Fahamu chakula cha Escamoles kutoka Mexico.

Fahamu chakula cha Escamoles kutoka Mexico.

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Ni majira ya saa tano Bibi Isabella Martinez miaka 60 anaingia jioni kuandaa chakula kwa ajili ya familia, pembeni anasaidiwa na Mjukuu wake wa kike wa miaka 20, Maria. Bibi Isabella Martinez akiwa anatafuta kuni ili apate kuwasha moto basi Mjukuu yeye anaandaa viungo vitakavyokwenda kutumia katika pishi hilo la leo. Maria anakatakata vitunguu maji kiasi, pia anatengeneza na vitunguu swaumu, pilipili, karoti, pilipili hoho pamoja na nyanya kwa ajili ya kupata roast.
1727293948281.png


Bibi Isabella Martinez anaondoka na Mjukuu wake na kuelekea pembeni ya makazi yao kwenye miti na anaanza kuchukua kitoweo ambacho ndo kinaenda kupikwa. Bibi Isabella anachokitoa sio kitoweo cha kawaida, bali anatoa mayai na mabuu ya mchwa kutoka kwenye miti hiyo, wakiwa na kibeseni kidogo basi Bibi na Mjukuu wake wanakusanya kiasi cha kutosha kwa ajili ya chakua chao.

1727294008502.png


Wanarudi nyumbani wakiwa na furaha kwani jioni watakuwa na chakula kizuri sana cha asili ambacho kwa lugha yao kinaitwa Escamoles, chakula ambacho kinatengenezwa kwa kutumia mayai na mabuu ya mchwa aina ya Liometopum apiculatum, maarufu kama mchwa wanaopatikana kwenye miti.

1727294637703.png


Escamoles kwa baadhi ya watu unaweza kuwa ni mlo wenye kutia kinyaa ila ukifika mitaa ya Jiji la Mexico City kwenye migahawa kama vile Pujol, Nicos, Limosneros na mingine basi ukiagiza Escamoles unaletea mabuu ya mchwa yaliyopikwa kwa ustadi mkubwa sana, unabaki kushushia mlo wako na Modelo Especial ya baridi.

1727294081223.png


Chakula hiki cha Escamoles kimeanza kutumika kama mlo tangu enzi za Aztecs, hapa tunazungumzia karne ya 14, Aztecs ambao walikuwa na utamaduni wa kutumia Escamoles kama sehemu ya kujipatia protein kutokana na wadudu. Hivyo ufundi wa kupika chakula aina ya Escamoles umekuwa ukirithiwa kutoa vizazi na vizazi, maeneo kama Hidalgo, San Luis Potosi, Guanajuto, pamoja na Queretaro wamekuwa mstai wa mbele sana katika kufanya utamaduni wa kula chakul hiki kuendelea vizazi na vizazi.

Sio ajabu kukutana na mtoto akicheza vyema sana na sufuria katika kutengeneza mlo wake wa Escamoles. Mapishi ambayo Bibi Isabella Martinez anafanya alifundishwa na Mama yake ambaye kwa sasa ni marehemu na alifundishwa akiwa bado ni mtoto mdogo sana, ila namna na utaalamu wa kuvuna mabuu na mayai ya mchwa bado upo kichwani mwake mpaka sasa kwa zaidi ya miaka 50. Binafsi Bibi Isabella anadai kuwa chakula cha Escamoles kina ladha ya kipekee, ladhaa tamu sana mfano wa kula siagi.

1727294129547.png


Ukiachana na Mexico kuna baadhi ya migahawa duniani inatoa huduma ya chakula hiki, Ukienda Marekani pale Houston kwenye mgahawa wa Hugo’s basi ukiagiza Escamoles watakuletea, lakini pia Guelaguetza ndani ya Jiji la Los Angeles pia wanatoa huduma ya chakula hiki.

1727294248472.png


Watu wengi kutoka Mexico wamekuwa hawavutiwi sana na chakula hiki kikiandaliwa na kisasa na wanavutiwa kikiandaliwa kienyeji, kwani kwenye migahawa mikubwa wanaweka madoido mengi sana kupoteza ile ladha halisi ya mabuu ya mchwa hawo, wapo wanapika na kuongeza vitu kama, natural flavours na baadhi kupika mabuu kwa muda mrefu kiasi cha kufanya chakula kutepeta.

1727294363802.png


Nikuulize tu, Je ukifika kwenye migahawa na hoteli zetu ukapatia orodha ya vyakula, ukakuta kuna chakula hiki cha Escamoles, una ubavu wa kuagiza chakula hiki?​
 
Back
Top Bottom