Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Tanzania haijashinda waasi wowote ndiyo maana ipo ya mwisho! Sasa Nigeria imeshinda waasi waasi gani mpaka ishike namba ya juu?
Swali la msingi sana hili. Wanahangaika na Boko Haramu kiasi cha kuteka wale mabinti 200 mpaka sasa intelijensia yao haijui wako wapi.
 
Mkuu mnapokuwa na mtu kama Yeriko kama mmojawa raia wenu na akaendekeza siasa mpaka kwenye masuala yanayohitaji kuonesha uzalendo hakuna namna zaidi ya KUMTUKANA tu.huyu ni mpuuzi
Kule Rwanda huwa wanawatumbukiza mtoni watu kama Yeriko
 
Mleta uzi mwehu somalia nchi ya kuwa mbele kuliko sisi?Uganda hata kenya wanashindwa na al shababu hao wa congo m23 inawatoa jasho nigeria karibuni boko haramu wanachukua nchi zambia wanani?zimbabwe wanani?

Ukisoma mpaka mwisho utaona kuna chanzo cha takwimu hizo
 
Hata kwa UJINGA tunaongoza sana... Kidumu Chama cha Masengejuu ...
 
YERIKO leo unalo, wewe unafikiri kila unachopost humu utaungwa mkono na siasa zako uchwara za vidole viwili kama PANYAROAD. Usiwatanie kabisa watanzania na jeshi lao linalopata heshima kitaifa na kimataifa kila uchwao.
 
Sikuballiani na hii ripoti uchwara.Yaani DRC tumewasaidia kuanzia kufundisha askari wao hadi kuwafurusha M23.Kenya jeshi lake ni hovyo kabisa tazama tangu wamekwenda Somalia wamefanya nini,Uganda jeshi lao tumewafunza,Sudan nchi imegawanyika baada ya vita vya muda mrefu sana.Somalia wana jeshi zuri kuliko Tanzania huu ni uongo wa mchana kweupe.
 
YERIKO leo unalo, wewe unafikiri kila unachopost humu utaungwa mkono na siasa zako uchwara za vidole viwili kama PANYAROAD. Usiwatanie kabisa watanzania na jeshi lao linalopata heshima kitaifa na kimataifa kila uchwao.

Haha duuuh
 
Yericko! Unataka tuwe bora katika kila jambo? Viongozi wetu wamechagua kuwa kipau mbele ili kuifanya nchi ing'ae kimataifa ni kuwekeza nguvu zatu katika UFISADI! Hutaki kukubali wakati tuliwachagua ili watusaidie kupanga mipango yetu ya maendeleo!
 
Tusimhukumu Yeriko kwa kuleta ripoti ya utafiti. Hivyo ndivyo ripoti ya utafiti inavyosema.

Jambo la msingi ni kuzidi kujiuliza vigezo vilivyotumika, na uzito wa kila kigezo. Tukishavijua vigezo, tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kukubaliana na ripoti au kukataa kufuatana na vigezo vilivyotumika.

Tusisahau kuwa karibu zana zote za kisasa tulizo nazo tumepewa na hawa hawa waliotufanyia ranking. Yabidi kujiuliza pia, tulikuwa tunasema nini wakati wa kuomba hizi zana za kisasa. Kama unaenda kwa tajiri unasema naomba msaada maana nyumbani kwangu hakuna hata chumvi, watoto wangu hawajawahi kuonja chai kwa mwezi mzima, ndani ya familia yangu hakuna mwenye kiatu hata mmoja, n.k; kisha ukasaidiwa viatu, chumvi, mchele, mafuta na nyama; halafu baada ya miezi 6, tajiri yule yule aliyekufadhili anafanya ranking ya umaskini, unadhani wewe uliyekuwa unalala miguuni pake ukiomba chumvi utakuwa wangapi? Natathamini sana nidhamu, uzalendo, na mafunzo ya wanajeshi wetu. Sina uhakika na mengine ambayo nayo ni muhimu pia kwa ubora wa jeshi.

Kushinda vita siyo kigezo pekee kinachotumika katika ubora wa jeshi maana vita siyo kama mchezo wa mpira ambapo timu hupangwa katika madaraja, na wakati wote huwa kuna mashindano. Nigeria kushambuliwa na Boko Haram, Kenya kushambuliwa na Alshabab siyo uthibitisho pekee wa ubovu wa majeshi yao.

Je sisi hapa tuna uhakika tungekuwa tunapigana na Boko Haram au Alshabab matokeo yangekuwaje? Mkumbuke kuwa vita vya ugaidi ni vigumu sana kuvishinda maana adui huwa hawi wazi.

Itoshe tu kusema, tunalishukuru sana jeshi letu kwa nidhamu, weledi, uzalendo na nidhamu iliyotukuka lakini kwa wakuu wa nchi na na wakuu wa jeshi letu ni muhimu kuitazama kwa umakini ripoti hii kujua wapi ni sahihi na wapi haipo sahihi. Yaliyo sahihi ni lazima yafanyiwe kazi. Mfahamu pia, unalivyolihudumia jeshi lako ikiwa ni pamoja na maisha binafsi ya askari wako, vifaa vya kivita na vya matumizi ya kawaida pia huelezea ubora wa jeshi. Ni kweli tunautambua uzalendo wa jeshi letu lakini kwa upande wa pili, tunalihudumia vipi?

nakuunga mkono mkuu,hata mimi namkubali yeriko but kwa hili hapana takwimu zingine hutolewa kiusalama zaidi kwa manufaa ya watu Fulani au nchi fulani,nahisi tz hainunui silaha ndio maana imekuwa hivo.akili za kuambiwa changanya na za kwako
 
Unakataa siasa kuongoza kila kitu wakati hii orodha imesimama kisiasa?..
Hao waliowekwa juu yetu waguse waone cha moto
 
Tanzania ina watu wanauelewa mdogo sana yeriko yeye kaleta utafiti uliofanywa na wewe leta was kwako. Miaka 5 ijayo Tanzania itakuwa na wajinga wengi sana, mungu wasaidie
 
Ukana Shilungo
Mkuu, ni bora umemweleza Yeriko kwa kuangalia uhalisia wa jeshi letu na majeshi ya nchi jirani. Tanzania ndio kinara wa kulinda amani barani Afrika. Tanzania tumewateketeza M23 tena kwa muda mfupi sana. Majeshi yetu yameweza kuhakikisha nchi inakuwa na amani na usalama muda wote. Mwache Yeriko adanganyike na fugures za mataifa ya magharibi

Hivi somalia huwa ipo bara gani?.
Mnakimbilia Congo kisa kuna madini?
Ondoen seleka na anti Baraka.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom