Are you serious unaijua Nigeria au unaisikia, jeshi la Nigeria ni la kulinganisha na la Afrika Kusini.
Umesema kweli mkuu, hata mie sijafurahishwa na porojo hizo. JWTZ ingekuwa kama alivyoielezea Yericko Nyerere, basi Tz ingekuwa imevurugika kuliko hata DRC na Somalia maana hata sie tuna kila kitu cha kuwavutia mabepari kutuvuruga. Na pia tusingekuwepo DRC kuneutralize vikundi ambavyo vimesumbua sana huko DRC.MKUU YERIKO Nakukubali mno,kwa hili nipo kinyume.
NB.Opesesheni ya Kumuondoa Mohamedi Bakari Commoro ilisemekana ni impossible Tz iliomba logistic tu,ikapata ikaenda na yule bwana aliondoka alfajiri na majeshi yetu yakamvalisha dila na mtandio,wakamwambia aende kwa amani.
- Kenya wanasumbuliwa na al shabaab,wakenya wanauwawa na vijikundi vya kigaidi vidogo dogo.wangekuwa na intelgensia imara na jeshi imara,wasingesumbuliwa.kenya hajawahi kufanya mission yoyote ya kijeshi kama vile ukombozi wa kusini mwa Afrika nyakati zile,wana well equiped army,wanakosa displined army,wanakosa experienced army.
- Kongo hawana jipya,kabla aliingiliwa ikulu karibu auawawe miaka miwaili iliyopita,anasumbuliwa na vikundi vya waasi,M23 TZ chini ya mwavuli wa UNO waliwapa kipigo cha paka mwizi,na biashara yao ikaisha.Kongo angekuwa na inelgensia imara na jeshi imara angekuwamaliza vikundi vya waasi mwenyewe.Jizi tu Mheshimiwa Rais Kikwete alifunga mafunzo ya maafisa wa Jeshi,wengi walikuwa toka Kongo.
- Uganda zaidi ya miongo miwili anasumbuliwa na Joseph Kony,kijikundi tu kidogo ambacho kikitokea tanzania wanagongwa toka kwenye pori walilojificha na kesho tunahesabu Mizoga tu.angekuwa na jeshi imara asingesumbuliwa namna hiyo.
Ukombozi wa nchi za kusini Mchango wa Tanzania,Sudani na nyingine nyingi.Nasikitika Yeriko kuwa mimi ni shabiki mkubwa na mwanachama wa CHADEMA,inapokuja issue ya kitaifa hasa jeshi mimi naliheshimu sana,unaandika hapo kwa sababu nchi ina amani kwa sababu ya jeshi letu unalolitusi,bora ungezungumzia jeshi la polisi kuliko JWTZ jeshi letu lililotukuka.
EAST AFRICA EAGLE naomba uje umpe shule Yeriko Nyerere na mods wapeleke uzi huu Jamii forum Intelgensia ambako kuna watu hawingii huku jukwaa la siasa,ili ajibiwe kwa weledi wa hali ya juu!
Kwa kumalizia wewe na mimi labda hatujui sawasawa kuhusu jeshi letu.Nashauri Ngome wamchukue Yeriko nyererer wakamhoji Pale Ngome upanga kwa nini analitusi jeshi letu tukufu.
Nmesikitishwa sana na ndugu Yeriko nyerere.
Ukana Shilungo.
Nivigumu siasa kuongoa mambo ya kitaalamu, hili hata wahenga walilinena, wakati wenzetu wakijenga mataifa yao kijeshi na kiulinzi yakawa imara na ya kisiasa zaidi, sisi tunaendelea kuonyeshana namna mwanajeshi anavyopasua tofari kwa kichwa, yani utafiki ni jeshi la enzi za akina Mkwawa.
Wakati wa miaka ya sitini mpaka miaka ya tisini, Tamzania ilikuwa ya kwanza barani Afrika kwakuwa na idara ya ujasusi imara ikifuatiwa na Zimbabwe, lakini leo Zimbabwe ni ya kwanza ikifuatiwa na Misri na Tanzania ni ya Tatu.
Hali kadhlika baada ya vita vya Uganda, Tanzania ilipanda kwenye viwango vya ubora na uimara wa kijeshi hasa sifa zikienda kwa kikosi cha ardhini kile kilichopambana na majeshi ya Nduli katika uwanda wenye maji ya kiuno kwa mda wa siku sita mfululizo mpaka kikashinda kikiongozwa na Brigedia Kiwelu ambae baada ya mapambano yale alibatizwa na kuitwa KAMBARE, jina hilo lilifuati uwezo wake wa kuzama mda mrefu majini huku akiji mapigo vikosi vya Nduli vilivyokuwa vimejichimbia mlimani katika mto Kagera,
Sifa hizi zilieneoa duniani kote na tafiti nyingi za mashirika ya kijasusi zikafanywa nakusema Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika kwakuwa na Jeshi imara la miguu,
Hivi sasa siasa zimeharibu sifa hizo na utafiti wa wakala wa usalam wa taifa wa Amerika umeweka takwimu hizi hapa mpya ambao Tanzania ni ya mwisho kati ya nchi 22 zilizofanyiwa utafiti.
ORODHA KAMILI.
1 Egypt
PwrIndx: 0.6122
2 Algeria
PwrIndx: 1.1698
3 Ethiopia
PwrIndx: 1.3229
4 South Africa
PwrIndx: 1.3467
5 Nigeria
PwrIndx: 1.5261
6 Kenya
PwrIndx: 1.7689
7 Morocco
PwrIndx: 1.8499
8 Tunisia
PwrIndx: 1.8635
9 Angola
PwrIndx: 2.2599
10 Libya
PwrIndx: 2.3353
11 Sudan
PwrIndx: 2.3465
12 Democratic Republic of the Congo
PwrIndx: 2.6642
13 Uganda
PwrIndx: 2.6895
14 South Sudan
PwrIndx: 2.7689
15 Ghana
PwrIndx: 2.9726
16 Zimbabwe
PwrIndx: 3.0955
17 Cameroon
PwrIndx: 3.3009
18 Zambia
PwrIndx: 3.5013
19 Somalia
PwrIndx: 3.5462
20 Mozambique
PwrIndx: 4.1026
21 Madagascar
PwrIndx: 4.2547
22 Tanzania
PwrIndx: 4.3423
Chanzo: Countries Ranked by Military Strength (2014)
Napenda nikusahihishe kidogo kuhusiana na maelezo niliyoweka red. Wakati wa vita vya Uganda, Division iliyopigana ikiwa ndani ya maji ya kiunoni iliongozwa na Brigedia (wakati huo) Mwita Marwa na ndiye alipewa hilo jina la Kamanda "KAMBALE"
Nigeria wanaoshindwa na Boko Haram nao wapo juu kijeshi!
kitendo cha kukosekana waasi tz ni ishara tosha kuwa tuna jeshi makini! Nakuhakikishia hakuna kenge yeyote atakaeleta kitovu chake tz na akabaki mzima!!
Hapa pigeni domo tu mfurahishe genge ila jwtz ni moto wa kuotea mbali. Km umewahi kutembelea nchi za afrika nenda ukawaulize wanalifahamu vp jeshi la tz! Watakuambia.
Kweli nimeamini nabii hakubaliki nyumbani kwao.
Sangarara jaribu kutofautisha kati ya jeshi kupambana na kikundi cha uasi na jeshi kupambana na jeshi la nchi nyingine.Jumamosi Bokoharam wamelitimua hilo Jeshi kwenye mji wa Baga, ndio ulikuwa mji wa mwisho katika yote inayotenganisha Nigeria na nchi za Chad,Cameroon na Algeria.
Wanajeshi waliokuwa kwenye mji huo wamepigwa na kukimbia.
Sasa muda wowote Boko haram wataanzisha mashambulizi tena dhidi ya mji mkuu wa Jimbo la Josi, Maiduguri
Kuna nini hapo?
Hapa nafikiri wamezungumzia majeshi ya Ulinzi wa mipaka na siyo wanausalama wa raia na mali zao!Na wale wanaoshindwa na panya road?.
Ngongo kumbuka kuna wanajeshi wa Tanzania walikuwa Iraki kuyasaidia majeshi ya Marekani sijui kama tulikuwa tunawazidi wamarekani kijeshi.Sikuballiani na hii ripoti uchwara.Yaani DRC tumewasaidia kuanzia kufundisha askari wao hadi kuwafurusha M23.Kenya jeshi lake ni hovyo kabisa tazama tangu wamekwenda Somalia wamefanya nini,Uganda jeshi lao tumewafunza,Sudan nchi imegawanyika baada ya vita vya muda mrefu sana.Somalia wana jeshi zuri kuliko Tanzania huu ni uongo wa mchana kweupe.
Sangarara jaribu kutofautisha kati ya jeshi kupambana na kikundi cha uasi na jeshi kupambana na jeshi la nchi nyingine.
Ngongo kumbuka kuna wanajeshi wa Tanzania walikuwa Iraki kuyasaidia majeshi ya Marekani sijui kama tulikuwa tunawazidi wamarekani kijeshi.
Kwenda kusaidia nchi kijeshi sio lazima uwe unaizidi kijeshi.