Fahamu A-Z kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Naanzaje kutofautisha wakati ni sehemu hiyo hiyo ya mambo yenu wazanzibar? Mnabaguana sana bila sababu ya msingi. Tafuteni maendeleo. Siasa hizi zinawafitinisha bila sababu

Maendeleo yanadidimizwa na Wabara kuikalia kimabavu Zanzibar, hebu iacheni muone kama haitoendelea
 
Umeongea kwa hisia sana mheshimiwa asante kwa taarifa hiyo maana kuna wengine wanalalama tu.
Bila shaka muungano huu unafaida zaidi Kwa wazanzibar zaidi za watanganyika

Sasa kwanini watanganyika ndio wanaoung'ang'ania ?
 
Wewe ndio unazungumza kama umelewa vile. Inamaana huo Muungano ndio unatulinda sisi Wazanzibari na njaa? Wewe umesahau kuwa Bara walikuwa kila kitu wanachukua Zenji? Kwani hicho Chakula munatugawia bure au tunanunua kwa Pesa zetu? Kama tunanunua kwa nini tushindwe kununua kutoka nchi nyengne?
 
Viongozi hata wawili wa Tanzania bara ni;
Philip mpango~ makamu wa Rais
Majaliwa kassimu~ Waziri mkuu
 
Viongozi hata wawili wa Tanzania bara ni;
Philip mpango~ makamu wa Rais
Majaliwa kassimu~ Waziri mkuu
Majaliwa Kassimi ni waziri mkuu wa Tanzania au Tanzania bara(Tanganyika)?

Philipo Mpango ni makamu wa rais wa Tanzania au Tanzania bara (Tanganyika)

Elewa swali kwanza ndipo ujibu
 
Majaliwa Kassimi ni waziri mkuu wa Tanzania au Tanzania bara(Tanganyika)?

Philipo Mpango ni makamu wa rais wa Tanzania au Tanzania bara (Tanganyika)

Elewa swali kwanza ndipo ujibu
Naona hatuelewani
 
Ushahidi wa baraza la mapinduzi kuridhia muungano uko wapi ? Kama huna ushahidi wa hilo huwezi tumia jina la muungano, ni mavamizi ya Tanganyika dhidi ya Zanzibar.
 
Naona hatuelewani
Wewe umesema muungano ni kati ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar nimekubaliana na wewe.
Tumeona Zanzibar Ina uongozi wake sawa, swali langu wanaiongoza Tanzania bara ni akina nani?

Umemtaja Samia Suluhu,Philipo Mpango na Majaliwa Hawa Ni viongozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania sio viongozi wa Tanzania bara.

Tuambie viongozi wa Tanganyika ni nani Kama ilvyo kwa Zanzibar walivyo akina Hussein Mwinyi
 
kwa andiko lako hili matatizo na kero za muungano yanatokea kwa kutofahamu, mfano ARSO, EASC, ISO, CODEX, WTO na taasisi zote zinazofanana na hizo, zanziba haitakiwai kuwa mwanachama maana zinahusika na biashara za kimataifa. sasa Zanziba ina shirika lake la viwango na inapigania kuwa mwananchama wa taasisi za kikanda na kimataifa kuhusu biashara nilizozitaja hapo juu
 
Wabunge ndo wanaiongoza Tanzania bara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