Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Are you serious unaijua Nigeria au unaisikia, jeshi la Nigeria ni la kulinganisha na la Afrika Kusini.

Jumamosi Bokoharam wamelitimua hilo Jeshi kwenye mji wa Baga, ndio ulikuwa mji wa mwisho katika yote inayotenganisha Nigeria na nchi za Chad,Cameroon na Algeria.

Wanajeshi waliokuwa kwenye mji huo wamepigwa na kukimbia.

Sasa muda wowote Boko haram wataanzisha mashambulizi tena dhidi ya mji mkuu wa Jimbo la Josi, Maiduguri

Kuna nini hapo?
 
ingekuwa kwenye rushwa tanzania ingeshika nafasi ya kwanza lakini kwenye usalama tupo ziro kabisa
 
MKUU YERIKO Nakukubali mno,kwa hili nipo kinyume.

  1. Kenya wanasumbuliwa na al shabaab,wakenya wanauwawa na vijikundi vya kigaidi vidogo dogo.wangekuwa na intelgensia imara na jeshi imara,wasingesumbuliwa.kenya hajawahi kufanya mission yoyote ya kijeshi kama vile ukombozi wa kusini mwa Afrika nyakati zile,wana well equiped army,wanakosa displined army,wanakosa experienced army.
  2. Kongo hawana jipya,kabla aliingiliwa ikulu karibu auawawe miaka miwaili iliyopita,anasumbuliwa na vikundi vya waasi,M23 TZ chini ya mwavuli wa UNO waliwapa kipigo cha paka mwizi,na biashara yao ikaisha.Kongo angekuwa na inelgensia imara na jeshi imara angekuwamaliza vikundi vya waasi mwenyewe.Jizi tu Mheshimiwa Rais Kikwete alifunga mafunzo ya maafisa wa Jeshi,wengi walikuwa toka Kongo.
  3. Uganda zaidi ya miongo miwili anasumbuliwa na Joseph Kony,kijikundi tu kidogo ambacho kikitokea tanzania wanagongwa toka kwenye pori walilojificha na kesho tunahesabu Mizoga tu.angekuwa na jeshi imara asingesumbuliwa namna hiyo.
NB.Opesesheni ya Kumuondoa Mohamedi Bakari Commoro ilisemekana ni impossible Tz iliomba logistic tu,ikapata ikaenda na yule bwana aliondoka alfajiri na majeshi yetu yakamvalisha dila na mtandio,wakamwambia aende kwa amani.

Ukombozi wa nchi za kusini Mchango wa Tanzania,Sudani na nyingine nyingi.Nasikitika Yeriko kuwa mimi ni shabiki mkubwa na mwanachama wa CHADEMA,inapokuja issue ya kitaifa hasa jeshi mimi naliheshimu sana,unaandika hapo kwa sababu nchi ina amani kwa sababu ya jeshi letu unalolitusi,bora ungezungumzia jeshi la polisi kuliko JWTZ jeshi letu lililotukuka.

EAST AFRICA EAGLE naomba uje umpe shule Yeriko Nyerere na mods wapeleke uzi huu Jamii forum Intelgensia ambako kuna watu hawingii huku jukwaa la siasa,ili ajibiwe kwa weledi wa hali ya juu!

Kwa kumalizia wewe na mimi labda hatujui sawasawa kuhusu jeshi letu.Nashauri Ngome wamchukue Yeriko nyererer wakamhoji Pale Ngome upanga kwa nini analitusi jeshi letu tukufu.
Nmesikitishwa sana na ndugu Yeriko nyerere.

Ukana Shilungo.
Umesema kweli mkuu, hata mie sijafurahishwa na porojo hizo. JWTZ ingekuwa kama alivyoielezea Yericko Nyerere, basi Tz ingekuwa imevurugika kuliko hata DRC na Somalia maana hata sie tuna kila kitu cha kuwavutia mabepari kutuvuruga. Na pia tusingekuwepo DRC kuneutralize vikundi ambavyo vimesumbua sana huko DRC.
 
kweli wewe ni zero. hivi unaamini hata somalia wana jeshi imara kuliko letu? nchi ambayo iko kwenye mapambano ya koo tangia 1994 alipofariki Said Barre? utakuwa taahira wewe sio hivi hivi. somalia ambao wameshindwa hata kupambana na Al-Shabbab? au na hao weme-includiwa? kuwa mbayuwayu, usiamini tu kila uambiacho.

Nivigumu siasa kuongoa mambo ya kitaalamu, hili hata wahenga walilinena, wakati wenzetu wakijenga mataifa yao kijeshi na kiulinzi yakawa imara na ya kisiasa zaidi, sisi tunaendelea kuonyeshana namna mwanajeshi anavyopasua tofari kwa kichwa, yani utafiki ni jeshi la enzi za akina Mkwawa.

Wakati wa miaka ya sitini mpaka miaka ya tisini, Tamzania ilikuwa ya kwanza barani Afrika kwakuwa na idara ya ujasusi imara ikifuatiwa na Zimbabwe, lakini leo Zimbabwe ni ya kwanza ikifuatiwa na Misri na Tanzania ni ya Tatu.

Hali kadhlika baada ya vita vya Uganda, Tanzania ilipanda kwenye viwango vya ubora na uimara wa kijeshi hasa sifa zikienda kwa kikosi cha ardhini kile kilichopambana na majeshi ya Nduli katika uwanda wenye maji ya kiuno kwa mda wa siku sita mfululizo mpaka kikashinda kikiongozwa na Brigedia Kiwelu ambae baada ya mapambano yale alibatizwa na kuitwa KAMBARE, jina hilo lilifuati uwezo wake wa kuzama mda mrefu majini huku akiji mapigo vikosi vya Nduli vilivyokuwa vimejichimbia mlimani katika mto Kagera,

Sifa hizi zilieneoa duniani kote na tafiti nyingi za mashirika ya kijasusi zikafanywa nakusema Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika kwakuwa na Jeshi imara la miguu,

Hivi sasa siasa zimeharibu sifa hizo na utafiti wa wakala wa usalam wa taifa wa Amerika umeweka takwimu hizi hapa mpya ambao Tanzania ni ya mwisho kati ya nchi 22 zilizofanyiwa utafiti.

ORODHA KAMILI.

1 Egypt

PwrIndx: 0.6122

2 Algeria

PwrIndx: 1.1698

3 Ethiopia

PwrIndx: 1.3229

4 South Africa

PwrIndx: 1.3467

5 Nigeria

PwrIndx: 1.5261

6 Kenya

PwrIndx: 1.7689

7 Morocco

PwrIndx: 1.8499

8 Tunisia

PwrIndx: 1.8635

9 Angola

PwrIndx: 2.2599

10 Libya

PwrIndx: 2.3353

11 Sudan

PwrIndx: 2.3465

12 Democratic Republic of the Congo

PwrIndx: 2.6642

13 Uganda

PwrIndx: 2.6895

14 South Sudan

PwrIndx: 2.7689

15 Ghana

PwrIndx: 2.9726

16 Zimbabwe

PwrIndx: 3.0955

17 Cameroon

PwrIndx: 3.3009

18 Zambia

PwrIndx: 3.5013

19 Somalia

PwrIndx: 3.5462

20 Mozambique

PwrIndx: 4.1026

21 Madagascar

PwrIndx: 4.2547

22 Tanzania

PwrIndx: 4.3423



Chanzo: Countries Ranked by Military Strength (2014)
 
Napenda nikusahihishe kidogo kuhusiana na maelezo niliyoweka red. Wakati wa vita vya Uganda, Division iliyopigana ikiwa ndani ya maji ya kiunoni iliongozwa na Brigedia (wakati huo) Mwita Marwa na ndiye alipewa hilo jina la Kamanda "KAMBALE"

Oooho kamanda nakushukuru sana kwakunisahihisha, nilisahau kidogo!

