Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mpaka sasa ni wazi kuna factors zinazo-influence kusambaa kwa ugonjwa huu na factors hizo huenda ndio chanzo kikubwa cha tofauti ya kusambaa ugonjwa huu katika nchi za Kiafrika na zile za Ulaya, Marekani na Asia.
Hata tofauti ya idadi ya vifo nayo ni sababu moja wapo inayoponyesha umuhimu na ulazima wa jambo hili kufanyiwa utafiti.
Nasema hivi kwasababu siku zote linapokuja suala la umasikini na magonjwa, Afrika ndio huongoza kama ilivyo kwa HIV, kipindupindu n.k ila kwa corona naona hali inakuwa tofauti kabisa.
Ugonjwa huu ulianzia huko China na kama ni kusambazwa na abiria wanaosafiri kwa ndege, basi hata Afrika ilipaswa iwe imeathirika kwani kuna ndege nyingi tu zinaingia Afrika kutoka China kama ilivyo kwa Ulaya,Marekani na Asia.
Kingine cha ajabu ni kuwa, hivi sasa nchi za Ulaya na Marekani zinachukua hatua za juu sana katika kudhibiti ugonjwa huu zikiwemo kuzuia ndege kuingia katika nchi hizo, kufunga mipaka, kuzuia raia wake kutoka majumbani n.k,huku sisi Afrika tukizembea kabisa ila bado tu rate ya kusambaa huu ugonjwa Afrika bado iko chini mpaka sasa.
Swali ni je, hali hii inatokana na nini? Hapa hatuoni kuna umuhimu wa kufanyika utafiti wa kina juu ya jambo hili?
Au Afrika tuna vipimo duni na vichache kutosheleza kubaini maambukizi ya huu ugonjwa na hivyo inawezekana tuna wagonjwa wengi tu wasiojulikana?
Au ndio baada ya muda gonjwa hili litabakia Afrika kwa wingi na kwa muda mrefu huku likiwa limedhibitiwa katika nchi za wenzetu?
Maswali ni mengi kuliko majibu!!