SoC01 Fahamu fursa ya kutumia bussiness whatsapp kufanya biashara

SoC01 Fahamu fursa ya kutumia bussiness whatsapp kufanya biashara

Stories of Change - 2021 Competition

BussinessMentor

New Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
4
Reaction score
5
nawasalimu wote katika jukwaa hili la JamiiForum

Nitazungumzia bussiness whatsapp kama nyanja muhimu ya kujiingizia kipato


Mtandao wa whatsapp umekuwa ukipata umaarufu kila kukicha kwasababu unakua kwa kasi kila siku Kutoka kwenye status za kuandika mpaka status za picha na video. Kutoka kwenye magrupu yenye ukomo wa watu 60 mpaka sasa magrupu ya watu nyomi hadi 257.

Ni wazi kwamba mtandao wa WhatsApp umezidi kuwa bora ili kuendelea kuwafurahisha watumiaji wake. Bora ukose application zingine kwenye simu lakini si WhatsApp.

WhatsApp imekuwa zaidi ya sehemu ya kuchat na kutumiana jumbe zenye kufurahisha (meme), bali ni fursa ya kibiashara kwa wajanja.



Whatsapp bussiniss hutumiwa na watu wengi kutangaza biashara zao kupitia status na pia kupitia magroup mbali mbali ya kibiashara utakuta mtu mmoja kwenye whatsapp na viewerz Zaidi ya elfu moja inakuwa rahisi kuwafikia watu wengi kwa mda mchache

Watu wameanzisha magrupu ya WhatsApp kwa lengo la kuendesha semina na mafunzo mbalimbali. Kuendesha vikundi vya kukopeshana, maarufu kama ‘vikoba’. Vilevile magrup haya yanatumika kuhamasisha watu kujumuika kwenye matamasha na warsha mbalimbali.

Siku hizi hata vikao vya Sendoff na harusi vinaendeshwa kwenye magrupu ya WhatsApp. Kama bado umejiunga kwenye magrupu ya kipuuzi, basi umebaki wewe tu na wapuuzi wachache. Wenzako tunasaka fursa!

Yani siku hizi kupata namba ya mtu ni rahisi sana kwa sababu anajua baadaye utaona matangazo ya biashara yake kwenye status. Wala si kwa ubaya, ni katika harakati za kutafuta masoko na kujipatia riziki. Wewe ambaye huna cha kutangaza usione kero.



Kwa ujumla whatsapp business ni tofauti na whatsapp zingine kwasababu inavitu vya ziada

Sasa tuiangalie WhatsApp Business kiundani zaidi. Vitu ambavyo utavipata ndani yake ni kama ifuatavyo;.

  • Business profile
  • Ujumbe automatic wa salamu
  • Customer Management
  • Takwimu/statistics
  • Majibu ya haraka (quick replies)


Business Profile

Ukiangalia profile ya mtu anayetumia WhatsApp Business utaona ina muonekano tofauti na ile ya kawaida. Hapa utaona vitu kama jina la biashara, maelezo ya biashara (business description), location pamoja na siku na masaa anayofungua biashara yake. Hivi ni vitu ambavyo huwezi kuviona kwa mtu anayetumia WhatsApp ya kawaida.



Customer Management

Hapa unaweza kuchambua na kupangilia namba za WhatsApp ulizonazo katika makundi mbalimbali ya wateja. Kwa mfano unaweza kumwekea alama (label) kama vile mteja mpya, aliyelipa, asiyelipa, aliyetoa oda mpya na aliyemaliza oda yake.



Ujumbe Automatki wa Salamu


Hapa unaweza kutengeneza ujumbe wa salamu utakao kuwa ukitumwa kwa kila anayekutumia meseji. Ili kuondoa kero na usumbufu, ujumbe huu hutumwa endapo tu hamjawasiliana kwa kipindi cha siku 14. Ujumbe huu wa salamu unaweza kuwa unaelezea kwa ufupi juu ya shughuli unayofanya. Ni namna ambavyo wewe utapenda iwe.

Takwimu

Katika application ya WhatsApp Business, unaweza kupata takwimu kuhusu meseji ulizotuma. Utaweza kuona idadi ya meseji ulizotuma, zilizofika na zilizosomwa.

Quick replies and away message

Sikushauri utumie sana hii feature kwani humfanya mtu ajisikie kama ana wasiliana na roboti badala ya mtu. Kama namba yako ya mawasiliano ya kawaida ndiyo hiyo hiyo unatumia kwa biashara zako bora usitumie hii setting kwani si kila mtu ni mteja wako.



Jinsi ya kuwezesha WhatsApp Business

Ni rahisi sana kuseti business profile kwenye application ya WhatsApp Business. Unachotakiwa kufanya ni kwenda Playstore ama Appstore na kudownload WhatsApp Business. Baada ya hapo fungua application na uende kwenye Settings.

Kama unatumia android bofya kwenya vidoti vitatu upande wa juu kulia > Settings > Business settings > Hapo utaona setting zote unazotaka kufanya

Hitimisho:-

Kwanza nikuombe kura yako ni ya muhimu sana.Pia Biashara ya kutumia uwanja wa whatsapp inahitaji ujiunge kwenye magroup ya watu tofauti tofauti mfano kwenye maeneo ya vyuo vikuu kuna magroup mengi ya wanavyuo ambao wanamahitaji ya vitu vingi kama laptop,nguo na bidhaa zote za urembo kama mkufu na herein itakuwa rahisi kuwafikia wengi kwa mda mfupi

�~�W*)
 
Upvote 1
Back
Top Bottom