Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Hakika mkuu
Taarifa nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FAHAMU: Karantini binafsi (Self-quarantine)

Karantini binafsi inamaanisha kujizuia kuwasiliana ama kukutana na watu wengine na jamii kwa ujumla kadri iwezekanavyo.

Mtu anahitaji kufanya hivyo ikiwa amekutana na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona na bado yuko katika hali nzuri (hana dalili za COVID-19).

Kujiweka karantini binafsi ni muhimu ili kuzuia watu wengine kupata maambukizi.

Hii inajumuisha kukaa nyumbani au kusalia katika makazi ya peke yako kwa muda wa siku 14.

Bado muhusika anaweza kwenda nje kwa matembezi, kufanya mazoezi au mizunguko ya peke yake lakini hapaswi kukaribiana zaidi na watu wengine.
 
Wakuu naomba kujuzwa mtu wa kwanza mweusi Mwenye asili ya Afrika kufariki kwa corona.!
Je kuna ukweli kuwa virus hawa hawana athari kubwa kwa watu weusi ukifananisha na wenye ngozi nyeupe?
Sikusudii kuleta hoja ya ubaguzi wa rangi lakini natamani kujua.
Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndo wanao report ukweli
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe jibu unalo mkuu. Chukua tahadhali now. Maana jina lako hilo mzigo ukiwasili mjini hapa, sisi wenye majina yetu tutakusindikiza yan.
Na yule mchezaji wa Leceister imekuwaje amepatwa na Corona? Au kwa kuwa anatumia jina la kizungu
Just some jockes! Ila kiukweli blacks nadhan bado tunao uwezo wa kuumudu ugonjwa huu hadi sasa. Labda tuone huko mbeleni. Ukute haujatuvamia vilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…