Fahamu jinsi ya kuanza biashara kwa mtaji mdogo (Mfano: Milioni 1)

Fahamu jinsi ya kuanza biashara kwa mtaji mdogo (Mfano: Milioni 1)

Hatujui mazingira uliyopo maana biashara ni kutatua changamoto za wanaokuzunguka
Maana tunaweza kukushauri uuze kuni au mkaa kumbe unaishi Masaki ambako wanatumia gesi tutakuponza au tukakwambia ufungue liquour store kumbe uko Zanzibar. Kwa hiyo deal na changamoto za hapo ulipo.

Ushauri wa jumla sasa kama wewe ni wa popote kambi , Jogoo hafi kwa utitiri ni hivi 😂😂

Nashauri Biashara ya mazao hasa maharage maana kidogo mzunguko wake uko chap na hayana process nyingi kama mazao mengine,Na ile flow yake unakua unaiona inavyopanda na kushuka. Usijihusishe na zile za kuweka store eti baadae bei ipande utaumia Hela ni ndogo hiyo!!
labda unaweza kutumia mbinu hii utajibana kwa zile faida unazopata ukawa unanunua mahindi utunze !! Ila ule msingi wa mtaji wako usipumzike yan ule ni kuzunguka tu ukikusanya kwa week unashusha mnadani unarudi kukusanya

Pia kwa huo mtaji ingia chimbo ununue na kuuza Mwenyewe. Usipige simu wala kuagiza kushirikiana na watu haikwepeki ila hakikisha na wewe uko miongoni sio kuambiwa ambiwa tu Zama chimbo msimu ukifika unanunua na kuleta mnadani hii unauza kwa ndoo (debe) ila si haba. Raha ya kuuza mnadani ni kwamba kwa mtaji wako hakuna mali kauli hakuna dalali ni wewe na wanunuzi direct ni kutoa cash unampa bidhaa.

Ukikaa vizuri ndo uanze kuleta town uhangaike na leseni za kuuza na kununua! (Ukifika hapa njoo tena tukupe ushauri tena)

Hiyo hela ukiiheshimu na ukawa mwaminifu (Nakazia hapa) na ukaishi na watu vizuri inakuchomoa ! Simaanishi utakua tajiri ila hautabaki ulipo.

Mungu akufungulie milango.
 
Wadau msaada ninamawazo ya kukopa bajaji kwa kutanguliza milion 1 lkn nikipiga hesabu ya marejesho na pesa uipatayo kwa dereva wa hiyo bajaji nikama daraja tu inapita kwako. Sasa kwa wale wazoefu nifafanulieni hili suala
 
😂😂😂 eeh etii jogooo afii kwa utitirii” una kituuu mkuuu , Tupeane mdaa tudiscus zaid
 
Wadau msaada ninamawazo ya kukopa bajaji kwa kutanguliza milion 1 lkn nikipiga hesabu ya marejesho na pesa uipatayo kwa dereva wa hiyo bajaji nikama daraja tu inapita kwako. Sasa kwa wale wazoefu nifafanulieni hili suala
Usifanye hiyo kitu utalia
 
Back
Top Bottom