Fahamu jinsi ya kuwasiliana na Viziwi kwa njia ya Alama

Fahamu jinsi ya kuwasiliana na Viziwi kwa njia ya Alama

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Habari za saizi wakuu,

Twende moja kwa moja kwenye mada yetu ya Leo.

Lugha ya alama nini?

Lugha ya alama Tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa hadhira iliyokusudiwa na jamii husika.

Lugha ya alama imegawanyika katika makundi mawili;

1. Alama kwa njia ya herufi (alphabet)
2. Alama kwa njia ya ishara.

Katika mada hii ntaongelea zaidi kipengele cha kwanza ambacho ni ALAMA KWA NJIA YA HERUFI..

Kwanini?

Kwa sababu kipengele hiki ni rahisi kumfundisha mtu aliye mbali na akaelewa mfano hapa JAMII FORUMS.

Kipengele cha pili hufundishwa MUBASHARA .

Tulisongeshe,

ALAMA KWA NJIA YA HERUFI (ALPHABET)

Herufi A, B, C,D,E,F,G, H,I,J, K, L, M,N,O mpaka Z huweza kuandikika kwa kutumia vidole vyetu.

Mbinu gani hutumika?

Mbinu zitumikazo hapa ni kukunja vidole kwa kufuata umbo la herufi husika.

Mfano herufi "C" ukitizama katika picha hapo chini utaona KIDOLE GUMBA na vidole vingine vimekunjwa kuunda shape ya herufi C. Utaratibu huu pia hutumika katika kuandika herufi zinazo fuata.

NB: Herufi "I" na "J" katika picha utaona kama zinafanana, utaratibu wa kuzitofautisha upo hivi, UKITAKA KUANDIKA HERUFI J ANZA KWA KUANDIKA HERUFI ,"I" THEN KUWA KAMA UNACHORA HERUFI J HEWANI.

72453ddd3ee3cd7b225040237ac64135.jpg

55ac6f54a4f4accaf3df94ff08e5cb9d.jpg

Wakuu TUMIENI umakini kuchunguza MIKUNJO YA VIDOLE pamoja na alama husika mtagundua mikunjo ya vidole na imekunjwa kwa kufuata UMBO LA HERUFI HUSIKA. Mfano mzuri tizameni herufi Y.

HERUFI HIZI HUTUMIKA JE?

Herufi hizi hutumika kwa kuandika neno au maneno uliyokusudia kwa mhusika (kiziwi) kwa kufuata herufi tajwa hapo juu katika picha.

Jaribu sasa kwa kuanza na maneno kama DADA, KAKA, MAMA, BIBI n.k,
Ni rahisi sana na utaweza kuwasiliana au kuongea na kiziwi yeyote.

Karibuni kwa nyongeza , maoni, hoja na maswali.

Ahsanteni.
 
Hizo kuna bubu flani alinifundisha zamani kidogo, basi kila tukikutana tulikuwa tunapiga story na tunacheka kabisa yaani.

Ukizizoea zinakuwa tamu sana, sasa uwakute mabubu wanaongea hehe. Jamaa hata kama ulijifunza lazima utoke kapa vyenye wanazipeleka fasta.
 
Hizo kuna bubu flani alinifundisha zamani kidogo, basi kila tukikutana tulikuwa tunapiga story na tunacheka kabisa yani,
Ukizizoea zinakuwa tamu sana, sasa uwakute mabubu wanaongea hehe. Jamaa hatakama ulijifunza lazima utoke kapa vyenye wanazipeleka fasta
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]
Mkuu hii elimu hasa hasa kipengele cha pili ili uimudu vizuri lazima uwe unapractice kila mara,
Nikipata muda nitatoa elimu nyingine kuhusu namna ya kuandika namba kwa ishara.
 
Hivi ukishaijua SI ndio UNIVERSAL?.....hamna haja ya kujifunza French, English n.k???
Ndio ni UNIVERSAL lakini ina barrier nyingi kama , sababu hutoweza kuwasiliana vizuri sehemu zifuatazo,
1.Gizani
2.kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi
3.nk
Pia umbali ni barrier
 
Habari za saizi wakuu,
Twende moja kwa moja kwenye mada yetu ya Leo,

Lugha ya alama nini?

Lugha ya alama tanzania ni chombo cha mawasiliano ambacho humuwezesha mzungumzaji kufikisha ujumbe kwa jamii kwa adhira iliyokusudiwa na jamii husika.

Lugha ya alama imegawanyika katika makundi mawili,

1. Alama kwa njia ya HERUFI ( alphabet)
2. Alama kwa njia ya ishara.

Katika mada hii ntaongelea zaidi kipengele cha kwanza ambacho ni ALAMA KWA NJIA YA HERUFI

Kwanini?

Kwa sababu kipengele hiki ni rahisi kumfundisha mtu aliye mbali na akaelewa mfano hapa JAMII FORUMS,
Kipengele cha pili hufundishwa MUBASHARA .

Tulisongeshe,

ALAMA KWA NJIA YA HERUFI (ALPHABET),
Herufi A, B, C,D,E,F,G, H,I,J, K, L, M,N,O,....mpaka Z
Huweza kuandikika kwa kutumia vidole vyetu,

Mbinu gani hutumika??

Mbinu zitumikazo hapa ni kukunja vidole kwa kufuata umbo la herufi husika.

Mfano herufi "C" ukitizama katika picha hapo chini utaona KIDOLE GUMBA na vidole vingine vimekunjwa kuunda shape ya herufi C,
Utaratibu huu pia hutumika katika kuandika herufi zinazo fuata.

NB: herufi "I" na "J" katika picha utaona kama zinafanana, utaratibu wa kuzitofautisha upo hivi, UKITAKA KUANDIKA HERUFI J ANZA KWA KUANDIKA HERUFI ,"I" THEN KUWA KAMA UNACHORA HERUFI J HEWANI.
72453ddd3ee3cd7b225040237ac64135.jpg

55ac6f54a4f4accaf3df94ff08e5cb9d.jpg

Wakuu TUMIENI umakini kuchunguza MIKUNJO YA VIDOLE pamoja na alama husika mtagundua mikunjo ya vidole na imekunjwa kwa kufuata UMBO LA HERUFI HUSIKA,
Mfano mzuri tizameni herufi Y
HERUFI HIZI HUTUMIKA JE ??

Herufi hizi hutumika kwa kuandika neno au maneno uliyokusudia kwa mhusika (kiziwi) kwa kufuata herufi tajwa hapo juu katika picha,

Jaribu sasa kwa kuanza na maneno kama DADA, KAKA, MAMA , BIBI n.k,
Ni rahisi sana na utaweza kuwasiliana au kuongea na kiziwi yeypte

Karibuni kwa nyongeza , maoni, hoja na maswali.

Ahsanteni
Tumia picha ya pili iliyopitishwa na CHAVITA. Hiyo ya kwanza ni sahihi kwa nchi nyingine, lakini baadhi ya alama hazitumiwi Tz.
 
Umenikumbusha zamani sana mdogo wangu alikua na rafiki wa aina hiyo wakawa wanakuja nyumbani wanaongea kwa ishara ya vidole na vitendo wananisema wanacheka sijui kitu nikatumia mda kujifunza alama za vidole izo juu nilivo jua nilijisikia furaha akija dogo ayupo tunaongea nae fresh akawa anafurahi hajisikii upweke aliipenda sana familia yangu akawa kama mwanafamilia ukizijua hizo alama unakuta yeye mwenyewe anakufundisha na vitendo mfano mama unashika maziwa, baba unashika kichwa na kidevu babu unashika kichwa na mkono unaigiza kama kushika bakora, dada unakunja ngumi na kunyoosha kidole cha shahada nyumba unakutanisha vidole vyote vya mikono kama pembe tatu ni raha sana ukijua
 
Hivi ukishaijua SI ndio UNIVERSAL?.....hamna haja ya kujifunza French, English n.k???
Kila nchi wana lugha yao ya alama mfano American Sign Language, French Sign Language, Tanzania Sign Language.

Baadhi ya herufi za lugha ya alama zinatofautiana kati ya lugha ya alama ya nchi moja na nyingine. Zaidi ya hapo kuna alama za namba ambazo zinazotumika Tanzania (kutokana na lugha ya Kiswahili) zinatofautiana na zile zinazotumika Uingereza (zinazotokana na luvha ya Kiingereza).

Lugha ya alama haikamiliki kwa kujua alama za herufi na nambari, bali kuna alama nyingine nyingi ambazo pia hupitishwa kutokana na lugha ya kawaida ya nchi husika. Mfano, alama ya Morogoro ni kuchora herufi 'M' ya kawaida hewani, wakati alama hiyo hiyo inaweza kumaanisha kitu kinginr katika lugha ya alama ya nchi nyingine.

Hivyo tambua lugha ya alama sio Universal kwa maana ukiijua ya Tanzania utamudu kuwasiliana na Mkenya, Mtaliano, Mmarekani na Mchina pasipo vikwazo.

Sanjari na hayo lugha ya alama ni maalum kwa ajili mawasiliano miongoni mwa watu walio na matatizo ya kusikia na wasio na matatizo hutumia kuwasiliana na wenye matatizo. Hivyo umuhimu wa kukua lugha za kimataifa kama Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kichina unabaki pale pale.
 
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]
Mkuu hii elimu hasa hasa kipengele cha pili ili uimudu vizuri lazima uwe unapractice kila mara,
Nikipata muda nitatoa elimu nyingine kuhusu namna ya kuandika namba kwa ishara.
Well said mkuu
 
Kila nchi wana lugha yao ya alama mfano American Sign Language, French Sign Language, Tanzania Sign Language.

Baadhi ya herufi za lugha ya alama zinatofautiana kati ya lugha ya alama ya nchi moja na nyingine. Zaidi ya hapo kuna alama za namba ambazo zinazotumika Tanzania (kutokana na lugha ya Kiswahili) zinatofautiana na zile zinazotumika Uingereza (zinazotokana na luvha ya Kiingereza).

Lugha ya alama haikamiliki kwa kujua alama za herufi na nambari, bali kuna alama nyingine nyingi ambazo pia hupitishwa kutokana na lugha ya kawaida ya nchi husika. Mfano, alama ya Morogoro ni kuchora herufi 'M' ya kawaida hewani, wakati alama hiyo hiyo inaweza kumaanisha kitu kinginr katika lugha ya alama ya nchi nyingine.

Hivyo tambua lugha ya alama sio Universal kwa maana ukiijua ya Tanzania utamudu kuwasiliana na Mkenya, Mtaliano, Mmarekani na Mchina pasipo vikwazo.

Sanjari na hayo lugha ya alama ni maalum kwa ajili mawasiliano miongoni mwa watu walio na matatizo ya kusikia na wasio na matatizo hutumia kuwasiliana na wenye matatizo. Hivyo umuhimu wa kukua lugha za kimataifa kama Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kichina unabaki pale pale.
Thanks mkuu, basi Mimi nilidhani ni universal.
 
Sipati picha bubu wa Kikuyu akikutana na bubu wa kisandawi hali inakuwaje wakati wa mawasiliano kwa ishara za herufi!
====
Asante sana mleta uzi.
 
Kwa faida ya wale wanaotaka kujifunza lugha ya alama ya Tanzania waende CHAVITA kununua kamusi ya lugha ya alama na santuri ya video (Video CD). Hakika ni rahisi sana kujifunza lugja ya alama.
Ofisi za chavita zipo wap?Na wapi naweza jifunza hii lugha
 
Hongera MKUU umejitahidi xana. Poa ni muhim sana kwa watu wote wenye uwezo wa kusikia sauti kujifunza lugha hii ili kuwasaidia hawa wenzetu viziwi. Namshkur mungu nimejifunza lugha hii Na kwa sasa naweza kuwasiliana nao vizur n pia nawafundisha masomo yote. Ni lugha nzuri sana ila ni lugha ambayk haina siri kwa maana kuwa ukiongea kwa ishara mwingine anaweza kuona Na kujua unachoongea.
 
Kwa wale mnaopenda kutongoza au kutongozwa Na viziwi kuweni makini maana hawa viziwi lugha yso haina siri Na pia wana mapenzi ya kweli akipnda anapenda kweli hatanii kama mnaosikia sauti
 
Hizo kuna bubu flani alinifundisha zamani kidogo, basi kila tukikutana tulikuwa tunapiga story na tunacheka kabisa yani,
Ukizizoea zinakuwa tamu sana, sasa uwakute mabubu wanaongea hehe. Jamaa hatakama ulijifunza lazima utoke kapa vyenye wanazipeleka fasta
Neno Bubu hua c vema kulitumia,maana wenyewe viziwi hawalipendi Na endapo akijua umemwita yy Bubu hapo kidg kutakua Na shida.tumia neno kiziwi ndo maana sahihi.
 
Kila nchi wana lugha yao ya alama mfano American Sign Language, French Sign Language, Tanzania Sign Language.

Baadhi ya herufi za lugha ya alama zinatofautiana kati ya lugha ya alama ya nchi moja na nyingine. Zaidi ya hapo kuna alama za namba ambazo zinazotumika Tanzania (kutokana na lugha ya Kiswahili) zinatofautiana na zile zinazotumika Uingereza (zinazotokana na luvha ya Kiingereza).

Lugha ya alama haikamiliki kwa kujua alama za herufi na nambari, bali kuna alama nyingine nyingi ambazo pia hupitishwa kutokana na lugha ya kawaida ya nchi husika. Mfano, alama ya Morogoro ni kuchora herufi 'M' ya kawaida hewani, wakati alama hiyo hiyo inaweza kumaanisha kitu kinginr katika lugha ya alama ya nchi nyingine.

Hivyo tambua lugha ya alama sio Universal kwa maana ukiijua ya Tanzania utamudu kuwasiliana na Mkenya, Mtaliano, Mmarekani na Mchina pasipo vikwazo.

Sanjari na hayo lugha ya alama ni maalum kwa ajili mawasiliano miongoni mwa watu walio na matatizo ya kusikia na wasio na matatizo hutumia kuwasiliana na wenye matatizo. Hivyo umuhimu wa kukua lugha za kimataifa kama Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kichina unabaki pale pale.
Swadakta MKUU umemaliza.asante kwa kutoa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom