Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)


Kwa inchi za Afrika wala siamini kama idadi iko hivyo

Coz tunakatabia kakusema tutawastua wanainchi
 
Arabuni naona wanasavaivu......na afrika kwa mbali China na Italy ndiyo wameathirika sana....tuombe kheri mambo ni mazito sana.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa naona Taarifa kwa vyombo vya habari zikitolewa na viongozi wetu ila kwa lugha moja tu ya Kiswahili.

Napendekeza kuwa:
Kuwe na utaratibu RASMI wa kuhakikisha kuwa TAARIFA zote muhimu za kitaifa na Kimaataifa, ziwe zinatolewa kwa Lugha mbili, yaani KISWAHILI na KIINGEREZA

Nimeandika kwa nia njema kwani, kutoa taarifa kwa lugha ya Kiswahili pekee na kuachia watu wajitafsirie mtaani wenyewe; kunatoa nafasi kwa watu wasio kuwa na nia njema kujitafisiria kwa kadri wanavyoona inafaa.

Lakini pia, kuna mashirika mengi yana watu wasio kuwa na umahiri wa lugha ya kigeni, hivyo wanavyo ambiwa watafisiri, huishia kutafisiri KWA LUGHA NYEPESI NYEPESI huku akijifanya kuwa, hakuna jipya ILA kimsingi ni kuwa hana uelewa wa kutosha wa kutafsiri (Kumbuka: Mashirika ya wakezaji haya ajiri wakalimani).

Kwa suala la Corona kwa sasa ambalo lina athiri afya za watu wengi Globally na biashara hasa ya utalii; napendekeza kuwa kila linapotolewa tamko litolewe mara moja nakala zote mbili (ya Kiswahili na Kiingereza) itumwe kwenye taasisi inayosimamia makampuni ya wageni - TATO ili wafikishie wanachama wao.

Na hata yanapotolewa matamko mengine yanayo gusa Biashara , Mfano kubadilika kwa tozo mipakani, kwenye vivutio nk nakala zote mbili (Kiswahili na Kiingereza) zitumwe MARA MOJA kwa TATO. Nafikiri hiyo ni njia nzuri ya kuwasiliana na wadau na kuonyesha kuwa Tuna wajali

Kimsingi kuna TAARIFA muhimu zinatolewa ILA haziwafikii baadhi ya wadau muhimu wakiwemo WAWEKEZEZAJI kwa uzito uliokusudiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…