Thanks sana mkuu!
 
kitendo cha kukosekana waasi tz ni ishara tosha kuwa tuna jeshi makini! Nakuhakikishia hakuna kenge yeyote atakaeleta kitovu chake tz na akabaki mzima!!

Hapa pigeni domo tu mfurahishe genge ila jwtz ni moto wa kuotea mbali. Km umewahi kutembelea nchi za afrika nenda ukawaulize wanalifahamu vp jeshi la tz! Watakuambia.

Kweli nimeamini nabii hakubaliki nyumbani kwao.

ha ha ha ha! nchi ambayo jiji lake kuu analokaa rais linatekwa na watoto wa miaka 20 eti panya road inajigamba kuwa na jeshi imara!!!
 
Sisi tunaongoza kulew na kupiga mbupuu(kinyume chake)
 
Jumamosi Bokoharam wamelitimua hilo Jeshi kwenye mji wa Baga, ndio ulikuwa mji wa mwisho katika yote inayotenganisha Nigeria na nchi za Chad,Cameroon na Algeria.

Wanajeshi waliokuwa kwenye mji huo wamepigwa na kukimbia.

Sasa muda wowote Boko haram wataanzisha mashambulizi tena dhidi ya mji mkuu wa Jimbo la Josi, Maiduguri

Kuna nini hapo?
Sangarara jaribu kutofautisha kati ya jeshi kupambana na kikundi cha uasi na jeshi kupambana na jeshi la nchi nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Sikuballiani na hii ripoti uchwara.Yaani DRC tumewasaidia kuanzia kufundisha askari wao hadi kuwafurusha M23.Kenya jeshi lake ni hovyo kabisa tazama tangu wamekwenda Somalia wamefanya nini,Uganda jeshi lao tumewafunza,Sudan nchi imegawanyika baada ya vita vya muda mrefu sana.Somalia wana jeshi zuri kuliko Tanzania huu ni uongo wa mchana kweupe.
Ngongo kumbuka kuna wanajeshi wa Tanzania walikuwa Iraki kuyasaidia majeshi ya Marekani sijui kama tulikuwa tunawazidi wamarekani kijeshi.

Kwenda kusaidia nchi kijeshi sio lazima uwe unaizidi kijeshi.
 
hata vita ya uganda hatukuwa na silaha za ajabu ni smg na sar anaetaka aje.
 
Law 3:conceal your intention
LAW 21😛lay a sucker to catch a sucker. Seem dumber than your marker.
 
Sangarara jaribu kutofautisha kati ya jeshi kupambana na kikundi cha uasi na jeshi kupambana na jeshi la nchi nyingine.

Kwani we unalipimaje Jeshi la Tanzania na la Nigeria?


Mpaka Mataifa Yapigane? Haya basi, sisi tuliposhambuliwa na Amin tulimuondoa kwa uwezo mkubwa.

Nigeria Kampiga nani?
 
Ngongo kumbuka kuna wanajeshi wa Tanzania walikuwa Iraki kuyasaidia majeshi ya Marekani sijui kama tulikuwa tunawazidi wamarekani kijeshi.

Kwenda kusaidia nchi kijeshi sio lazima uwe unaizidi kijeshi.

Tanzania haikwenda kule visiwani kusaidia, ilienda kumuondoa Rais wa nchi Kijeshi, maana yake iliwaoverpower wanajeshi wa nchi hiyo Kijeshi.

M23 unataka kusema walikuwa hawajalishinda jeshi la DRC?
 
Huu ni Uongo kabisa..
South Sudan,
Somalia
Nigeria
Majeshi yao yakiboya sana..
 
inasikitisha sana , yaani umahiri wetu upo kwenye kuvunja matofali ya cement chapa NYATI tu !
 
Back
Top Bottom