Habari, Ndugu watanzania wenzangu na dunia kwa ujumla. Natumai mko wazima na afya njema. Kwa hakika dunia kwa sasa inashuhudia janga kubwa la virus huyu wa Corona. Kuna mamilioni ya watu tayari wameshaathirika na wengine wengi wamopoteza maisha ila pia wapo waliopona.
Kwa mpaka sasa
CHINA ina case 80,928 kwa ujumla, ikiwa 34 na zaidi ni mpya. Jumla ya idadi ya waliokufa ni 3,245, ikiwa vifo vipya 8 na zaidi. Hata hivyo watu 70,420 wamepona. Kesi zinazofanyiwa kazi kwa sasa zimebakia 7,263 katika hizo 2,274 ni sugu na pengine haziwezi kutatulika.
Nchi ambazo zimeathirika sana ni China, Italy, Iran, na Spain. Lakini Nchi ambazo zinakamatwa na ugonjwa huu kwa kasi mno kwa sasa ni USA na South Korea.
Ikiwa idadi ya kesi zote marekani ni 9,464 na 205 na zaidi ni mpya zinaongezeka. Idadi ya vifo vyote marekani 155 na 8 na zaidi ni vipya vinavyoongezeka. Na idadi ya watu 108 wamepona na kesi 64 ni sugu zikitarajiwa hazina matibabu. Katika South Korea idadi ya kesi zote ni 8,565, ikiwa 152 na zaidi ni kesi mpya zinazoengezeka. Idadi va vifo vyote Souuth Korea ni 91 na 7 na zaidi ni vifo vipya vinavyooengezeka. Watu 1,947 wamepona na ikiwa kesi 59 ni sugu zinazotarajiwa kuwa hazina matibabu.
Katika nchi yetu Tanzania Mpaka sasa kuna kesi 6 jumla na 3 na zaidi zikiongezeka. Tunamshukuru mungu hakuna aliyekufa na wala hakuna kesi sugu. Kama inavyoonekana katika picha niliopiga katika website inayokusanya taarifa zote za corona Virus
Ama kuhusu hali ya kiuchumi, kampuni nyingi zimefungwa. Lakini serikali ya Italy imetoa amri maduka yote, baa, na migahawa ifungwe kwa muda. Kwa hiyo huko Italy hali ya kiuchumi inazidi kuwa ngumu. China baadhi ya viwanda vimerudi katika utendaji kazi wa kawaida wa siku zote. Ila bado changa moto ya uchumi na kibiashara inatagemewa kuwepo kwa sababu China ndio Tegemeo la African na Nchi Nyingi ikiwemo Marekani. Hivyo China viwanda vinafanya kazi vizuri baadhi ila ngege na meli nyingi za kusafirisha mizigo zimesimamishwa kufanya kazi. Bali kampuni chache ndio zinafarisha ila kwa bei ghali mara mbili zaidi ya awali ikiwemo UBI ,UPS, na DHL.
Pia marekani inategemea lock-down yaani kufunga baadhi ya maduka, super market na migawa katika wiki chache zijazo kulingana na hali itakavyokuwa.
Lakini pia Japan huenda ikathibitisha ya kuwa dawa za kutibia mafua ambazo ni Avigan huenda zikauwa virus wa korona kwa asilimia kubwa. Kwasababu zimejaribiwa kupewa kwa watu walioathirika na wamepona kabisa na kesi zao zilikuwa ni sugu. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kutafuta suluhisho na kinga thibiti. Habari hiyo ikitolewa na Jarida la japan linalojulikana kama japantimes.
Kwa habari kamili binya kiungo kifuatacho
Binya hapa
Tahadhari zinahitajika kuchukuliwa
1. Taarisha ndoo yako ya maji na uchanganye na Dittol ili ukirudi nyumbani uoshe mikono kwa maji hayo.
2. Jaribu kutopeleka mikono usoni mara kwa mara.
3. Epuka kusalimiana kwa mikono au kukumbatia
4. Oga maji yenye kuchanganywa na Dittol kabla kuingiliana na kufanya mapenzi.
5. Vaa glavzi kwenye mikono na tinga shati ya mikono mirefu ukienda katika shunguli zako.
6. Kaa mbali na watu unaowahisi wanakohoa au wana dalili za mafua.
7. Epuka visababisho vyote vinavyoanzisha mafua. Kama vile vumbi n.k
8. Epuka kula wanyama pori kwa sasa kama vile nguruwe mwitu, nyoka, mende, popo(Bat) n.k
9.Epuka kugusana kimwili na mtu mwengine hasa kwenye dalala na mwendo kasi.
10. Ukihisi dalili yoyote ya ugonjwa huu tafadhali jisalimishe hospital kwa kuokoa wengine.
DALILI ZA CORONA VIRUS
1. Homa inayoambatana na baridi kali.
2. Homa inayoambatana na mafua makali.
3. Kuhisi unaishiwa na pumzi mara moja au kupata tabu katika kuvuta hewa.
4. Kikohozi na homa kali.
5. Kuhisi mwili unakwisha nguvu na kuchoka mno ikiambatana na homa kali.
Tunamuomba Mungu atuepushe na Janga hili kwa sote . Ameen
NOTE: Ijulikane ya kwamba mask huvaliwa na watu walioathirika tu. Ili wasiambukize watu wengine.
UPDATED