Fahamu jinsi ya kutengeneza pesa kutumia Mobile App

The Master pizo

Senior Member
Joined
Dec 18, 2019
Posts
149
Reaction score
125
Habari za leo wandugu!

napenda kushirikishana nanyi jambo moja ambalo yamkini wengine walishalizungumzia au wanalifanya lakini sio mbaya na mimi nikiligua kwa nafsi yangu.

kwa kipindi hiki cha sasa kumekuwa na wimbi kubwa la kukosa ajira na hivyo kupelekea mai9sha kuwa duni kwa baadhi ya watu wengi lakini hiyo isiwe kigezo cha sisi kutokujaribu mambo mbali mbali hasa ya online kwa ajili ya kuona kama tutapata chhochote kitu.

kwanza tuanze kama ifuatavyo kama kichwa cha habari kilivyo kinahusu moja kwa moja masuala ya mobile app lakini mimi sizungumzii mambo ya coding yaani nazungumzia making app through other website that offer a free android app au application za kutengenezea appskuna site kama appgeyser, andromo, appcreator 24 sasa mimi nitazungumzia appcreator 24 ambayo inatoa nafasi nyingi za sisi kuweka matangazo.

APP CREATOR 24


hiyo site inakupa uwezo wa kutengeneza apps nyingi sana kama lakini mimi nitazungumzia kwa wale wenye blogs au website hii ndio itawafaa zaidi.
hapa ina maanisha kwamba tunatoka kwenye ule mfumo wa mtembeleaji kuingia google kukutafuta na badala yake anakuwa na application yako ambayo atakuwa anapata taarifa bila mzunguko wowote ule.
Sasa tuanze kutengeneza app ya blog yetu ili tuelewane

HATUA YA KWANZA
jisajili kwa kubonyeza hapo APPCREATOR 24
kisha baada ya hapo bonyeza mahali palipoandikwa CREATE APP kisha utajaza taarifa kama unavyoona hapo chini


Baada ya hapo bonyeza next utaletwa katika ukurasa huu hapo chini


chagua muonekano kisha bonyeza next kisha utaletwa mahali pa kuchagua aina ya app unayotaka kama picha inavyoonyesha hapo chini

sasa ukifika hapo chagua BLOG APP maana ndio nilichopanga kuelezea leo ukishabonyeza itafunguka sehemu inayofuata ambayo ndio ya muhimu sana

jaza jina la blog yako kisha chini ingiza link ya blog yako kwa usahihi kisha bonyeza next na tutakuwa tumemaliza kutengeneza app yetu utabonyeza hapo GO TO APP MANAGER

HATUA YA PILI
twende tukaingize matangazo katika app yetu hata kabla hatujaijaribu ili kuokoa muda
tutaenda kutumia site ya STARTAPP ili kuwekamatangazo yetu

jisajili hapa STARTAPP ili twende pamoja

baada ya kujisajili sasa bonyeza mahali pameandikwa my apps kisa bonyeza mahali pameandikwa add new app baada ya kubonyeza hapo utaletwa sehemu ya kuweka app url yako sasa kwa kuwa sisi hatujaiweka app yetu play store tunatakiwa tubonyeze pale chini palipoandikwa click here
baada ya hapo utatakiwa uingize app name na app platform

kisha tutabonyeza add app


sasa tumefikia pazuri tunywe maji kidoooogooooo

haya tuendelee sasa copy hiyo app ID utakayopewa hapo
baada ya ku copy twende kwenye ile site yetu ya mwanzo app creator 24
bonyeza mahali pameandikwa Ads paste ID yako mahali husika kwenye collumn ya startapp kama picha inavyoonyesha

baada ya kumaliza hatua zote hizo bonyeza save kisha nenda mahali pameandikwa download app bonyeza hapo ili kuipakua app yetu
sasa wakati unaipakua usisahau ku copy link yake ambayo utaikuta ndani ya maelezo kama kwenye picha hapo chini

baada ya kucopy link twnde kwenye site ya startapp ili tukamalize kazi bonyeza my apps kisha utaona app yako imeandikwa missing url


bonyeza hapo ili tuiweke ile link yetu ya app tuliyoicopy muda mfupi uliopita kisha chagua category na app maturity kama picha inavyoonesha kisha bonyeza alama ya tiki


mpaka hapo tumeshamaliza kila kitu now ni wakati wa ku install app yetu ili kuijaribu




now tumemaliza topic yet ya leo kama hujaelewa nakukaribisha DM kwa msaada zaidi
mbarikiwe

kujisajili bonyeza hapa APPCREATOR 24
kujisajili bonyeza hapa STARTAPP
 

Attachments

  • 1603110523844.png
    20.5 KB · Views: 40
Naomba kuuliza, kwanini programmers wanahangaika na coding wakati kuna njia rahisi ya kutengeneza apps.
Je integrations ninazoweka kwenye mobile app kupitia android studio ninaweza zifanya kupitia hizo app creators unazozisema?
 
Naomba kuuliza, kwanini programmers wanahangaika na coding wakati kuna njia rahisi ya kutengeneza apps.
Je integrations ninazoweza kwenye mobile app kupitia android studio ninaweza zifanya kupitia hizo app creators unazozisema?
Huwezi hata siku moja. App creator nyingi zinatumia library za zamani. UI za app zake kma unavyoona hapo juu ni mbovu na outdated. Na pia iko limited na vitu unavyoweza fanya. Hzo creator mara nyingi zinaweza kutengeza basic apps tu zisizo na complication. Na compatibility ya hzo app ni mbovu.
 
Naomba kuuliza, kwanini programmers wanahangaika na coding wakati kuna njia rahisi ya kutengeneza apps.
Je integrations ninazoweza kwenye mobile app kupitia android studio ninaweza zifanya kupitia hizo app creators unazozisema?
Jibu ni No unayotumia NJIA hiyo ni kwamba wewe unafata MFUMO wap wa utengenezaji Na sio MFUMO wako

Muonekano ni kutoka kwao Labda Utumie drag and drop like sketchware or thunkable
 
Kiufupi ni kwamba Hizo app creator ni kwa wale wasio na Elimu ya coding Na HAWANA pesa sidhani kama mtu Mwenye pesa yake anawaza kutumia Hizo Appcreator maana ni za hadhi yako chini Ila kibongo bongo unazikuta mpaka play store

App creator ninayoipenda ni sketchware japo Ni ngumu kidogo
 
Kuna appcreator zilozo boreshwa lakini
 
Naomba kuuliza, kwanini programmers wanahangaika na coding wakati kuna njia rahisi ya kutengeneza apps.
Je integrations ninazoweka kwenye mobile app kupitia android studio ninaweza zifanya kupitia hizo app creators unazozisema?
Kila kilicho rahisi kina gharama

1:ukitengeneza app yako kwa code maana yake utaweka matangazo yako 100% na utachovuna ni 100% ya kile ulicho takiwa kupata ila kwa hawa appcreator wao wanaweka 40%-20% matangazo yao hivyo kuna kiasi utakikosa

Ukiona umepata 60000/=tsh maana yake ulitakiwa kupata laki...

Kingine hauwezi kua flexible online app creator hua wana theme ,widgets na templates zao so huwez create kitu unique lazima ufate the way wao wanataka udesin
 
unachoongea kina ukweli kwa sababu wao wamekupa free app yao na kukuwekea sehemu ya kupata chochote kwa njia ya matangazo usitegemee watakupa pesa yote wewe wao wataendeshaje ofisi yao?

haina tofauti na site za freelancer ambazo wanakukata kwenye malipo uliyolipwa
 
Oky oky kutengeneza ni kiasi gani mzeee ili ikutafye inbox
 

Mtoa mada unajifurahisha hivi maisha yangekuwa simple hivyo si kila mtu angekuwa coder?...Tuache uvivu kams tunapenda kupata hela via codes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…