Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Korea Kusini

Visa vipya 334 vimeripotiwa nchini humo na kufikia jumla ya visa 1,595.

Kifo kipya (1) kimeripotiwa nchini humo na kufikisha jumla ya vifo 13 hadi sasa.

Mazoezi ya kijeshi kati ya nchi hiyo na Marekani yaliyopangwa kufanyika hivi karibuni yameghairishwa mpaka hapo baadaye kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo.
 
UPDATE: Wizara ya afya ya China imeripoti visa vipya 433 pamoja na vifo vipya 29 nchini humo.

Ongezeko hilo linapelekea idadi ya visa vyote ulimwenguni kufikia 82,147 huku idadi ya vifo vyote kutokana na virusi vya Corona ikifikia 2,772 duniani kote kwa mujibu wa takwimu rasmi.
 
Asante kwa update mkuu. Hivi kwa level ya janga China inaweza kuwa imeomba msaada WHO ,hivyo tukapata takwimu sahihi? Kuna mahojiano na mchina USA, kasema hali ni mbaya sana China maambukizo na vifo yapo digit za million

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli hizi habari nimezisikia. Inadaiwa idadi ya vifo ni kubwa mnoo japo china imekua ikitoa takwimu ndogo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani mmepata JIBU
Kwanini marekani anamuogopa muajemi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Denmark's first case of coronavirus

Denmark's TV2 says one of its reporters has tested positive for coronavirus after going on holiday in northern Italy. He developed symptoms on Wednesday morning.
 
mwamba hongera sana kwa kazi ya kutuhabarisha ila samahani ningependa kufahamu izi taarifa huwa unazipata wapi na kuhakikisha kuwa ni za kweli
 
Wachina wanaoingia Tz ni wengi zaid ila mamlaka husika hawasemi, Bora Kenya wameitangazia dunia, hiyo Ndege ingetua KIA wala msingesikia habari yeyote
Nimejaribu kutafakari nimekosa majibu kwann wakenya wanataka kuhatarisha maisha yetu jamani hv umoja wa east africa hawaliona hili au

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Algeria

Serikali ya nchi hiyo imesema haina mpango wa kuzuia maandamano ya umma au kusitisha safari za ndege kwenda Italia, baada ya nchi hiyo kuripoti kisa cha kwanza cha Corona kwa mwanaume ambaye ni raia wa Italia.

Mkurugenzi wa kuzuia na kupambana na magonjwa ya kuambukizi nchini Algeria, Djamel Fouar amesema maafisa wanawafuatilia kwa karibu watu wote waliokuwa na mawasiliano na mtu huyo mwenye umri wa miaka 61. [DW]
 
Nimeshangaa kuna watu wamekupa like aisee.

We kama umechoka kuishi ni wewe peke yako tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…