Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Ule wakati wa ebola huku africa nao wazungu huko walikuwa wanachukuliaje?
 
Mtaani kwangu wanasema korona ni ya mzungu sisi mazoezi kama kawa kama dawa
 
Latest data hizo, tusipoangalia tutapukutika.
Screenshot_20200331-215856.jpg
 
Hii Corona ni kama vita ya 3 ya Dunia, tofauti yake ni kwamba Dunia nzima inapigana dhidi ya adui mmoja Corona.

Lkn, all in all ni bado athari zake ni zaidi ya vita vya kawaida. Watu wanakufa, hakuna uzalishaji, nchi zimesimama.

Hapa akili ya kiuchumi na kiafya zaidi ndio inahitajika kwa Kiongozi wa juu kitaifa, huku wanasayansi wakiendelea kufanya yao kwenye maabara.

Ok, assume wewe ndio mwenye nafasi ya Kuongoza Taifa lako katikati ya vita hii. Tuambie wewe ungefanyaje?
 
Mimi ningefanya yafuatayo kwa nchi kama Tanzania:

1. Nahutubia Taifa. Natuma statement mbili tu kwa raia wangu. Nawaambia Corona inaua na inasambaa Dunia nzima, kila mmoja kwa nafasi yake afahamu kuhusu hili, pili nawaambia kipaumbele cha maisha yetu sasa ni Kula ili tuishi pamoja na Matibabu ili tupone Kwa wale wanaoumwa ama kuugua magonjywa ya aina yoyote tofauti na Corona. Mengine yote tuachane nayo kwa sasa, hadi tupate muelekeo sahihi wa kuikabili hii Corona.
 
Katika hili la Corona ,kuna wengine watakuwa wameweka nadhiri kwamba hata nikiona dalili zote siendi kupimwa ili nife na wengine nisife pekee yangu.

Mawazo Kama haya kwa baadhi ya watu hayakosekani hivyo Serikali inatakiwa iweke hata sheria ya kuwashtaki watu watakaojulikana na Corona na hawakutaka kupima kwa hiari wakaambukiza wengine.

China imeweza kiudhibiti Corona haraka kwa sababu wachina wanaijua Serikali yao na hata walipopewa amri ya kutotoka nje wakatii bila malalamiko kwa sababu wanajua Serikali yao lakini huku nchi za Afrika kila mtu anajifanya anajua na wengine wanapopewa amri wanaenda kinyume ili kuona Nini kitatokea. Tubadilike jamani sio kulalamika tu.
 
Mzee kasema tusiogope, tuchape kazi tu. Hivi "vimafua" vitapita tu.
 
Wasalaam,

Nitoe pole kwa ndugu zetu waliofikwa na misiba kutokana na gonjwa hili hatari ulimwenguni kwa sasa.

Pia nitoe pole kwa wote wanao ugua ugonjwa huu, mwenyezi Mungu awaponye kwa uweza wake.

Tatu na ndio point yangu inaposimamia, ni kwamba dunia haina budi kutambua kuwa, yupo mtawala wa HAKI atawalaye juu ya tawala zote za DUNIANI.

Yeye akitaka jambo, huwa, haijalishi nchi yenu inawataalamu kiasi gani, mna jeshi kubwa kiasi gani, mna pesa kiasi gani au hata mnaogopwa kiasi gani.

Corona virus inausumbua ulimwengu uliojaa wanaojiita superpowers na wengineo.

Corona ime-prove kwamba hata pesa sio jawabu la mambo yote, kwenye uhai pesa haina thamani tena, kumbe kiburi cha mwanadamu ni kwa sababu ya AFYA aliyonayo tu.

Ni wakati sasa wa kufanya TOBA, na kutambua kuwa yupo Mungu ambaye kila goti lapaswa kupigwa kwake! Kwani uweza, na nguvu na utukufu vyote ni vyake yeye.

Tazama mataifa yenye majeshi ya kutisha pamoja na vifaa vya kivita vya maanangamizi, bado majeshi na vifaa hivyo havina msaada katika kuokoa uhai wa watu wao.

Mungu ibariki Tanzania na kuilinda Corona isituue in Christ Jesus name AMEN.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunakumbushwa tu kuwa maisha ya hapa duniani sio ya kudumu na kwamba maisha yetu hasa ni katika roho.
 
Ndugu zangu tumuombe Muumba wa mbingu, ardhi na vilivyovyomo baina baina ya mbingu na ardhi atuondolee huu mtihani wa CORONA hebu tuangalie mataifa yenye kila aina ya technology yanavyoteketea vip sisi hapa TZ na Africa kwa ujumla tutasalilmika. Eeh Allah turehemu sisi na familia yetu katika hili janga Corona Virus Live Tracker
 
Back
Top Bottom