Wasalaam,
Nitoe pole kwa ndugu zetu waliofikwa na misiba kutokana na gonjwa hili hatari ulimwenguni kwa sasa.
Pia nitoe pole kwa wote wanao ugua ugonjwa huu, mwenyezi Mungu awaponye kwa uweza wake.
Tatu na ndio point yangu inaposimamia, ni kwamba dunia haina budi kutambua kuwa, yupo mtawala wa HAKI atawalaye juu ya tawala zote za DUNIANI.
Yeye akitaka jambo, huwa, haijalishi nchi yenu inawataalamu kiasi gani, mna jeshi kubwa kiasi gani, mna pesa kiasi gani au hata mnaogopwa kiasi gani.
Corona virus inausumbua ulimwengu uliojaa wanaojiita superpowers na wengineo.
Corona ime-prove kwamba hata pesa sio jawabu la mambo yote, kwenye uhai pesa haina thamani tena, kumbe kiburi cha mwanadamu ni kwa sababu ya AFYA aliyonayo tu.
Ni wakati sasa wa kufanya TOBA, na kutambua kuwa yupo Mungu ambaye kila goti lapaswa kupigwa kwake! Kwani uweza, na nguvu na utukufu vyote ni vyake yeye.
Tazama mataifa yenye majeshi ya kutisha pamoja na vifaa vya kivita vya maanangamizi, bado majeshi na vifaa hivyo havina msaada katika kuokoa uhai wa watu wao.
Mungu ibariki Tanzania na kuilinda Corona isituue in Christ Jesus name AMEN.
Sent using
Jamii Forums mobile app