kitovu chake tz na akabaki mzima!!

Hapa pigeni domo tu mfurahishe genge ila jwtz ni moto wa kuotea mbali. Km umewahi kutembelea nchi za afrika nenda ukawaulize wanalifahamu vp jeshi la tz! Watakuambia.

Kweli nimeamini nabii hakubaliki nyumbani kwao.
 
Hii list imepangwa kibiashara tu mpanga listi anataka tukanunue silaha kwao
Umeona eeeeeh! Nadhani Tanzania tumewekwa wa mwisho kutokana na kutonunua silaha kwenye mataifa ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani
 
Watu wanatumia nguvu nyingi sana kumpiga mleta mada, lakini wanasahau utafiti unapigwa kwa utafiti na kuangalia vingezo vilivyotumika katika utafiti husika.
kimsingi tunapaswa kujitasimini kwa kina sana
 
Ripoti ya hovyo sana hii, hakuna tofauti na ile iliyoonyesha eti Tanzania ni ya pili kwa umaskini duniani. Akili za kuambiwa tuchanganye na zetu,
 

Mkuu Ni Busara Sana Kulipa Jeshi Letu Heshima Yake! Lakini Ogopa Sana Nchi Ambayo Majeshi Yake Yako Kwenye Operation Za Kiusalama Muda Wote. Waliotoa Repoport Wana Sababu Zao Tusiwabeze. Hizi Changamoto Kwa Wakuu Wa Majeshi Ya Kwetu. Ila Si Siamini Kama Nchi Yetu Jeshi Lake Ni La Kisiasa Kuliko Hata Uganda.
 
Kwenye hili nimejikuta nacheka....

Seriously,

DRC inayoshindwa kulinda mipaka yake, imegeuzwa shamba la bibi na Rwanda eti iko juu yetu, tulioenda kuwatoa M23 and mind you, hawa jamaa wangepewa mwezi mmoja wangekuwa Kinshasa.

This is a joke
 
Nakubaliana na wewe Mkuu. Tanzania tunasambaratisha maadui kabla hawajaweka ngome. Somo tosha tumelipata kule Mtwara ambako vijana walijikusanya wakawa wanapata mafunzo ya kigaidi. Tuliwateketeza wote japo hatujawaua
 

Wale wa lumumba kama kawaida na uvivu wao wakusoma watakuja humu na vijembe oh! ilienda ikarudi.Siasa ikishaingizwa kwenye fani yoyote kila kitu kinajiangukia/kuporomoka kama mabua ya mahindi.

Kuna haja sana! Makamanda wa vikosi husika kuwa wadadisi wa mambo na kuchukua hatua mara moja!Naamini tusinge fikia kiwango hicho kama kweli maofisa husika na wale wanasiasa wanaopewa majukumu husika kutimiza majikumu yao sawa.

Tatizo la msingi limeanzia toka enzi ya Rtd General Mboma,pale JWTZ ilipogeuka kuwa mfanyabiashara ,badala ya kuwa Mlinzi wa Umma wa watanzania-chini ya Usimamizi na uangalizi wa Ikulu-Raisi mstaafu Ben Mkapa

NB.Bila kuwa shughulikia wahusika wote na Scandali hii-JWTZ itaendlea kuporomoka zaidi ya hapo ilipo.
Na kingine lakutupiwa jicho ni uteuzi wa Waziri wa Wizara husika na dhani sasa utamaduni huu wa kujiteulia watu wasio na uzoefu au hata mwanga wa nini Jeshi linahitaji au mwelekeo gani inatakuwa kuwa nao unafaa ubadilike.





Apr 15, 2008 - Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyoitwa Buhemba ilivunjwa. Askari walihamishwa kwa mikokoteni ya kukokotwa na ng'ombe ili kupisha ...
 


ndg yng km mambo huyajui ni heri ukae kimya, kuhusu kuwapiga m23 ktk misitu ya kongo ni makomando wa jwtz ndio waliowang'oa wale waasi.

Jiografia ya nchi ya kongo yenye milima na misitu mikubwa iliyashinda majeshi mengi ikiwemo afrika kusini. Ni juhudi ya makomandoo jwtz kutega mabomu ktk njia za waasi baada ya kuwasoma mbinu zao na jwtz waliwakurupusha m23 ktk moja ya maficho yao na kisha kujikuta wanaingia kwenye mtego wa jwtz na ndipo mabomu yalipoanza kulipuliwa na waasi kupoteza dira.

Haikuwa kazi nyepesi na majeshi yote ya ukombozi waliwapigia saluti jwtz kwa kazi nzuri ya kishujaa! Leo ww kiumbe mdogo unabeza.

Jwtz wanafanya kazi kwa amri ya amiri jeshi mkuu, kuhusu panya road jwtz hawakupokea amri yeyote inayowataka wakapambane na hao uimburu na wala jeshi la polisi hawakukiri kushindwa so jwtz hawakurupuki ktk kufanya kazi.

Ktk mambo ya msingi tuache ushabiki maandazi.
 
EnyiwanaTanganyika hii ripoti inaukweli hebu tujiulize ubora wa intelijensia yetu upo wapi, uimara wa jeshi unaanzia kwenye intelijensia.

Ukiwa na zero intelijensia jeshi halina cha maana.

Mpaka leo hatujuwi nani kapokea fedha za Escrow hapo Stanbic

Mpaka leo hatujuwi nani alilipuwa wahanga wa soweto Arusha

Mpka leo haijulikani nani aliuwa padri kule zanziba na kujeruhi wengine

Mpaka leo hatujuwi wezi waliohifadhi fedha Uswisi

Mpaka leo hatufaham nani na nani kwa ujumla wao walipakiza twiga na swala wakiwa hai ndani ya ndege ya jeshi kilimanjaro

Mpaka leo hatujuwi nani alipakia meno ya Tambo ndani ya meli ya katibu mkuu wa ccm

Mpaka leo hatujuwi wauza dawa za kulevya wale mabosi

Mpaka leo hatujaambiwa Gavana wa zamani alikufa yaani Balali na ilikuwaje

Mpka leo mambo ya Deep green, meremeta, kagoda, Epa namengineyo bado kitendawili

Mpaka leo IPTL, Dowans, Pap nk wanatuibia tu, na nimakampuni feki

Mpaka leo faru wamekwisha anayemaliza hatumjuwi

Sasa hilo jeshi litapataje kuwa lakisasa na bora kama intelijensia yao ipo chini kiasi hicho??????????????????????????????
 

Mbona povu Mkuu.
Yerick ametoa Mpaka na source,au unafikiri hii list kaandaa Yericko ?
 

Napenda nikusahihishe kidogo kuhusiana na maelezo niliyoweka red. Wakati wa vita vya Uganda, Division iliyopigana ikiwa ndani ya maji ya kiunoni iliongozwa na Brigedia (wakati huo) Mwita Marwa na ndiye alipewa hilo jina la Kamanda "KAMBALE"
 
Ukishaanza na kujiunga na Mafisadi na Mafia wa aina hii ya Victor Bout usitegemee masilahi ya Umma ndani ya Jeshi .
Mara zote malengo ya Jeshi yanapotea kabisa na badala yake Jeshi linageuka kuwa taasisi ya Makamanda wachache ambao wanakuwa Mabilionea ,na kuwa ingiza wanasiasa ndani yake au Kinyume chake,kwa maana ya Wanasiasa kuwa ingiza Makamanda kwenye madili kama hayo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…