Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Poleni kwa majukumu ya kila siku ndugu zangu, lakini pia tusichoke kujikinga na hili janga jipya Covid-19 au Corona, haya ni mawazo ambayo nafikiria yanaweza kuwa msaada zaidi kama tukichukua hatua kabla ugonjwa haujaenea sana, sio mwandishi mzuri kwenye mapungufu mnivumilie.

Nikitazama majirani zetu naona wamechukua hatua madhubuti pamoja na kufunga mipaka ya nchi zao lkn tanzania mpaka sasa tumefunga shule na vyuo pamoja na kusisitizwa kunawa mikono na Sanitaizer au sabuni.

Rwanda huruhusiwi kusafiri ulipo kwenda mkoa mwingine, nadhani kwa sasa Tanzania inaitaji kuchukua hatua hii, Maambukizi makubwa kwa sasa yapo DSM na Zanzibar lakini wenzetu Zanzibar wamefunga mipaka yao hatakiwi mgeni yeyote kwenda kutembea Zanzibar.

Kwakuwa wagonjwa wengi wapo DSM kuna haja wakazi wa DSM wazuiwe kusafiri na kutotoka nnje ya DSM kama moja ya tahadhari, kama unadharura ya kutoka basi ukae karantini kwa gharama zako na siku 14 zikiisha uruhusiwe kusafiri, hivyo hivyo kwa mikoa iliopakana na Mipaka ya nchi jirani, kuliko kuja kuwekwa karantini nchi nzima na kuzuiwa kutoka nnje ni bora hili lifanyike, najiuliza kuna watu hawana kipato cha kueleweka wataishi vp,kuna mtu anaondoka asubui jioni anakuja na mboga familia ile huyu ataishije? Hapa tunaweza tukajikuta tuna pambana na magonjwa mawili la njaa na Corona nawakilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninashauri baa zote zifungwe maana huko uangalifu/u makini kwa waliowengi sio wa kutosha
Samahanini kwa wadau wenzangu wa kupiga vyombo.

Pia msongamano uliozidi kwenye daladala udhibitiwe, yaani abiria wasisimame.
 
Funga bar
Funga migahawa
Funga makanisa
Funga misikiti
Funga masoko yasiyo ya chakula
Funga mipaka


Tia vikwazo vya kusafiri kwa DAB na wananchi wake
 
Hata mimi nilimwambia mshkaji wangu leo kwamba bora wazuie watu kusafiri kutoka mikoa iliyoathirika kwenda mikoa salama ili kuzuia ugonjwa kusambaa mikoa yote hali itakayopelekea kufungwa nchi nzima huko mbeleni.
 
Kuna uzi niliona title ikisomeka "moderator wa JF wana uwezo mdogo mno wa kufikiri" nilipotaka kufungua nilikuta ushafutwa.

Naanza kutilia shaka hili🤔
 
I tend to agree, shame on CIA and FBI for not detecting this in advance.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utafiti wa hivi karibuni, umeonesha yafuatayo:

1) Wazee bado ndio wanaoongoza kwa vifo lakini uzee siyo sababu pekee.

2) Wanaume ni waathirika zaidi wakilinganishwa na wanawake.

3) Ulikuwa na afya ya namna gani kabla ya kupata coronavirus, ni sababu kubwa bila ya kujali umri wako.

4) Huko China, 80% ya waliofariki walikuwa kwenye umri wa miaka ya 60.

5) Huko Utaly, 80% ya waliofariki walikuwa kwenye umri wa miaka ya 70 na zaidi.

6) Wanaopata coronavirus wakiwa na umri chini ya miaka 50, kati 10 na15% wanakuwa wagonjwa wagonjwa sana au wagonjwa wa kadiri (seriously sick or moderately sick).

7) Watu wa umri wa kati, hata wakinusurika, huwa wanalazimika kukaa wiki kadhaa hospitalini wakitibiwa.

8) Ufaransa, wagonjwa 300 wa mwanzo waliolazwa ICU, walikuwa na umri chini ya miaka 60.

9) Takwimu za Italy zinaonesha kuwa 25% ya waliopatwa na Coronavirus walikuwa na amri kati ya miaka 19 - 50.

10) Spain, theluthi 1 ya wagonjwa wake wote ni watu wenye umri chini ya miaka 44

11) Marekani, 29% ya wagonjwa wake ni watu wenye umri kati ya miaka 20 - 44

12) Huko China, mtoto mmoja wa miaka 14 alifariki; na watoto wanaopata ugonjwa huu, 6% wanakuwa wagonjwa sana (seriously ill).

13) Wengi wa wanaokufa huonesha kupata nafuu, na baada kama ya wiki moja hivi hali zao hubadilika ghafla na kuzorota (deteriorating, experiencing organ demaging inflamation)

Wataalam wanashangazwa na sababu ya wanawake kutoathirika zaidi. Lakini utafiti uliofanywa wakati wa SARs, unaonesha kuwa wanaume wanaathirika zaidi kutokana:
1) Uvutaji sigara
2) Hormone ya Estrogen inaoenekana kuwasaidia wanawake.

Mpaka sasa, huko Ufaransa, theluthi 2 za waliolazwa kutokana na Coronavirus ni wanaume.

Hii ni sehemu ya matokeo ya utafiti uliofanywa na:

AP Writers - Nicole Winfield (Rome), Maria Cheng (London), Angela Charlton (Paris) katika utafiti wao walioupa Kichwa Cha Habari 'Age is not the only risk for severe coronavirus disease.

Utafiti huu, kwa haraka, unaendana na picha ya hapa kwetu (japo sample bado ni ndogo sana). Waathirika wetu karibia wote mpaka sasa ni wenye umri chini ya miaka 50.
 
Lakini pia tutofautishe kati ya watafiti na watoa taarifa na wasambazaji wa matokeo ya tafiti. Hapa watafiti ni waliotajwa, wengine wote tunatoa au kusambaza taarifa za utafiti, ambalo ni jambo muhimu sana kwa kila mmoja wetu.
kuna watu wapuuzi sana ni wale wavivu wa kusoma wavivu wa kujifunza mapta
article za uchunguzi kila siku zinatolewa na wataaramu wanaokaa maabara ama eneo wakifanya chunguzi tena hutumia gharama kubwa ya pesa ili tu kukuletea habari za mabariko mapya ktk maisha.

sasa wewe unasema ngoja nishare na wenzangu unakutana na mpuuzi km huyo asiyependa kusoma na kujifunza mapya anaanza kuandika yasiyo na tija
wkt hayo maandiko yapo katika SITE za kuaminika ninvilentu unaamua kutafasiri kwa kiswahili ili habari ieleweke.

ni juzi tu nilikuwa duka la dawa nanunua dawa sasa akamwambia mteja mmoja alikuwa anamuuzia dawa za UTI baada kumuuzia kuwa anywe maji mengi Mm nikapinga nikamwambia kunywa maji kulingana na shughuri unazofanya na uhitaji wa mwili wako muhimu jitahidi usikae na njaa muda mrefu na jitahidi akae sehemu yenye hewa nzuri ili dawa zisimchukue sana.

akasema km huyo tatizo wabongo wataalamu wengi nikambwambia wewe mfamasia lkn hujifunzi mapya nikachukua ile dawa nikatoa kikaratasi cha ndani nikaanza kumsomea yule mgonjwa side efect na angalizo km ana tatizo fulani zile dawa asitumie km mjamziti na magonjwa mengine kisha nikamuuliza haya kakuambia au amekupa tu dawa na kukuambia tu unywe maji mengi then nikamuuliza haya nimesema mm kujifanya mtaalam au yameandikwa humu.

nikamwambia mambo mengne kwa hawa madocta wa kibongo unatakiwa ujiongeze ama sivyo wanakuletea matatizo nikamwambia km ligha inapanda.

soma mwanzo mpk mwisho halafu uone kuna sehemu wamesema kunywa maji mengi ukinywa dawa hii hvyo nikamshauri dada zingatia kura na kupumzika zaidi unapotumia hizi dawa kunywa maji kawaida tu kadri mwili unavyotohitaji maji na namna unavyotoa jasho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…