Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Facts: 16 most powerful militaries in Africa

Tanzania ina watu wanauelewa mdogo sana yeriko yeye kaleta utafiti uliofanywa na wewe leta was kwako. Miaka 5 ijayo Tanzania itakuwa na wajinga wengi sana, mungu wasaidie
Umeona ee..badala ya watu kujadili na kuainisha mapungufu ya ripoti wao wanadhani Yericko ndiye aliyeiandaa ripoti, Mungu tusaidie angalau utupandishie IQ.
 
tuwekee ukweli mkuu , tumzodoe mleta uzi .

Mkuu hapana aisee, sitaki kuamini kabisa..
Jeshi la Somalia, na South Sudan kama yako imara kwa kiwango cha kuzidi hili la Mwamunyange pamoja ya kuwa ni la Kiboya lakini bado sijalishusha chini ya hizo nchi hapo jju
 
Hao waliofanya huu utafiti wanafikiri kwa kusema hvyo ndo Tanzania itatetemeka kwenda kununua silaha zao.

Silaha zimewadodea ndo wanakuja utafiti wao uchwara. Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuingia gharama kununua silaha zisizo na kazi wakati technologia inakuwa kila siku na silaha za kisasa zinavumbuliwa kila uchao. Ni kupoteza hela tu.

Wakitaka kufahamu waite mechi ya kirafiki.
 
Kwani we unalipimaje Jeshi la Tanzania na la Nigeria?


Mpaka Mataifa Yapigane? Haya basi, sisi tuliposhambuliwa na Amin tulimuondoa kwa uwezo mkubwa

Nigeria Kampiga nani?
Mkuu kujua uwezo wa nchi kijeshi sio lazima uione inapigana, SA hajapigana lakini hatuwezi kuizidi kijeshi.
 
Mkuu kujua uwezo wa nchi kijeshi sio lazima uione inapigana, SA hajapigana lakini hatuwezi kuizidi kijeshi.

Mi nasema Jeshi letu ni bora kuliko la Nigeria, kwa nini unanivutia kwa hao wazungu wa south?
 
Kama wanazani jeshi letu ni legelege wajalibu kuvamia halafu waone hizo takwim sio sahihi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nivigumu siasa kuongoa mambo ya kitaalamu, hili hata wahenga walilinena, wakati wenzetu wakijenga mataifa yao kijeshi na kiulinzi yakawa imara na ya kisiasa zaidi, sisi tunaendelea kuonyeshana namna mwanajeshi anavyopasua tofari kwa kichwa, yani utafiki ni jeshi la enzi za akina Mkwawa.

Wakati wa miaka ya sitini mpaka miaka ya tisini, Tamzania ilikuwa ya kwanza barani Afrika kwakuwa na idara ya ujasusi imara ikifuatiwa na Zimbabwe, lakini leo Zimbabwe ni ya kwanza ikifuatiwa na Misri na Tanzania ni ya Tatu.

Hali kadhlika baada ya vita vya Uganda, Tanzania ilipanda kwenye viwango vya ubora na uimara wa kijeshi hasa sifa zikienda kwa kikosi cha ardhini kile kilichopambana na majeshi ya Nduli katika uwanda wenye maji ya kiuno kwa mda wa siku sita mfululizo mpaka kikashinda kikiongozwa na Brigedia Mwita Marwa ambae baada ya mapambano yale alibatizwa na kuitwa KAMBARE, jina hilo lilifuati uwezo wake wa kuzama mda mrefu majini huku akiji mapigo vikosi vya Nduli vilivyokuwa vimejichimbia mlimani katika mto Kagera,

Sifa hizi zilieneoa duniani kote na tafiti nyingi za mashirika ya kijasusi zikafanywa nakusema Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika kwakuwa na Jeshi imara la miguu,

Hivi sasa siasa zimeharibu sifa hizo na utafiti wa wakala wa usalam wa taifa wa Amerika umeweka takwimu hizi hapa mpya ambao Tanzania ni ya mwisho kati ya nchi 22 zilizofanyiwa utafiti.

ORODHA KAMILI.

1 Egypt

PwrIndx: 0.6122

2 Algeria

PwrIndx: 1.1698

3 Ethiopia

PwrIndx: 1.3229

4 South Africa

PwrIndx: 1.3467

5 Nigeria

PwrIndx: 1.5261

6 Kenya

PwrIndx: 1.7689

7 Morocco

PwrIndx: 1.8499

8 Tunisia

PwrIndx: 1.8635

9 Angola

PwrIndx: 2.2599

10 Libya

PwrIndx: 2.3353

11 Sudan

PwrIndx: 2.3465

12 Democratic Republic of the Congo

PwrIndx: 2.6642

13 Uganda

PwrIndx: 2.6895

14 South Sudan

PwrIndx: 2.7689

15 Ghana

PwrIndx: 2.9726

16 Zimbabwe

PwrIndx: 3.0955

17 Cameroon

PwrIndx: 3.3009

18 Zambia

PwrIndx: 3.5013

19 Somalia

PwrIndx: 3.5462

20 Mozambique

PwrIndx: 4.1026

21 Madagascar

PwrIndx: 4.2547

22 Tanzania

PwrIndx: 4.3423



Chanzo: Countries Ranked by Military Strength (2014)[/


Ha ha ha tafiti zingine hazina mashiko. DRC, Nigeria, Somalia, South Sudani ziko juu ya Tz. Tuamini ipi?? Kati ya tafiti hii na ile iliyoweka Jwtz kuwa ni moja ya majeshi bora duniani? Hizo ni propaganda za Rwanda na Malawi.
 
Hii listi imepangwa na wanyarwanda nini??
Mbona nafsi inakataabkukubaliana na takwimu hizo!

Mpuuzi yeyote anaweza kuandaa ripoti yake ya utafiti wa kipuuzi kisha akaiandika kwa kiingereza akijua atawatisha wabongo.
Hiyo ni ripoti ya kipuuzi kama za wapuuzi wengine tu, huwezi kuniambia Somalia, Congo DRC ziko juu wakati hazina hata jeshi la kueleweka.
 
Mimi ni muumini wa wa fikra machipuko, huamini kuwa, hakuna upuuzi ulio upuuzi mtuputu, Vijana turuhusu akili zetu zizunguke nyuzi 360, tusijifungie kwenye matawa ya akili zetu, tusidumae katika muono huo huo,

Utafiti hupingwa kwa utafiti, kamwe haupingwi na matakwa ya mbongo zetu, niseme wazi, mimi nilipoona taarifa hii nilistuka, kwakuwa akili yangù iliamini kuwa Tz ni ya kwanza Afrika kwakuwa na jeshi imara hasa nikirejea historia ya ukombozi wa kusini mwa jangwa la Sahara na vita vya Uganda,

Ninawashangaa kweli tena ninawashangaa kwelikweli wale wote wanaopinga utafiti huu bila kupinga kwa utafiti mbadala, tangu watu waanze kuchangia hapa sijaona mtu akija na utafiti mbadala ili atushawishi kuupinga utafiti huu,

Nani anajua ripoti ya JWTZ ya uimara wa jeshi letu? Nani anajua ripoti ya Wizara ya Ulinzi juu ya uimara wa jeshi letu? Nani anayo na atuletee hapa ripoti yoyote mbadala ya uimara wa majeshi ya Afrika? Turuhusu mbongo zetu zitamalaki kwa mapana yote, tusifungwe na mawazo yetu mgando, tujenge tabia ya udadi yakinifu kwa falsafa ya sura tenge!

Hivi sisi tunaopinga huu utafiti tunatumia utafiti ama takwimu zipi zinazotambuliwa kitaifa na kimataifa?
 
Tanzania kipindi cha nyuma tulikuwa tunapambanishwa na nchi kama Ethiopia, Algeria, Misri nk, sio Kenya, Uganda, eti na Rwanda jamani!!!. Na hii inatokana na kuzidi kwa utawala mbovu ambapo ni chanzo cha kuingiza siasa Jeshini. Mafisadi yanapo tafuta kukubalika Jeshini kwa ajili ya usalama wao, nidhamu lazima ishuke kwa maofisa wa kuu wa Jeshi. Na hiyo inachangia kuharibu mfumo kwa masuala ya kiulinzi ambayo ni muhimu . Kiukweli tumeshuka japo sio katika kiwango hicho. Nafasi yetu bila shaka imechukuliwa na Angola.
 
Aliyeandika upuuzi huu ajaribu kutia mguu nchini ndipo atajua TZ ni ya mwishoni au la. Nchi ambazo masuala ya kijehsi yako surrounded na secrecy, huwezi kusema umefanya utafiti, chanzo cha data zako ni kipi.

somalia ina jeshi imara, bila serikali??
 
MKUU YERIKO Nakukubali mno,kwa hili nipo kinyume.

