Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Watafiti wanadai kuwa kuna uwezekano wa maambukizi mengi zaidi ya kama watu 44,000 mjini Wuhan, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko idadi rasmi inayoripotiwa hivi sasa.

====

Researchers say as many as 44,000 people could be infected with the coronavirus in Wuhan, far more than official figures suggest. [SCMP]
 
Ujerumani: Visa vya 'Coronavirus' vimekwishafikia vinne (4) nchini humo katika jimbo la Bavaria.

====

UPDATE: Germany confirms three further cases of coronavirus.

The disease, which has killed nearly 100 people in China, has now infected four people in Bavaria. All four instances are thought to be connected to the recent visit of a Chinese work colleague to the area. [DW]
 
Ethiopia: Watu wanne wanaoshukiwa kuwa na virusi hatari vya Corona wametengwa na wanafanyiwa uchunguzi zaidi katika mji mkuu wa Addis Ababa.

Tangu Jumatano iliyopita abiria wote wanaowasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Bole kutoka China wamekuwa wakifanyiwa uchunguzi kubaini kama wanaambukizwa virusi hivyo.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Addis Ababa, Waziri wa Afya wa Ethiopia Dkt. Liya Tadesse, amesema kuwa wagonjwa wanne wanaoshukiwa kuwa na virusi hatari vya corona wametengwa na wanafanyiwa uchunguzi zaidi.

Wagonjwa wote ni raia wa Ethiopia na kwamba watatu kati yao ni wanafunzi kutoka chuo kikuu cha eneo la Wuhan nchini China, ambako ni chimbuko la mlipuko wa virusi hivyo.

[BBC]
 
Ethiopia: Maafisa wa afya nchini humo wanasema kuwa sampuli ya damu imetolewa kwa watu wanne (4) wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Corona na sampuli inatarajiwa kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
 
Tayari ndege inayobeba raia wa Kimarekani waliokuwepo mjini Wuhan nchini China imekwisha ondoka na kuelekea nchini Marekani.
 
BREAKING: Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona imeongezeka kutoka 106 hadi 131.

Taarifa ya vifo vipya 25 ni kutoka katika mkoa wa Hubei pamoja na visa vipya takribani 840 kwa siku iliyopita, jana pekee (Januari 28).

====

JUST IN: China coronavirus: death toll reaches 131 as number of cases surpasses that of Sars.
  • There are 840 newly confirmed cases in Hubei province, Chinese health authorities say.
The total death counts with the new coronavirus infection are all reported in mainland China, with 125 in Hubei province, where the outbreak began, and six in other provinces. About 3,300 people are hospitalised in Hubei province, with more than 20,000 being observed for infection. [SCMP]
 
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mpaka sasa;
  • Idadi ya visa vyote duniani ni 5,572.
  • Idadi ya vifo mpaka sasa ni 131.
  • Idadi ya wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi ni 1,109.
 
MPYA: Marekani inafikiria kusitisha safari za ndege kati ya Marekani na China. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Marekani, White House.

====

BREAKING: White House considering to suspend flights between the U.S. and China. [CNBC]
 
Ethiopia: Maafisa wa afya nchini humo wanasema kuwa sampuli ya damu imetolewa kwa watu wanne (4) wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Corona na sampuli inatarajiwa kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hapa ndo tatizo lilipo. Huu ugonjwa mtu anatakiwa aachiwe huru baada ya 14 days quarantined.....

Afrika huu ugonjwa utaripuka baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
China kupitia Wizara ya Afya imetangaza kuwa itaanza kutoa ripoti rasmi kuhusiana na virusi vya Corona mara mbili kwa siku.

Mpaka sasa China imekuwa ikitoa ripoti hizo mara moja tu kwa siku.

====

China's National Health Commission will start releasing coronavirus updates twice a day, according to state-run media.

Until now there was only 1 national update a day.
 
Ndege yenye raia wa Kimarekani kutoka Wuhan nchini China inategemewa kutua jijini California mnamo Jumatano lakini swali kubwa limeibuliwa;

Hata kama abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hawakuambukizwa, Je kuna haja ya kuwatenga?

====

An airliner from Wuhan, China, is expected to land in California on Wednesday, bringing US citizens who could possibly be infected with deadly coronavirus. Health officials face a tough question: Even if passengers are healthy, should they be quarantined? [CNN]
 
Raia 206 wa nchi hiyo wamekwisha kuondolewa kutoa maeneo ya Wuhan nchini China na wamekwisha wasili jijini Tokyo, kwa mujibu wa maafisa kutoka nchini Japan.

Takribani raia 450 zaidi wa Kijapani bado hawajaondolewa kutoka eneo hilo la China lililoathiriwa zaidi za virusi hatari vya Corona.

====

UPDATE: 206 Japanese nationals who were evacuated from Wuhan, China, arrived in Tokyo on Wednesday morning via a chartered flight operated by ANA, according to Japanese officials. About 450 more Japanese citizens have not departed yet. [CNN]
 
Hapo awali, kulikuwa na taarifa kuhusu mpango wa Marekani kusitisha safari za anga kati ya nchi yake na China lakini taarifa iliyotoka hivi punde ni kuwa Marekani imeamua kutositisha safari hizo angalau kwa sasa.
 
Kuna mabadiliko mengine: Ripoti mpya inasema kuwa idadi ya vifo imefikia 132 huku idadi ya visa vyote ikifikia 5,974 mpaka mwishoni mwa siku ya jana Januari 28. [Reuters]

Ripoti za siku ya leo zitatolewa hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom