Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Asante sana mkuu
Waga hulali mkuu???
Maana tunafrahia sana update zako especially mimi na pia afya yako ni ya maana zaid
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama atakuwa na Corona, TUMEKWISHAAA!!!
Let's hope kuwa mgonjwa huyo yupo salama.

Mpaka sasa bado majibu ya vipimo vyake hayajapatikana. Tuendelee kusubiri.
 
Wa Egypt vipi majibu yametoka?
Vipimo vyake vya mara ya mwisho vilionesha negative, ila kama nilivyosema hapo awali kuwa majibu ya vipimo alivyofanyiwa yana utata.

Kuna uwezekano kuwa mtu huyo hakuwa na maambukizi kabisa ila makosa ya kivipimo yalifanyika.
 
Asante sana mkuu
Waga hulali mkuu???
Maana tunafrahia sana update zako especially mimi na pia afya yako ni ya maana zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani nawe pia kwa kuendelea kufuatilia taarifa hizi.

Kuna wakati huwa nalala na pia kuna wakati huwa silali. Yote hayo yanafanyika kwa muda na wakati maalumu.

Afya ni jambo la maana zaidi, ni kweli!
 
UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 87 vimetangazwa nchini humo na kufikisha jumla ya visa 433 hadi sasa huku idadi ya vifo kutokana na virusi vya COVID-19 ikiwa ni viwili (2) nchini humo hadi hivi sasa.
 
UPDATE: Iran imeripoti visa vipya 10 pamoja na kifo kipya kimoja (1) kutokana na virusi vya Corona.

Hadi sasa visa takribani 28 pamoja na vifo vitano (5) vimeripotiwa nchini humo.
 
UPDATE: Japan

Ndani ya saa chache zilizopita, visa vipya vipatavyo 24 vimeripotiwa nchini humo. Mpaka sasa idadi ya visa vyote nchini Japan imefikia 129.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…