Awali ya yote niwape pole wakazi wa Arusha kwa taharuki iliyowakumba pamoja na nchi yote kwa ujumla.
Tukio la kugundulika mgonjwa wa Corona ni pigo kubwa katika jamii yetu kiuchumi na kijamii, shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zimeanza kuyumba.
Hii ni kutokana na historia mbaya ya gonjwa hili la kutisha.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimesikitishwa sana na kiongozi/mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambavyo hajaonyesha umakini na unyeti katika gonjwa hili.
Tizama video ili twende pamoja
Mh. Gambo alipokwenda kwenye tukio hotelini/Lodge ya Themi valley plot no 120, akiongozana na RPC na maafisa wengine wa jeshi, wameenda kama vile wanaenda kuigiza..location.
Hii ni kutokana na wao kutovalia vifaa vya kujikinga.
Maafisa wa Polisi pamoja na Gambo mwenyewe wengi wao aidha wamevaa mask pekee bila kuvaa gloves au kutokuvaa vyote kabisa.
Hii inasikitisha kwani wao ndio wanapaswa kuwa mfano kwa kizazi cha kibongo kisichojua chochote katika kujikinga na gonjwa hili.
NATOA RAI SI KWA GAMBO PEKEE BALI KWA VIONGOZI WOTE KUWA MFANO WA KUIGWA KWA KUVAA VIFAA MAHUSUSI VYA KUJIKINGA NA GONJWA HILI
Poleni Themi Valley lodge, mna mandhari nzuri, kuna wakati mlinifaa sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app