Bora hiyo. Kuna moja saido alienda chini na beki wa Mlandege, akatoa pasi moja nzuri sana kwa Baleke ya kupress tu kidogo upande wa kulia wa goli. Yeye akabambikizia tena mabeki upande wa kushoto kipuuzi kabisa akaharibu nafasi nzuri sana ya kushinda goli la wazi. Na bado akaendelea kuharibu nafasi nyingine nzuri tena na tena! i
Kama wanaanza kupunguza wachezaji, binafsi naona waanze na Baleke. Jamaa ana IQ ndogo sana ya ushambuliaji. Nguvu nyingi kwenye vitu vya kutumia akili kidogo tu.
Namna bora ya kuwapunguza hawa kina onana, saido, sarr na wengineo ni kuwaletea competition tu. Yani waletwe vijana wa kuwakata namba na wao bado wakiwepo. Waone namna walivyotakiwa kucheza kupitia wachezaji wengine halafu watimuliwe mazima!