Fahamu A-Z kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Huu si muungano ni Uvamizi wa Tanganyika kwa Zanzibar
Ni rahisi kusema hivyo leo. Wakati ule mambo yalipokuwa magumu baada ya mapinduzi, survival ya mapinduzi ilikuwa ni kuungana na Tanganyika tu, ili kujiongezea uwezo wa kujilinda.
Tunaanza kudanganyana baada ya kushiba wali maharage ya kutoka bara kwamba muungano ni uvamizi. Huu muungano ni muungano wa upendo. Ingawa wana siasa wanaotaka madaraka kirahisi wanauchukia kweli
 
Survival gani Na nchi imevamiwa? Hakuna Mapinduzi ni uvamizi Na ndio miaka yote wavamizi wanamweka wao Raisi wanayemtaka
 
Usipotoshe watu. Tunajua na Kumbukumbu ziaonyesha hivyo kua kwa Upande wa tanganyika Muungano uliridhiwa na Bunge. Na kabla ya hapo ilitangangazwa kwenye Gazeti rasmi la Serikali. Upotoshaji unakuja kwa Upande wa Zanzibar, ni lini Baraza la Mapinduzi liliridhia Muunganoß Kuna minits zozote za baraza zinazoonensha hivyo kama Kisibitisho? Ni lini na gazeti lipi la Serikali ulitangazwa kabla ya kupitishwa na Baraza la Mapinduzi? Wakati Huo Salim rashid alikuwa ndie katibu wa baraza la Mapinduzi na kathibitisha hicho kitu hakikuwepo. Marehemu Nassor Hassan Moyo alikuwa ndio mtendaji mkuu wa Waserikali na ndie aliefuatana na Karume kwenda Dar kwa kiao Hicho cha Muungano na Nyerere na Mwanasheria wake wa Kingereza. Nassor Hassan Moyo hata hakuruhusiwa kuingia Kikaoni.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati ho alikuwa Wolfgang Durado na yeye hakuwa na habari na kathibitisha hadharani. Sasa hio habari wewe umeitolea wapi?
 

Kwanini Karume hakutaka kuwahusisha wenzake kwenye suala la Muungano? Kwanini huu Muungano tatizo linasukumwa Tanganyika na sio Zanzibar ambayo iliuhitaji sana huu Muungano sababu ya kulinda Mapinduzi yake? Kosa la Tanganyika liko wapi sasa kama mambo yote ya kisheria yalifuatwa upande wa huuu?
Historia inawacheka wanaotafuta mbuzi wa kafara. Nashangaa hawaongelei muingiliano wa watu, hasa kutoka Zanzibar kukaa Tanzania bara. Muungano ukivunjwa nani atakuwa majeruhi mkubwa? Hawa wanasiasa mbona kama wanachochea kuni wakati wengi wanaishi na kufanya kazi zao Tanzania Bara?
 
Mkuu tuanzie hapa.
Je, unaweza ainisha vitu ambavyo umeona nimedanganya hapo?
 

Zanzibar haijawahi kuuhitaji Muungano, Unatakiwa utafautishe Zanzibar na Karume au CCM
 
Mkuu tuanzie hapa.
Je, unaweza aunisha vitu ambavyo umeona nimedanganya hapo?
Kwanza hakuna neno aunisha katika Kiswahili. Umedanganya kusema kuwa Mkataba wa Muungano uliridhiwa na baraza la Mapinduzi sio kweli.
Kwa Upande wa Zanzibar hakuna chombo chochote ambacho kiliridhia mkataba huo. Na kama kweli kiliridhia ilikuwa Kopi ya mkataba huo ulioridhiwa uwepo UN. Kwa taarifa yako mpaka hivi sasa UN hakuna copy yoyote ya Mkataba wa Muungano, kilichokuwepo ni taarifa tu ya balozi wa tanganyika wakati huo aliekuweko UN ndio alitoa taarifa Upande mmoja kuwa nchi mbili ziliungana ambacho ni Kinyume na mikataba ya kimataifa. Kwa taarifa yako hivi sasa Wazanzibari wana kesi UN kuhusu Muungano na ukweli utatoka hadharani karibu sana
 
Kwani huo unaouita Munngano una faida gani kwa Zanzibar, ispokuwa ni Genge La Watanganyika kuwaweka Madarakani Vibaraka wao Zanzibar kwa Mgongo wa Mungano. Kama ni mMuingiliano wa Watu, wazanzibari wanamuingiliano zaidi na Mombasa lakini sio huu Ulaghai wa Kisiasa.
Hata nchi Za Europe zimeungana, unaweza kwenda nchi yoyote ukakaa na huulizwi na Mtu. Lakini kila nchi ina madaraka yake ya kujiamulia mambo yake. Na sisi Wazanzibari tunautaka zaidi huo muingiliano wa watu na sio ulaghai wa Kisiasa unaoitwa ukoloni
 
Zanzibar haijawahi kuuhitaji Muungano, Unatakiwa utafautishe Zanzibar na Karume au CCM
Naanzaje kutofautisha wakati ni sehemu hiyo hiyo ya mambo yenu wazanzibar? Mnabaguana sana bila sababu ya msingi. Tafuteni maendeleo. Siasa hizi zinawafitinisha bila sababu
 
Nini watanganyika wananufaika nacho sababu ya Muungano? Mnaongea mkiwa mmeshiba. Mnasahau chakula kinatoka wapi. Ngoja njaa ije ndio akili zitaingia kichwani.
Na huo umati wa watu sababu ya kuongezeka kwa kasi kubwa watakaa na kulima wapi? Mchanga na kujenga utatoka wapi? Mnashadidia mambo kama vile hamjawahi kusoma alama za nyakati mkazielewa
 
Umeongea kwa hisia sana mheshimiwa asante kwa taarifa hiyo maana kuna wengine wanalalama tu.
Bila shaka muungano huu unafaida zaidi Kwa wazanzibar zaidi za watanganyika
 
Kwenye hitimisho umesema muungano umechukua nafasi kubwa ya kuwaunganisha wananchi na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

Ungetusaidia kidogo kuhusu viongozi wa Tanzania bara Ni akina Nani? Na viongozi wa Tanzania Zanzibar ni akina nani? Katika kuimarisha hayo mahusiano otherwise ABCD zako zitakuwa hazina lengo la kudumuisha muungano zaidi ya kuficha matatizo ya muungano
 
Mkuu Rais wa sasa kwa Tanzania ni mzanzibar na makamu wake ni mtanganyika huo ndo muungano.
Vivyo hivyo sehemu mbalimbali kuna wazanzibar na watanganyika
 
Mkuu Rais wa sasa kwa Tanzania ni mzanzibar na makamu wake ni mtanganyika huo ndo muungano.
Vivyo hivyo sehemu mbalimbali kuna wazanzibar na watanganyika
Swali langu Muungano ni kati ya Tanganyika (Tanzania bara ) Kama mnavyoiita na Zanzibar ( Tanzania Zanzibar) uimara wa muungano huu unatokana na viongozi kati ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar

Viongozi wa Tanzania Zanzibar wapo je viongozi wa Tanzania bara ni akina Nani?

Embu orodhesha viongozi wa Tanzania bara hata wawili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…