  1. Kenya wanasumbuliwa na al shabaab,wakenya wanauwawa na vijikundi vya kigaidi vidogo dogo.wangekuwa na intelgensia imara na jeshi imara,wasingesumbuliwa.kenya hajawahi kufanya mission yoyote ya kijeshi kama vile ukombozi wa kusini mwa Afrika nyakati zile,wana well equiped army,wanakosa displined army,wanakosa experienced army.
  2. Kongo hawana jipya,kabla aliingiliwa ikulu karibu auawawe miaka miwaili iliyopita,anasumbuliwa na vikundi vya waasi,M23 TZ chini ya mwavuli wa UNO waliwapa kipigo cha paka mwizi,na biashara yao ikaisha.Kongo angekuwa na inelgensia imara na jeshi imara angekuwamaliza vikundi vya waasi mwenyewe.Jizi tu Mheshimiwa Rais Kikwete alifunga mafunzo ya maafisa wa Jeshi,wengi walikuwa toka Kongo.
  3. Uganda zaidi ya miongo miwili anasumbuliwa na Joseph Kony,kijikundi tu kidogo ambacho kikitokea tanzania wanagongwa toka kwenye pori walilojificha na kesho tunahesabu Mizoga tu.angekuwa na jeshi imara asingesumbuliwa namna hiyo.
NB.Opesesheni ya Kumuondoa Mohamedi Bakari Commoro ilisemekana ni impossible Tz iliomba logistic tu,ikapata ikaenda na yule bwana aliondoka alfajiri na majeshi yetu yakamvalisha dila na mtandio,wakamwambia aende kwa amani.

Ukombozi wa nchi za kusini Mchango wa Tanzania,Sudani na nyingine nyingi.Nasikitika Yeriko kuwa mimi ni shabiki mkubwa na mwanachama wa CHADEMA,inapokuja issue ya kitaifa hasa jeshi mimi naliheshimu sana,unaandika hapo kwa sababu nchi ina amani kwa sababu ya jeshi letu unalolitusi,bora ungezungumzia jeshi la polisi kuliko JWTZ jeshi letu lililotukuka.

EAST AFRICA EAGLE naomba uje umpe shule Yeriko Nyerere na mods wapeleke uzi huu Jamii forum Intelgensia ambako kuna watu hawingii huku jukwaa la siasa,ili ajibiwe kwa weledi wa hali ya juu!

Kwa kumalizia wewe na mimi labda hatujui sawasawa kuhusu jeshi letu.Nashauri Ngome wamchukue Yeriko nyererer wakamhoji Pale Ngome upanga kwa nini analitusi jeshi letu tukufu.
Nmesikitishwa sana na ndugu Yeriko nyerere.

Ukana Shilungo.
Kaka ukana mimi nipo pamoja na wewe,Yericko ni mmoja wale watu ambao uchambuzi wao unaongozwa na itikadi zao.mimi nimeangalia hii web siku nyingi tuuinaitwa www.africaranking.com vigezo walivyotumia ni wingi wa vifaru,ndege,idadi ya askari na defence budget, sasa wewe unajeshi kubwa kama kenya alafu unashindwa kuwashika watu watano ambao wapo kwenye closed space kwa siku tatu hii ni sawa na mtu anayejisifu ana mtoto mkubwa kuliko mwenzie wakati mtoto mwenyewe taahira na mwenzie mdogo lakini IQ yake ni kubwa balaa.tuache kudharau vyetu akuna tulichojaribu kijeshi tukashindwa.
Lakini kaka kitu kingine yericko ni mwandishi mzuri tuu wa essay ambazo zina mpangilio mzuri lakini hazina uzito wowte katika uhalisia wowote
 
Kaka ukana mimi nipo pamoja na wewe,Yericko ni mmoja wale watu ambao uchambuzi wao unaongozwa na itikadi zao.mimi nimeangalia hii web siku nyingi tuuinaitwa www.africaranking.com vigezo walivyotumia ni wingi wa vifaru,ndege,idadi ya askari na defence budget, sasa wewe unajeshi kubwa kama kenya alafu unashindwa kuwashika watu watano ambao wapo kwenye closed space kwa siku tatu hii ni sawa na mtu anayejisifu ana mtoto mkubwa kuliko mwenzie wakati mtoto mwenyewe taahira na mwenzie mdogo lakini IQ yake ni kubwa balaa.tuache kudharau vyetu akuna tulichojaribu kijeshi tukashindwa.
Lakini kaka kitu kingine yericko ni mwandishi mzuri tuu wa essay ambazo zina mpangilio mzuri lakini hazina uzito wowte katika uhalisia wowote

Mkuu hivi huu ni uchambuzi wa Yericko au ni ripoti ya CIA??
 
Mkuu yeriko siwezi kukuunga mkono kwa ulichokiandika maana nikichekesho Somalia, Congo, Kenya ambayo inapeleka vifaru west gate itushinde?uongooo
 
Mkuu yeriko siwezi kukuunga mkono kwa ulichokiandika maana nikichekesho Somalia, Congo, Kenya ambayo inapeleka vifaru west gate itushinde?uongooo

Mkuu wangu nisamehe sana, sijaandika mimi haya,

Hiyo link inaeleza vizuri walioandika hayo!
 
Back
Top Bottom