Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Kumekuwa na taarifa nyingi sana kuhusiana na hili janga; uwepo wa visa, watu kushukiwa, watu kufa n.k. lakini mara nyingi taarifa hizo zimekuwa zikikanushwa.

Uwezo wa kubaini uwepo wa visa hivyo nchi nzima ni changamoto kubwa kwa mataifa mengi katika hatua za kukabiliana na COVID-19.

Kuchukua tahadhari ndiyo njia pekee inayobaki lakini bado pia kuna changamoto kubwa kuhusiana na hilo.

Kuna uwezekano huo wa kuwepo kwa visa na pia kinyume chake ingawa ni ngumu sana kusema kinyume chake kutokana na muingiliano wa kimipaka kati ya nchi na nchi, watu na watu, bado ni mkubwa.
Hakika mkuu
Taarifa nzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FAHAMU: Karantini binafsi (Self-quarantine)

Karantini binafsi inamaanisha kujizuia kuwasiliana ama kukutana na watu wengine na jamii kwa ujumla kadri iwezekanavyo.

Mtu anahitaji kufanya hivyo ikiwa amekutana na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona na bado yuko katika hali nzuri (hana dalili za COVID-19).

Kujiweka karantini binafsi ni muhimu ili kuzuia watu wengine kupata maambukizi.

Hii inajumuisha kukaa nyumbani au kusalia katika makazi ya peke yako kwa muda wa siku 14.

Bado muhusika anaweza kwenda nje kwa matembezi, kufanya mazoezi au mizunguko ya peke yake lakini hapaswi kukaribiana zaidi na watu wengine.
 
Wakuu naomba kujuzwa mtu wa kwanza mweusi Mwenye asili ya Afrika kufariki kwa corona.!
Je kuna ukweli kuwa virus hawa hawana athari kubwa kwa watu weusi ukifananisha na wenye ngozi nyeupe?
Sikusudii kuleta hoja ya ubaguzi wa rangi lakini natamani kujua.
Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndo wanao report ukweli
UPDATE: Italia

Visa 17,660 vimethibitishwa nchi nzima hadi hivi sasa.

Vifo 1,266 hadi sasa vimehusishwa na COVID-19 nchini humo.

Wenye ahueni wafikia 1,439 huku 1,328 hakiwa katika hali mbaya zaidi.

Nchi nzima yawekwa kizuizini, shughuli mbalimbali za kijamii zasitishwa, maduka, migahawa n.k. yafungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe jibu unalo mkuu. Chukua tahadhali now. Maana jina lako hilo mzigo ukiwasili mjini hapa, sisi wenye majina yetu tutakusindikiza yan.
Na yule mchezaji wa Leceister imekuwaje amepatwa na Corona? Au kwa kuwa anatumia jina la kizungu
Just some jockes! Ila kiukweli blacks nadhan bado tunao uwezo wa kuumudu ugonjwa huu hadi sasa. Labda tuone huko mbeleni. Ukute haujatuvamia vilivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom