Tusimhukumu Yeriko kwa kuleta ripoti ya utafiti. Hivyo ndivyo ripoti ya utafiti inavyosema.
Jambo la msingi ni kuzidi kujiuliza vigezo vilivyotumika, na uzito wa kila kigezo. Tukishavijua vigezo, tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kukubaliana na ripoti au kukataa kufuatana na vigezo vilivyotumika.
Tusisahau kuwa karibu zana zote za kisasa tulizo nazo tumepewa na hawa hawa waliotufanyia ranking. Yabidi kujiuliza pia, tulikuwa tunasema nini wakati wa kuomba hizi zana za kisasa. Kama unaenda kwa tajiri unasema naomba msaada maana nyumbani kwangu hakuna hata chumvi, watoto wangu hawajawahi kuonja chai kwa mwezi mzima, ndani ya familia yangu hakuna mwenye kiatu hata mmoja, n.k; kisha ukasaidiwa viatu, chumvi, mchele, mafuta na nyama; halafu baada ya miezi 6, tajiri yule yule aliyekufadhili anafanya ranking ya umaskini, unadhani wewe uliyekuwa unalala miguuni pake ukiomba chumvi utakuwa wangapi? Natathamini sana nidhamu, uzalendo, na mafunzo ya wanajeshi wetu. Sina uhakika na mengine ambayo nayo ni muhimu pia kwa ubora wa jeshi.
Kushinda vita siyo kigezo pekee kinachotumika katika ubora wa jeshi maana vita siyo kama mchezo wa mpira ambapo timu hupangwa katika madaraja, na wakati wote huwa kuna mashindano. Nigeria kushambuliwa na Boko Haram, Kenya kushambuliwa na Alshabab siyo uthibitisho pekee wa ubovu wa majeshi yao.
Je sisi hapa tuna uhakika tungekuwa tunapigana na Boko Haram au Alshabab matokeo yangekuwaje? Mkumbuke kuwa vita vya ugaidi ni vigumu sana kuvishinda maana adui huwa hawi wazi.
Itoshe tu kusema, tunalishukuru sana jeshi letu kwa nidhamu, weledi, uzalendo na nidhamu iliyotukuka lakini kwa wakuu wa nchi na na wakuu wa jeshi letu ni muhimu kuitazama kwa umakini ripoti hii kujua wapi ni sahihi na wapi haipo sahihi. Yaliyo sahihi ni lazima yafanyiwe kazi. Mfahamu pia, unalivyolihudumia jeshi lako ikiwa ni pamoja na maisha binafsi ya askari wako, vifaa vya kivita na vya matumizi ya kawaida pia huelezea ubora wa jeshi. Ni kweli tunautambua uzalendo wa jeshi letu lakini kwa upande wa pili, tunalihudumia vipi?
nakuunga mkono mkuu,hata mimi namkubali yeriko but kwa hili hapana takwimu zingine hutolewa kiusalama zaidi kwa manufaa ya watu Fulani au nchi fulani,nahisi tz hainunui silaha ndio maana imekuwa hivo.akili za kuambiwa changanya na za kwako